John Kaduma!

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241
Nchi yetu imebarikiwa vipaji na Taaluma za kila aina , lakini kinachonishangaza serikali yetu ama Taasisi husika hushindwa kuvitumia vyema kwa manufaa ya jamii,
tukija kwenye la kuwaenzi watu muhimu ndani ya jamii yetu kuna wengine wanasahaulika, namzungumzia aliyekuwa mchoraji mashuhuri katika ukanda wa Afrika Mashariki Ndg John Kaduma ( RIP )

huyu jamaa aliwahi kuchora katika magazeti na majarida mbalimbali kama Sani,BONGO, kisha Tabasamu, yeye ndiye mwanzilishi wa katuni ijulikanayo kama Baba ubaya na nyingine nyingi, mbali na hayo alikuwa akichora vielelezo kwa ajili ya vitabu vya watoto.
Nimejaribu kutafuta habari zake katika sehemu mbalimbali lakini nikapata sifuri, hii inamaanisha hakuna kumbu kumbu yoyote iliyotunzwa! hivyo kama kuna mtu yeyote aliye na habari hata kiduchu kumhusu huyu jamaa tafadhali ninaomba awasilishe jukwaani. asanteni
 
Inasikitisha sana mambo kama haya yanapotokea. Lakini kwa Upande wangu sidhani kama ili kuwa na kumbukumbu za mtu fulani ambaye amewahi kuwa na umaarufu katika siku za maisha yake inahitaji watu waliokuwa nae wamuenzi.

Ni kweli kwamba kazi za sanaa za John Kaduma zilikuwa zinastahili kuenziwa na mchango wake ulitakiwa kuthaminiwa sana chapa nchini, lakini nadhani jukumu la kwanza la kuhakikisha jambo hili linafanikiwa alikuwa ni Msanii Mwenyewe.

Inapotokea kwamba katika siku za maisha yako iumeshindwa kuienzi kazi yako ni vigumu sana kwa wengine kuja kuiendeleza once you are dead and gone... As for us who were there during Kaduma's reign we will always have memories to treasure!!!
 
inasikitisha sana huyu jamaa alikuwa ni mkali usipime kwenye suara la katuni nadhan yeye ndo aliyeanzisha gazeti la bongo
kazi za jamaa ziliniinspire sana niwe mchoraj sasa kinchonisikitisha jamaa amepotea kama upepo hakuna information yeyote kumuhusu yeye likin magazeti kama bongo sani tabasam yanaweza kuprovide information flani kumhu jamii but i wonder if those magazine aare still exist cause ni masiku mengi tokea nione hayo magazeti
 
Kwa magazeti ya Bongo na Sani lazima watakuwa na Archives( nina uhakika kama wamilika hawajabilika! ) na kuhusu Jarida la Tabasamu sijaliona mtaani kwa miaka kadhaa sasa, mmiliki wake alikuwa Daudi Masasi wa mjini Iringa.
 
Kaduma pamoja na Nico Yembayo walikuwa wakali sana katika fani ya uchorani hususan magazeti ya sani na Bongo, tutawakumbuka na kuwa miss sana..
 
Unajua mmenikumbusha mbali sana,michoro ya kaduma ilikuwa kama inataka kusema.Unamkumbuka Vick katika maji mazito,sijui yule jamaa zile imaginations alikuwa anazitoa wapi.Kuna hadithi moja alichora katika gazeti la heko,"RAFIKI MKIA WA FISI" usipime mtu wangu,alimchora ticha mkuu,ukimuangalia tuu unajua kweli huyu ticha mkuu.Jamaa alikuwa mkali lazima tukubali.
 
Kwenye riwaya pia alihusishwa, kama vile kweye picha za riwaya za Simbamwene, Kivumbi uwanjani, na zile za kina insekta Fog, nk. Kweli bwana alikuwa na kipaji, kinacho hitaji kumbukumbu.
 
ni kweli umesema ''MAJI MAZITO'' umenikumbusha mbali sana kipindi hicho nilikuwa nafuatilia sana hadithi hii jinsi
Omari alivyonyanyasika kwa Mtoto Vicky, ukweli serikali haina kumbukumbu ya watu muhimu kama hawa walioweza
kuipeperusha bendera ya Tz vizuri, wabadilike sasa wasifanye vitu kwa mazoea
 
Kafariki huyu mchoraji? lini

Masikini RIP. Naomba kuuliza huyu John Kaduma amefariki lini?

...John Kaduma (RIP) aliugua na hatimaye kufariki na alizikwa kwao Iringa. Sikumbuki vizuri tarehe lakini ni kati ya 2002 -2003

Sina uhakika ni lini alifariki lakini hadi mwishoni mwa mwaka 1999 nilikuwa najua kuwa alikuwa amefariki, huenda ni mwaka huo ama kabla.

RIP John Kaduma.

Hivi huyu ndugu aliwahi kubadili jina na kuitwa "Mohammed Hussein"?

Nachojua hakuwahi kubadili jina. Jina Mohammed Hussein lilikuwa ni la kumshabikia aliyewahi kuwa mchezaji nyota wa Bandari ya Mtwara, Yanga na Simba, Mohammed Hussein "Mmachinga." Wakati John Kaduma akichora jarida la Tabasamu, crew ya jarida hilo ilikuwa ikijipigia chapuo kuwa inatumia mtindo wa wachezaji uwanjani wa 4-4-2 waliokuwa wakiuita "Samba Msele" na ndiyo maana John Mathias Kaduma alijipa jina la mcheza mpira. Majina mengine ya bandia ya John Kaduma yalikuwa,

  1. Fogasta
  2. John Black
  3. Baba Jack (Jina la bintiye Jacqueline)
  4. Tanzania One

Nikikumbuka kama wimbi la kitintale ilikuwa balaa

Wimbi la Kitintale nakumbuka aliyechora ni Chrisantus Katembo (Chris Katembo). Wakati huo naona Kaduma hakuwa na amani katika Sani hasa baada ya kufariki Said Mbwana Makatta Bawji aliyekuwa kiongozi na mtunzi wa Hadithi Mahiri kama Maji Mazito na Kizaizai iliyokuwa na akina Mayuku, Zumo, Mzee Ole, Obi, Linda na Seba.

Kaduma ameathiri sana mtindo wa uchoraji wa wasanii wengi wa Tanzania, miongoni mwao ni mimi. Nafikiria namna fulani ya kurudisha nguvu/kumbukumbu zake japo kidogo but in a modern way.

Tunawamiss Born Town, Bush Stars, Makwekwe. Tunawamiss Ndumilakuwili (Profesa), Madenge, Kipepe, Bob Mazish, Lodi Lofa, Pimbi, Mzee Mwalubadu, Kizibao, Wanzuki n.k.

Tunakumbuka kosa alilofanya Mzee Mwalubadu kulazimisha Kizibao apangwe matokeo yake akasababisha penati iliyofanya Bush Stars wafungwe. Siku hiyo Ndumilakuwili hakusema "Yan Kibadachi, Yan Shodan Kataa!"

RIP John M. Kaduma.
 
hakika ya kale ni dhahabu
 
Back
Top Bottom