John Cheyo ukienda bungeni unamwakilisha nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Cheyo ukienda bungeni unamwakilisha nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Jul 27, 2009.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Leo jioni hii nimemsikia Mh Cheyo Mbunge wa Bariadi akichangia hoja katika wizara ya Nishati na madini.

  Lakini maneno aliyoitimisha nayo yalinishangaza sana.
  Mheshimiwa huyu alihitimisha hoja yake kwa kumwambia spika kuwa "Namalizia kwa kuwambia wabunge wenzangu kuwa jana nilikalishwa kiti moto kuhusiana na mswada wa kupeleka pesa majimboni na ningependa kuwambia wabunge wenzangu kuwa mtu asitutishe maana sisi hapa ndio tuna uamuzi wa mwisho na sheria imetupa uwezo wa sisi kuamua tunavyotaka na si vinginevyo" (Sorry sikuandika neno kwa neno kwa mtiririko aliosema lakini nimeeleza kitu alichokisema) alimaliza kusema na kupokea makofi kutoka kwa wabunge wenzie huku Spika Samweli Sitta akipigilia msumari kwa kufurahi kwa yale mh Cheyo aliyomaliza kuyasema ingawa hayakuwa katika hoja inayozungumziwa.

  Jana nimefuatilia vizuri sana kile kipindi cha Star Tv ambacho kimekuwa hewani kwa masaa kama mawili hivi, ambako yeye na wabunge wenzie wawili walishiriki mjadala uliokuwa ukichangiwa pia na Kiongozi mmoja wa kafu (jina silikumbiki vizuri pamoja na Nape Nauye , na yule mwanaharakati ambaye pia jina lake silikumbuki) waliokuwa Dar es salaam.

  Pia walikuwa wakishiriki katika mjadala huo baadhi ya wachangiaji waliokuwa studio za Mwanza.
  Walishiriki watu mbali mbali waliopiga simu na kutoa maoni yao. Wakiwamo waliotokea shinyanga ambao walimshangaa Cheyo kwa msimamo wake na kumdharau sana.

  Mwisho wa mjadala ilielekea kama huo mswada haukuungwa mkono na watu wengi maana asilimia kama 84 ya wachangiaji waliupinga mswada kwa sababu mbalimbali na kwa kweli waliwaweka kiti moto wabunge wetu hawa.

  Nilivyoelewa huu mjadala ulikuwa unaleta taswira ya jinsi watu wengi walivyoushitukia mswada huo tokana na michango mbali mbali iliyotolewa na wachangiaji na wadau mbalimbali.

  Lakini nilipoyasikia maneno ya mbunge huyu ambaye zamani tulimbatiza jina la bwana mapesa, nilianza kumtilia mashaka kama kweli bado ni Cheyo yule yule wa UDP na bado ana damu ile ile ya zamani.

  Maana kama anaweza kusema kibabe bungeni dhidi ya wapiga kura wake, kuwa wao wabunge ndio wana uamuzi wa mwisho hata kama wapiga kura wake hawakubaliani na hoja. Basi amefirisika kisiasa. Amekwisha na hatakiwi tena kwenye benchi ya wana mageuzi. Naona demokrasia ya ushawishi imemwishia na ameamua kuungana na wabunge wa sisi M kuwapiga teke wapiga kura wake.
  Hafai kurudi bungeni kwa namna yoyote ile, na ni vizuri kuanza mkakati wa kumuondoa kabisa.
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wabunge wengi wameona wenzao tu wanafaidi sasa wale wenye roho nyepesi wameamua waonjeshwe asali
   
Loading...