John Heche: Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana?

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.

Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.

Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!

Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Kama kesi ya kuota mtukufu amekufa haina dhamana ni bora ikaunganishwa na zile tatu za mauaji,uhaini na armed robbery ambazo sheria zetu zinatambua kwamba hazina dhamana, vinginevyo ni mahakama kutumika vibaya kunyima watu haki zao, na watu wataendelea kuona maona hata kama mtukufu hayapendi.
[HASHTAG]#Justice[/HASHTAG] for Lema.
 
Kesi yenye haki ya dhamana inakosa dhamana kwasababu ya danadana. Halafu hizo mahakama huwa zinasema ziko huru. Uhuru upi wa kumnyima mtu haki kwa maelekezo? Mtoa mada hapo juu anasema alishaambiwa mapema na imetimia.
 
Siasa za kitata za mhe mbunge zinazoishia mahakamani karibu kila mara zinachosha.

Kama wanafanya kumkomoa wanayo sababu japo siyo ya msingi sana. Dola siku zote hutumia mabavu na vyombo vyake ipasavyo. Ni vizuri mhe. Mbunge akabadili mbinu kwani hii anayotumia haiioneshi kufaulu na itaishia kummpa taswira hasi miongoni mwa jamii
 
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.
Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.
Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!!!! Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!!!!!!!
Nani kasema kanyimwa dhamana? Ni mawakili wasomi wasio na uwezo wa kutafsiri sheria, kanuni na taratibu ndo wamemgharim.
 
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.

Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.

Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!

Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Heche awaulize Mawakili wasomi Mallya na Kibatala kwanini rufaa yao ilitupiliwa mbali? Mawakili wameshindwa kujenga hoja awaulize mawakili....
 
halafu ana sahau kuwa dhamana ya Lema ilikuwa inapiganiwa na mawakili wao kwa kujenga hoja mahakamani lakini wameshindwa kujenga hoja na rufani yao ikatupwa sasa wana anza kulia.
 
Hicho kiswahili ulichotumia ni kutoka nchi IPI?? Hahahaha nyie ndio watanzania wa kuhonga uhamiaji zamu yenu inakuja....

Unajuaje mi Mtanzania? Hiyo mihemko inawaendesha kama inavyomwendesha Godiii. Matokeo yake mnastarehe na familia zenu mwenzenu anasota jela na kuiachia familia yake upweke.
 
Hiyo kesi ina mkono wa mtu tena anyeongozwa na shetani angekuwa ana ongozwa
na Mungu angekuwa hata na chembe ya kuheshimu sheria,ni kesi gani ambayo inaahirishwa mwezi hadi mwezi,wakati taratibu mtuhumiwa ana takiwa afikishwe mahakamani kuendelea na kesi yake ndani ya siku 14.
 
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.

Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.

Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!

Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Ana kesi mbili zinazofanana. Masharti ya dhamana ya kesi ya kwanza ameyavunja kwa kufanya kosa kama lile la kwanza. Kuna haja gani ya kupewa dhamana wakati akiwa huru yeye hajipangi kujibu tuhuma zinazo mkabili bali anatumia uhuru huo kutukana na kusambaza uchochezi.

Wacha aisome namba dadeki
 
Kesi yenye dhamana inanyimwa dhamana.....

Jibu lake ni jepesi mno ambalo hata mtoto wa Chekechea anaweza kujibu.

Jibu lake ni kuwa mahakama hiyo inakuwa imepewa maagizo toka juu kwa yule Bwana ambaye alijiapiza kuwa yeye hajaribiwi..........
 
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.

Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.

Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!

Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Kama mtu anafanya makusudi kwa kujua atapata dhamana.hapa mwisho
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom