John Julius Mbungo, Mkurugenzi msaidizi wa TAKUKURU 'kachero' mwandamizi aliyeandaliwa kwa muda sasa aje kuwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
JJ Mbungo, Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa ndiye Mkurugenzi Msaidizi wa TAKUKURU.

Kachero huyo mbobevu alitolewa jeshini na kupelekwa Takukuru kwa mkakati maalum wa yeye kwanza ahudumu kama Mkurugenzi msaidizi huku akiendelea kuzifahamu barabara changamoto za Idara hiyo na hapo baadae aje kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu.

Inasemekana mda wa yeye kuhudumu katika hiyo Ofisi kama Mkurugenzi Mkuu umewadia.Duru zinatabanaisha kwamba toka juzi Mkuu wa Nchi anatarajiwa mda wowote kumtangaza JJ Mbungo kuwa yeye ndiye sasa bosi wa Idara hiyo.
Itoshe kumtakia kila lililo la kheri bwana JJ Mbungo katika majukumu yake mapya-tarajiwa.
 
Kutokana na mizizi ya rushwa TAKUKURU baada ya kuhuishwa sasa inaenda kuwa msingi wa mabadiliko ya kimkakati kwa taasisi zote.
 
Diwani Athumani na Mlowola waliokuwa Wakurugenzi walijifunzia wapi ?
Kwanini asingepewa from day one kama arguement yako ni Sahihi ?
UVCCM utoto wenu unatia Kinyaa sana
Kwa nini mnampangia Rais
 
JJ Mbungo Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa ndiye Mkurugenzi Msaidizi wa Takukuru.

Kachero huyo mbobevu alitolewa jeshini na kupelekwa Takukuru kwa mkakati maalum wa yeye kwanza ahudumu kama Mkurugenzi msaidizi huku akiendelea kuzifahamu barabara changamoto za Idara hiyo na hapo baadae aje kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu.

Inasemekana mda wa yeye kuhudumu katika hiyo Ofisi kama Mkurugenzi Mkuu umewadia.Duru zinatabanaisha kwamba toka juzi Mkuu wa Nchi anatarajiwa mda wowote kumtangaza JJ Mbungo kuwa yeye ndiye sasa bosi wa Idara hiyo.

Itoshe kumtakia kila lililo la kheri bwana JJ Mbungo katika majukumu yake mapya-tarajiwa.
Kama wasemavyo ya MUNGU mengi ndiyo hivyo na ya JMP ni mengi na tusikalili kwamba kila mtu anapokaimu ndio atachukua nafasi ya aliyejuu pindi atakapoondolewa. Tumwachie Mungu atakavyomuongoza Rais wetu Kuchagua atakayefaa kuchukua ukuu huo
 
Tatizo la rushwa nchini Tanzania ni la kimfumo. Kubadilisha mtu bila kurekebisha mfumo mzima nadhani haiwezi kusaidia sana. TAKUKURU imejikita kwenye kupambana na rushwa kwa kuadhibu watuhumiwa wa rushwa na siyo kuzuia rushwa kwa kung'amia mianya ya rushwa na kuiziba mapema.

Upande mwingine ukienda mahakamani na kuangalia ni jinsi gani kesi za rushwa zinaendeshwa basi utafahamu kwamba kukamata mtuhumiwa ni kitu kimoja na kumtia nguvuni ni kitu kingine tofauti kabia.

One Star General, Two Star General or Spy Master haiwezi saidia lolote lile kama mfumo ni mbovu katika kiwango cha kisheria na kisera: Hata Dr. Kipilimba alivyokuwa anaingia TISS tuliwaona mkimwaga sifa kemkem kama ilivyo kawaida yenu. Mkasema he's a serious man lakini amefanya nini cha ziada ???

NB: Tatizo kubwa la Rushwa hapa Tanganyika lipo kimfumo na kisera zaidi, japo wengi huwa hatupendi kukubali au pengine hatuelewi.
 
Kama wasemavyo ya MUNGU mengi ndiyo hivyo na ya JMP ni mengi na tusikalili kwamba kila mtu anapokaimu ndio atachukua nafasi ya aliyejuu pindi atakapoondolewa. Tumwachie Mungu atakavyomuongoza Rais wetu Kuchagua atakayefaa kuchukua ukuu huo
Aliondolewa Mlowol,Jamaa akiwa ana kaimu,akaletewa Diwani,anaweza pia akaletewa mwingine
Hakuna Formula
 
Ni Kachero Mbobezi wa Viwango vya Benard Kamilius,

Bin Kamilius alifikia kujifanya Muuza Spare za Magari kwa Miaka mitano kule Kampala miaka ya mwisho ya 1970s

Jeshi letu la Wananchi likasifiwa kwa kushinda vita huku tukisahau ‘Wachonga njia’ ya ushindi huo

Naamini Jasusi Mkuu Diwan Athuman atatungenezea kina Membe na Mahiga wa kutosha kwa kizazi kijacho
 
JJ Mbungo Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sasa ndiye Mkurugenzi Msaidizi wa Takukuru.

Kachero huyo mbobevu alitolewa jeshini na kupelekwa Takukuru kwa mkakati maalum wa yeye kwanza ahudumu kama Mkurugenzi msaidizi huku akiendelea kuzifahamu barabara changamoto za Idara hiyo na hapo baadae aje kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu.

Inasemekana mda wa yeye kuhudumu katika hiyo Ofisi kama Mkurugenzi Mkuu umewadia.Duru zinatabanaisha kwamba toka juzi Mkuu wa Nchi anatarajiwa mda wowote kumtangaza JJ Mbungo kuwa yeye ndiye sasa bosi wa Idara hiyo.

Itoshe kumtakia kila lililo la kheri bwana JJ Mbungo katika majukumu yake mapya-tarajiwa.

Japo umekuja hapa ama Kujipigia ' Promo ' ukiwa Wewe ndiyo Mhusika au labda amekutuma uje upime Upepo uone Maoni yetu mwambie tu ya kwamba pamoja na hizi Sifa zako za Kiutendaji ulizompa hapa lakini asishangae vile vile kuwa Rais JPM anaweza asimteue Yeye na akateuliwa Mtu kutoka kule ambako hamkujui na wala hamkumtegemea. Kwa maoni yangu huu Uzi ndiyo unaweza ukawa umemuharibia kabisa badala ya Kumsaidia. Hata hivyo kama akiteuliwa Yeye namtakia Kila la Kheri japo nina wasiwasi kama atakuwa ni Yeye kwa jinsi ninavyomjua Rais JPM asivyotabirika hasa linapokuja Suala zima la Uteuzi nchini.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom