John Heche: Nakupongeza sana Ummy kwa kupiga marufuku MaRC na MaDC hawa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Mbunge wa Tarime John Heche.

Nakupongeza sana mh Ummy kwa kupiga marufuku MaRC na MaDC hawa wanaokurupuka kuweka madaktari na manurse ndani kama fashion.

Ni jambo la ajabu kila DC na RC akienda sehemu bila kujali kama kuna vitendea kazi au madawa anaagiza daktari awekwe ndani.

Na hii ni kwenye kila nyanja utaalamu leo ni kama hauheshimiki mwingine akienda shuleni anaweka walimu ndani yaani ni vituko tupu.
 
Hili suala litakiwa kupingwa na watanzania wote, tuache kudhalilisha wataalamu wetu kwa mambo ya kisiasa.
Mkuu hili taitizo sisi ndio tumelisababisha maana watu wengi huwa wanashangilia pindi inapotokea ndio maana umegeuzwa kuwa mradi wa sifa!
 
Ummy Mwalimu naye mnafiki tu alisubiri watu wapige kelele weee ndipo azinduke, sasa hivi wengi walipoteza morale ya kazi kwa upuuzi wa ma DC na RC
 
Nchi itulie sasa.ilikua ni matatizo matupu hawa wakuu wa wilaya na mikoa walikua wanatafuta sifa za kipuuzi kwa kudhalilisha watu.makonda kashanyooshwa nae sasa
 
Kuna yule mwenyekiti aliwekwa ndani kisa kubishana na dc,yaani hutakiwi kujitetea
 
Watu wanaishi hawajui kesho wataamkaje.vioja na sifa za kipuuzi waache.hii sio north Korea
 
Anaandika Mbunge wa Tarime John Heche.

Nakupongeza sana mh Ummy kwa kupiga marufuku MaRC na MaDC hawa wanaokurupuka kuweka madaktari na manurse ndani kama fashion.

Ni jambo la ajabu kila DC na RC akienda sehemu bila kujali kama kuna vitendea kazi au madawa anaagiza daktari awekwe ndani.

Na hii ni kwenye kila nyanja utaalamu leo ni kama hauheshimiki mwingine akienda shuleni anaweka walimu ndani yaani ni vituko tupu.
Ummy amechelewa sana kuchukua hatua mpaka MAT wametoa tamko ndio anajitokeza.
 
Ummy amechelewa sana kuchukua hatua mpaka MAT wametoa tamko ndio anajitokeza.
Wanajua tatizo litakalotokea hapo mbele. Wanadhani madaktari ni kama waalimu au polisi. Madaktari hawatoshi nchini na nchi nyingi zinahitaji madaktari tofauti na polisi ambao wengi ni ....
 
Hili suala litakiwa kupingwa na watanzania wote, tuache kudhalilisha wataalamu wetu kwa mambo ya kisiasa.
Tukumbuke pia kuwa wako wataalamu ambao wanatumia taaluma yao vibaya:
1) majengo kuporomoka
2) wagonjwa kupatiwa huduma ya matibabu kwa rushwa
3) uuzaji wa madawa yaliyopitwa na muda au feki
4) ununuzi hewa
5) ukufunzi hafifu.
Na kadhalika

Nani awachukulie hatua wataalamu wa aina hiyo, ikizingatiwa nchi yetu ilifikia mahali ambapo ni kana kwamba kuna ombwe la utawala. Nchi ikageuzwa kuwa shamba la bibi!!
 
Wachukuliwe hatua za kisheria(wafikishwe mahakamani) ama kusimamishwa wakati uchunguzi unaendelea.
 
Back
Top Bottom