Rais Magufuli: CCM itatawala milele na milele! Wasioipenda watapata tabu sana

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema chama hicho kitaendelea kutawala milele kwasababu hakuna mbadala wake na wanaohangaika ‘watapata tabu sana’.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani jana, Rais Magufuli alisema CCM ipo na itatawala milele na kwa yeyote anayefikiri tofauti ‘atapata tabu sana’.

“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele. Kwa wanaohangaika watapata tabu sana siku zote, siku hakuna mbadala ni CCM hadi milele.

“Wanachama wa CCM tembeeni kifua mbele tumeamua kuleta Tanzania mpya inayowapigania wananchi hasa wanyonge ili waweze kushiriki katika maendeleo,” alisema Dk. Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alizitaka nchi sita zinazoshiriki kwenye ujenzi na usimamizi wa chuo hicho kuwa mfano katika kuwajenga viongozi wapya watakaoinua upya uzalendo barani Afrika.

Alisema chuo hicho kinachojengwa kwa ushirikiano baina ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama sita vilivyoshiriki harakati ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika kitakuwa na jukumu la kuwanoa vijana katika masuala ya itikadi na uongozi.

“Katika zama hizi, tunahitaji chuo hiki kitusaidie kuzalisha akina Julius Nyerere, Samora Machel, Agustino Neto, Sam Nujoma, Robert Kaunda na akina Robert Mugabe wengi.

“Chuo hiki kitakuwa kichocheo cha kujenga ushirika mpya wa kupigania maendeleo yetu ya kiuchumi. Suala hili linawezekana hasa ikizingatiwa vyama vyote washirika vina misingi ya kiitikadi inayofanana,” alisema.

Alieleza kuwa hana wasiwasi kwa kuwa kuanzishwa kwa chuo hiki kinachojumuisha vyama vilivyoshiriki harakati itakuwa ni kichocheo cha kushirikiana katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

Chuo hicho kinajengwa kwa ushirikiano wa vyama vya African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, FRELIMO cha Msumbiji, MPLA cha Angola, ZANU-PF cha Zimbabwe na SWAPO cha Namibia.

Vyama hivyo vilipata msaada mkubwa kutoka Tanzania chini ya iliyokuwa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, iliyoongozwa na marehemu Hashim Mbita.

“CCM chini ya Hayati Mwalimu Nyerere ndiyo iliyosimamia kuwahifadhi viongozi wa vyama hivyo na kuwapa mafunzo ya kiitikadi na kijeshi, hatimaye walifanikiwa kuzikomboa nchi zao kutoka kwa wakoloni,” alisema.

Alishauri pamoja na lengo lake kuu la kufundisha itikadi na uongozi mara kitakapokamilika miaka miwili ijayo, ni vyema chuo hicho kikaangalia namna ya kuongeza kozi nyingine zaidi za masuala ya maendeleo, ili kuhakikisha nchi zote zitakazonufaika zinafikia maendeleo ya kweli.

Ushiriki wa China

Akizungumzia ushiriki wa China katika ujenzi wa chuo hicho, Rais Magufuli alisema nchi hiyo chini ya chama rafiki cha Kikomunisti cha China (CPC) itatoa mchango wake katika kufundisha wakufunzi na wahadhiri.

Alisema anatoa shukrani kwa chama cha CPC ambao walikubali kujenga chuo hicho kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 45, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 100 za Tanzania.

Alisema Tanzania ni wanufaika wa misaada ya China ikiwamo Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na mingine, akieleza kuwa huu pia ni msaada mkubwa wenye heshima kubwa na kuahidi kuendelea kuuenzi urafiki.

Majukumu

Alisema kwa sasa chuo hicho kitakapoanza kitatoa mafunzo ya muda mfupi kuazia kozi za miezi mitatu, muda wa kati na kozi za muda mrefu za miaka mitatu.

