TANZIA John Livingston Mwakipesile, Mbunge wa zamani wa Kyela afariki dunia

JAMANI HAWA WATU WANAKUFA NA NINI??MBONA VIONGOZI HASA WALE WASTAAFU NA WENYE UMRI MKUBWA WANAONDOKA SANA!???
 
Simfahamu. Apumzike kwa amani. Na familia na wapendwa wake Mungu awape5faraja na nguvu wakati huu mgumu wanapitia.
 
Alituchelewesha sana. Chanjo tungeanza nazo mapema wazee hawa wangekuwa hai leo. Tunaendelea kupoteza watu leo kwa ajili yake.

Umenisoma ewe kajamaa?
Waulize India wachanja mapeeema lakini delta aliupiga mwingi tuuu.Lazima tutambua saa na majira ya sasa, tumrudie Mungu, tuombee bila kuchoka na yeye atatusikilizawaka jana tuliomba sasa hivi tinaona kuomba ni ushamba eti siyo sayansi.
 
Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered. Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy. We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage. The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen. Godfrey B. Mramba.
Mshana Jr , hapa tunaomboleza msiba wa John Mwakipesile, sio Mramba kaka.
 
Waulize India wachanja mapeeema lakini delta aliupiga mwingi tuuu.Lazima tutambua saa na majira ya sasa, tumrudie Mungu, tuombee bila kuchoka na yeye atatusikilizawaka jana tuliomba sasa hivi tinaona kuomba ni ushamba eti siyo sayansi.

India wameumudu ugonjwa baada ya kuwekeza zaidi kwenye kuchanjwa watu wao.

IMG_20210808_181807_546.jpg

Kwenye zoezi hilo walilazimika kuacha kuacha kusafirisha chanjo nje.

Danganyeni wasiojua.
 
Kina
India wameumudu ugonjwa baada ya kuwekeza zaidi kwenye kuchanjwa watu wao.

View attachment 1895401

Kwenye zoezi hilo walilazimika kuacha kuacha kusafirisha chanjo nje.

Danganyeni wasiojua.

Kinachosaidia sasa hata waliochanjwa wa poneapo ni herd immunity tu and nothing else. JPM akili kubwa aliliona hili bali hamtaki kukiri kwa vile kulikuwa na agenda ya kumpaka oil chafu iliyoshindwa kwa aibu kuu.
 
Aliyekuwa mbunge wa Kyela na baadae mkuu wa mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile amefariki dunia

Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 17, 2021. Marehemu Mwakipesile aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kyela (1995 hadi 2005) na kisha kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwaka 2006 hadi alipostaafu mwaka 2011.

RIP

====

Mbeya. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

"Tumepata taarifa na sasa naelekea nyumbani kwa marehemu kujua taarifa zaidi na nitaweza kukuunganisha na familia ya marehemu kwani mimi sio mzungumzaji wa familia," amesema Mlawa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kwamba ni pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa hakuwa na taarifa za kuugua kwa Mwakipesile.

"Ni kweli nimepokea taarifa za msiba huo mkubwa wa baba yetu na kada wa chama. Chama tunataratibu zetu, tutashirikiana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kumsitili marehemu Mwakipesile,” amesema mwenyekiti huyo.

Princes Mwaihojo, mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya amesema watamkumbuka marehemu kwa namna alivyoupigania mkoa huo kuvutia na kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.

Chanzo: Gazeti Mwananchi
1629191855012.png

Huyu John Mwakipesile atakumbukwa kwa KUIUA CCM Mkoa wa Mbeya.!!
Nasema hivyo kwa kujiamini.
Alikuwa sehemu ya mtandao wa JK.
Na alitumwa mahsusi kumdhibiti Profesa Mark Mwandosya ambaye nyota yake wakati huo ilikuwa iko juu.

Huyu Mwakipesile alihakikisha wale wanaomuunga mkono Mwandosya wanashughulikiwa na kuondolewa CCM katika nyadhifa zote.
Ilifikia Mwakipesile alidiriki kutaka kushiriki kumtoa Mwandosya katika U NEC katika uchaguzi wa CCM mwaka 2007, kwa kumtumia Thomas Mwan'gonda mtoto wa Kachero No 1, Abson Mwang'onda..
Ilishindikana kwa vile bado Mwandosya alikuwa na nguvu ndani ya CCM.

Wana CCM Mbeya hatujalisahau hilo , na kiasi hatujalisamehe kwa uozo ule.

Mtafaruku wa Mwandosya Vs Mtandao ulukuwa mkubwa sana Mbeya.
Hata alipokuja Waziri Mkuu Lowasa kutembelea Mbeya , vijana walimshabikia Mwandosya kwa kumwita. "raisi...raisi...raisi...!", jambo lilowaudhi sana mwanamtandao!

Matokeo ya kuivuruga CCM Mbeya iliyoongzwa na Mtandao wa JK, ambapo Mwakipesile alikuwa point man, yalikuwa mabaya sana kwa CCM.
Na vijana wengi kukimbilia CHADEMA kwa kumshabikia Sugu.

CCM Mbeya bado inachechemea mpaka leo.
RIP J Mwakipesile-CCM Mtandao.
 
Aliyekuwa mbunge wa Kyela na baadae mkuu wa mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile amefariki dunia

Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mbeya, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 17, 2021. Marehemu Mwakipesile aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kyela (1995 hadi 2005) na kisha kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuanzia mwaka 2006 hadi alipostaafu mwaka 2011.

RIP

====

Mbeya. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye Serikali ya awamu ya nne, John Mwakipesile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Ismail Mlawa amesema wamepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

"Tumepata taarifa na sasa naelekea nyumbani kwa marehemu kujua taarifa zaidi na nitaweza kukuunganisha na familia ya marehemu kwani mimi sio mzungumzaji wa familia," amesema Mlawa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jacob Mwakasole naye amethibitisha kupokea taarifa za msiba wa Mwakipesile na kwamba ni pigo kubwa kwao. Ameongeza kuwa hakuwa na taarifa za kuugua kwa Mwakipesile.

"Ni kweli nimepokea taarifa za msiba huo mkubwa wa baba yetu na kada wa chama. Chama tunataratibu zetu, tutashirikiana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kumsitili marehemu Mwakipesile,” amesema mwenyekiti huyo.

Princes Mwaihojo, mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya amesema watamkumbuka marehemu kwa namna alivyoupigania mkoa huo kuvutia na kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi.

Chanzo: Gazeti Mwananchi
Rip John.
 
Kina

Kinachosaidia sasa hata waliochanjwa wa poneapo ni herd immunity tu and nothing else. JPM akili kubwa aliliona hili bali hamtaki kukiri kwa vile kulikuwa na agenda ya kumpaka oil chafu iliyoshindwa kwa aibu kuu.

😂😂😂😂😂😂😂 Hiiiiii bagosha!

Kwani wewe ni mtalaamu mbobezi wa masuala ya afya?

Umelisikia tamko la serikali kutoka kwa wabobezi wataalamu wa afya kumhusu Gwajima?

"Atawajibishwa kwa vifo vyote hata vinavyotokea sasa kutokana na upotoshaji wake kuhusiana na chanjo."

Haiyumkiniki tamko hilo litawafuatilia wahusika wa upotoshaji wote hata kama wako Chato.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom