John Cena is BACK!!

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
WWE ilipata pigo kubwa wiki iliyopita baada ya John Cena kutimuliwa.
Juzi Jumatatu katika ukumbi wa Wells Fargo Centre,Philadelphia,Cena alionekana katikati ya mashabiki akiwa na tiketi yake mkononi. Uwepo wake ulianza kuhisiwa kabla hajafika kwani R-Truth alipanda ulingoni na kudai kuwa alijitolea kumsaidia Cena ila cena alikataa na ikamgharimu kazi yake. Pia akasema 'Nexus might have won the battle,but the war has not started yet.' Pia akatoa kauli kuwa mwanaNEXUS yeyote ajitokeze kupambana naye.Wakati Mcguillicuty akitoka anashambuliwa na mtu asiyeonekana sura bali viatu na kaptula kama vya Cena. Cena anamshambulia pia Heath Slater ulingoni na kumpigiza kwenye meza ya watangazaji. Wade Barret,bosi wa Nexus anajitokeza ulingoni kutangaza kuwa john cena atawindwa na ataipata. Hata hivyo Cena anajitokeza kwenye sikirini kubwa na kumwambia Baret kuwa kabla hajafukuzwa alitoa ahadi kuwa atamjeruhi mwanaNEXUS mmoja baada ya mwingine. Nexus wanamzunguka Cena na anawaambia wanakosea kufikiri kuwa adui yao ni yeye pekee wanakosea. Baadhi ya RAW SUPERSTARS wanawashambulia Nexus na Justin Gabriel anatandikwa Attitude Adjustment juu ya gari na Cena.
 
( The champ is back )!!!I love you,john cena!!!your the best!!!you can't see meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
johncena1.jpg
 
Back
Top Bottom