MWITIKIO:

1) Rais Magufuli alikosea kutamka kuwa CCM itatawala milele

2) Tundu Lissu akosoa kauli ya Rais Magufuli kuwa CCM itatawala milele
 
Ngoja ajidanganye huyo mkolomije kutokana na kiburi alichonachio cha kuzungukwa na vifaru vya kijeshi na magari ya washawasha........

Lakini anachosahau ni kuwa historia inaeleza wazi kuwa katika dunia hii hakuna serikali yoyote duniani hata kama ina nguvu kubwa za kijeshi, ambayo imewahi kuushinda Umma uliojizatiti!
 
Huu ni ukweli mchungu.

Kama wale tunaowategemea kisiasa kuitoa CCM madarakani lakini mpaka sasa hawajajua tofauti ya uanaharakati na chama cha siasa basi inabidi tuondokane na fikra kuwa CCM itaondoka madarakani.

Haishangazi kuona wajinga fulani wanashangaa pale mwanaharakati anapokubali uteuzi kutoka Ikulu kwa sababu wanadhani wanaharakati ni mpinzani wa serikali ya CCM.
 
Sasa kama polisi ni wako, umepika marufuku watu kusema na kuhoji unataka kujipima vip kuwa unakubalika? Wewe hujawahi kucheza hata mechi ya kirafiki unajifanya eti bingwa...

Weka usawa kwenye siasa, ruhusu tume huru, acha kuwafanya makada kuwa watumishi wa tume halafu ndio useme.

Hakuna fedheha kubwa kama mtu mzima kukosa aibu, CCM wamekosa aibu ndio maana nchi hii inaendelea kuwa masikini.

Rais anaona fahar kusikia wananchi wake ni masikini, biashara zinakufa, utu unapotea, watu wanauwawa hovyo kwa visingizio vya kunyoosha nchi wakati yeye alikuwa sehemu ya kupindisha.

Mungu msaidie Rais wetu, mpe busara na hekma kwani naye ni binadamu dhaifu kama binadam wengine asiendelee kupotoka mpaka akaingia kwenye kufuru zitakazomuangamiza.
 
Ngoja ajidanganye huyo mkolomije kutokana na kiburi alichonachio cha kuzingukwa na vifaru vya kijeshi na magari ya washawasha yanayomzunguka......

Lakini anachosahau ni kuwa histiria inaeleza wazi kuwa katika dunia hii hakuna serikali yoyote duniani hata kama ina ngivu kubwa za kijeshi, ambayo imewahi kuushinda Umma uliojizatiti
Tatizo ni huo umma uliojizatiti.
 
Anafanya kufuru huyu!

Kwani hajui kuwa kila chenye mwanzo duniani ni LAZIMA kiwe na mwisho?

Huyu anajidanganya kutokana na vifaru na magari ya washawasha yanayomzunguka, ambayo anajua wakati wowote yeye akiwa Commander in Chief, ataamrisha na viende popote anapotaka yeye!
 
Sasa kweli hata ukiangalia kuna upinzani upi wa kuitoa ccm madarakani? Msije mkaniambia chadomo

Sababu kwao kushinda kiti cha udiwani saivi ni kama kulokota embe chini ya mgunga
 
Kuna mtoto mtaani kwetu mchokozi kweli,akipigwa anaenda kusema kwa mama
 
Ngoja ajidanganye huyo mkolomije kutokana na kiburi alichonachio cha kuzungukwa na vifaru vya kijeshi na magari ya washawasha........

Lakini anachosahau ni kuwa historia inaeleza wazi kuwa katika dunia hii hakuna serikali yoyote duniani hata kama ina nguvu kubwa za kijeshi, ambayo imewahi kuushinda Umma uliojizatiti!
Tatizi huo umma uko wapi hapa tz? Huo umma upapenyea wapi na katiba hii? Viongozi wana CHADEMA wanashinda kiguu na njia Kisutu kwasababu ya katiba hii hii inayowapa wenye mamlaka kufungua kesi zisizo na miguu wala mikono. Tuendelee tu kujifariji na historia za nchi nyingine wakati hatujui katiba zao zilikuwaje.
 
Back
Top Bottom