John Heche ahoji kwanini Polisi walitumia nguvu kuwazuia Wananchi waliovamia Mgodi wa ACACIA?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,484
54,854
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge kuhusu polisi kutumia nguvu kupita kiasi wakati wakiwaondoa wananchi waliovamia mgodi wa Nyamongo. Amesikitishwa na kitendo cha Polisi kuwazua Wananchi waliovamia Mgodi wa Madini wa Nyamong'o unamilikiwa na ACACIA.

Serikali ilitutangazia ACACIA ni majambazi, wananchi tumeamua kwenda kupambana na Majambazi ili kuchukua kilicho chetu, kwanini Polisi Watukataze na watumie nguvu kututawanya?

Wananchi wa Tarime walivamia Mgodi wa dhahabu wa Nyamongo kama walivyoelekezwa na Mbunge wao=>Mara: Wananchi wavamia mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo na kupora Polisi wakiwepo!.

Wiki iliyoisha Mbunge wa Tarime aliahidi kuongoza Wananchi kuvamia Mgodi unaomilikiwa na ACACIA Wanaodaiwa hawapo nchini kisheria=>John Heche: Wananchi wa Tarime jiandaeni, Tutavamia mgodi wa Acacia na kupora kila kitu
 
Serikali ilitutangazia ACACIA ni majambazi, wananchi tumeamua kwenda kupambana na Majambazi ili kuchukua kilicho chetu, kwanini Polisi Watukataze na watumie nguvu kututawanya?
Soon mtasikia linatolewa tamko kali la kupiga marufuku kuvamia/kubugudhi wale tuliowaita wezi kama lile la kutowataja wastaafu.
 
sio busara. ni sawa na mbuge wa dodoma awaambie wananchi wavamie bunge kwa sababu walipitisha sheria zinazotoa mianya ya huo ujambazi wake. nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria sio huo uhuni.
 
sio busara. ni sawa na mbuge wa dodoma awaambie wananchi wavamie bunge kwa sababu walipitisha sheria zinazotoa mianya ya huo ujambazi wake. nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria sio huo uhuni.

Ukiisoma hii habari utaona sura mbili za serikali vs wananchi na CHADEMA

LIsu anaposema utaratibu wa kuzuia na kuunda tume ni Kinyume cha sheria maana yake ni sawa ni Heche kuwaambia ile ni mali yetu ACACIA wametuibia twende tukaichukue kwa upande mmoja. Wanaompinga LISU na kusema amehongwa ni sawa sawa na kupingana na Jeshi la polisi linalozuia wananchi wasivamie migodi maana watakua wamekiuka sheria.

Ukiangalia LISU yupo sahihi kama Jeshi la polisi lilivyo sahihi kuzuia wananchi kuvamia migodi. Lakini kuna ndugu zangu wanapiga vuvuzela kama wasiojua kusoma na kutumia Masaburi kufikiri.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom