alexelias
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,032
- 3,198
JJ Mbungo, Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa ndiye Mkurugenzi Msaidizi wa TAKUKURU.
Kachero huyo mbobevu alitolewa jeshini na kupelekwa Takukuru kwa mkakati maalum wa yeye kwanza ahudumu kama Mkurugenzi msaidizi huku akiendelea kuzifahamu barabara changamoto za Idara hiyo na hapo baadae aje kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu.
Inasemekana mda wa yeye kuhudumu katika hiyo Ofisi kama Mkurugenzi Mkuu umewadia.Duru zinatabanaisha kwamba toka juzi Mkuu wa Nchi anatarajiwa mda wowote kumtangaza JJ Mbungo kuwa yeye ndiye sasa bosi wa Idara hiyo.
Itoshe kumtakia kila lililo la kheri bwana JJ Mbungo katika majukumu yake mapya-tarajiwa.