John Fisso na Makika Kasuga hawa ndio walioliua Shirika la Chuma la Taifa

SOPINTO

Member
Oct 19, 2020
64
150
Awali ya yote kwanza nilipongeze Gazeti la Mwananchi kwa kazi nzuri sana juu ya uchunguzi wa kina katika kujua chanzo cha kifo cha Shirika la Chuma nchini , binafsi nimesoma matoleo yote mawili yaani toleo la Jumatano , Januari 27 na toleo la pili Januari 28 , 2021. Shirika la Chuma lilianzishwa mwaka 1966 likiwa na lengo kubwa katika kusimamia rasilimali madini aina ya Chuma nchini .

Lakini kwa kukosa uzalendo Meneja Mkuu wa shirika hilo Bw. John Fissoo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha Bw. Makika Kasuga ndio waliofanya juhudi zote za kuliua shirika hilo la taifa kwa tamaa zao na maslahi binafsi kwa kujimilikisha mali za shirika ikiwa pamoja na kuuza vitega uchumi mbalimbali vya shirika hilo kama vile Nyumba za shirika , Viwanja vya shirika , Fedha mbalimbali za Shirika hilo.

Gazeti la mwanachi mmefanya kazi yenu nzuri lakini maajabu ni kwamba chombo cha serikali ambacho kina kazi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini hakijui chochote juu sakata hili ameulizwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU anasema hana kumbukumbu sahihi , yaani mkurugenzi mkuu unasema huna kumbukumbu juu ya jambo la maslahi ya taifa? upo hapo kwa faida ya nani? Kwa hali hiii hata TAKUKURU ni sehemu ya kutoa na kupokea rushwa wala rushwa wote.
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,205
2,000
Usimlaumu huyo mkurugenz wa TAKUKURU usikute na yeye n kama mm nayejua leo kuwa kulikuwa na shirika la chuma nchi hii

Mwananchi wajaribu kufuatilia na shirika la plastiki huenda kuna mijizi mingine imefisadi shirika hili kama lilikuwepo lakni
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,398
2,000
Nahisi ni tatizo la kutojua kujibu maswali. Kwa kiongozi wa TAKUKURU, nahisi hakujua kuwepo kwa shirika hilo. Alichostahili kufanya ni kuichukuwa habari hiyo kuwa ni ya manufaa kwa ofisi yake na kuanza kuomba nyaraka husika. Mwananchi wangekuwa ndo whistle blower!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,489
2,000
Awali ya yote kwanza nilipongeze Gazeti la Mwananchi kwa kazi nzuri sana juu ya uchunguzi wa kina katika kujua chanzo cha kifo cha Shirika la Chuma nchini , binafsi nimesoma matoleo yote mawili yaani toleo la Jumatano , Januari 27 na toleo la pili Januari 28 , 2021. Shirika la Chuma lilianzishwa mwaka 1966 likiwa na lengo kubwa katika kusimamia rasilimali madini aina ya Chuma nchini .

Lakini kwa kukosa uzalendo Meneja Mkuu wa shirika hilo Bw. John Fissoo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha Bw. Makika Kasuga ndio waliofanya juhudi zote za kuliua shirika hilo la taifa kwa tamaa zao na maslahi binafsi kwa kujimilikisha mali za shirika ikiwa pamoja na kuuza vitega uchumi mbalimbali vya shirika hilo kama vile Nyumba za shirika , Viwanja vya shirika , Fedha mbalimbali za Shirika hilo.

Gazeti la mwanachi mmefanya kazi yenu nzuri lakini maajabu ni kwamba chombo cha serikali ambacho kina kazi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini hakijui chochote juu sakata hili ameulizwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU anasema hana kumbukumbu sahihi , yaani mkurugenzi mkuu unasema huna kumbukumbu juu ya jambo la maslahi ya taifa? upo hapo kwa faida ya nani? Kwa hali hiii hata TAKUKURU ni sehemu ya kutoa na kupokea rushwa wala rushwa wote.
... unawonea Mkurugenzi wa TAKUKURU! Tukio la miaka ya 70/80 awe na kumbukumbu nalo leo tena kaulizwa kwa kushtukiza? Anahitaji muda wa kufanya rejea.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,252
2,000
Na waliochoma jengo iliyokuwemo makao makuu ya NASACO miaka ya 80 kwa tamaa zao za kifisadi tunawasaka mmoja baada ya mwingine - hatuachi mtu salama
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
55,440
2,000
Na waliochoma jengo iliyokuwemo makao makuu ya NASACO miaka ya 80 kwa tamaa zao za kifisadi tunawasaka mmoja baada ya mwingine - hatuachi mtu salama
Mmoja wapo alikuwa waronga sjui nyaronga
Jaluo mmja alikuwa mjivuni sana
Sema alishatangulia mbele ya haki kitambo tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,139
2,000
Kuna mtu aliwai niambia sera ya viwanda imekwama kutekelezeka sababu nchi haina chuma.
Ebu anaeeelewa anielimishe chuma ina uhusiano gani na ukuaji wa viwanda?
Na si tuna liganga au chuma chake hakitoshi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom