John Demujacor: Demokrasia ni muhimu, lakini uongozi wa chama ni muhimu zaidi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
7ea69f28-062f-4bb1-a7d8-3211c5375f6a.jpg



Bw. John Demuyakor, mwanahabari wa Ghana anayesoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha China hivi karibuni alisema, "demokrasia ni muhimu, lakini uongozi wa chama ni muhimu zaidi, na mafanikio ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC katika suala hili yanapaswa kuigwa na vyama vya kisiasa vya nchi za Afrika."

Akizungumzia mada ya "kujenga na kuendeleza nchi ya ujamaa yenye umaalum wa China", Bw. John amesema, kwanza kabisa dhumuni la msingi la CPC la "kutumikia umma " linaendana na msingi wa demokrasia, jambo ambalo limeiwezesha CPC kuwaunganisha wachina bilioni 1.4, kuwaondoa Wachina milioni 100 kwenye lindi la umaskini, na pia ni msingi wa mafanikio ya chama hicho. Pili, chama kinapaswa kuongozwa na mtu anayekubalika kwa wananchi, na wakati huo huo, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kutambua uongozi wake na kuwa tayari kujifunza au hata kuiga mfano wake wa uongozi. Kwa bahati, rais Xi Jinping ni kiongozi wa namna hiyo, na anaongoza CPC kuhimiza kithabiti maendeleo ya kiuchumi na kijamii ndani ya nchi, na wakati huo huo kinafuata sera ya mambo ya nje ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kutoathiri maendeleo ya nchi nyingine. Ametembelea nchi za Afrika mara kadhaa na kujenga urafiki mkubwa na watu wa huko. Tatu, kigezo cha nchi kuwa na kidemokrasia au la, ni lazima kiwe kwamba kila mtu ana haki za msingi. CPC imetekeleza sera na mageuzi mbalimbali kwa vitendo, na vyote vimepata matokeo mazuri. Mapato ya watu yameongezeka na mazingira ya maisha yameboreka. Nne, maendeleo ya demokrasia pia yanapaswa kuegemea kwenye kuwepo kwa taasisi zenye nguvu za serikali na utawala wa sheria, jambo ambalo CPC imekuwa ikijitahidi kuendeleza.

John alieleza kuwa, vyama vya siasa katika nchi za Afrika vinapaswa kujifunza kutokana na sera, vitendo na uzoefu wa CPC, ili kweli waweze kuwatumikia vyema wananchi wa nchi zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom