Jogoo wa sasa wamepoteza majira

kikositija

Senior Member
Jun 19, 2017
123
103
Wanajamvi hii leo weekend,

Baba Salama ndio nimetoka kusalimiana na wadau kitaa baada ya shughuli kubwa iliyoniweka bize kwa takribani juma zima.

Maana mzee anasema tupige kazi na mimi nampa heko kwa sababu anaimba wimbo wangu alionifundisha mwalimu mkuu kuwa siku zote nifikirie nitamfanyia nini mama Tanzania katika uhai wangu ili japo jasho langu liwe na thamani katika kuchangia speed ya 7.20GDP.

Sasa cha kushangaza sasa hivi ni sasa 11.57 PM Jogoo wameshaanza kuwika kuashiria kunapambazuka nadhani nao wanaelewa kuwa Tanzania ya sasa ni ya mchakamchaka kwa hiyo hakuna kulala.

Swali langu ni je ni sahihi jogoo kuwika saa mida hii?

Sent from my Redmi 4X using JamiiForums mobile app
 
Huku niliko ni town hakuna wafugaji wa kutosha, so sina data ya kutoshoa
,
"No research no right to speech"

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
wanajamvi hii leo weekend ,baba salama ndio nimetoka kusalimiana na wadau kitaa baada ya shughuli kubwa iliyoniweka bize kwa takribani juma zima. Maaana mzee anasema tupige kazi na mimi nampa heko kwa sababu anaimba wimbo wangu alionifundisha mwalimu mkuu kuwa siku zote nifikirie nitamfanyia nini mama Tanzania katika uhai wangu ili japo jasho langu liwe na thamani katika kuchangia speed ya 7.20GDP
SASA cha kushangaza sasa hivi ni sasa 11.57 PM JOGOO wameshaanza kuwika kuashiria kunapambazuka ...nadhani nao wanaelewa kuwa TANZANIA ya.sasa ni ya mchakamchaka kwa hiyo hakuna kulala..SWALI langu ni jee ni sahihi jogoo kuwika saa mida hiiiii??

Sent from my Redmi 4X using JamiiForums mobile app
Mchinje huyo
 
mimi nimekulia kwenye maisha ya kilimo na ufugaji jogoo akiwika baada ya jua kuzama na kabla ya 03-04am alfajili kesho yake hiyo ni nyama.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Ndiyo kawaida kama kuna moto muda huo huo anachinjwa wenye kuchoma maini wanakula hata huku jamani jogoo wana wika saa2
 
Mchunguze vzr huyo jogoo atakuwa katoka mikoani...

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Jogoo wa kidojitali,anasoma majira kama yalivyo kulingana na namba yeye kajua ni asubuhi.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Nimelala Shamba jumamosi Simu ikakata charge,mara nasikia kokolikoooooo!!banee nikaamka najua kumekucha nikawasha generator kupampu maji..nimekuja kushtuka baada ya masaa mawili bado Giza ....nikamwamsha jirani kucheki saa ni saa kumi na robo alfajiri!!pumbaf Zak yule jogoo aliniamsha saa nane!!
 
Ni sawa kabisa kuwika muda huo.kawaida jogoo huanza kuwika kila baada ya nusu saa hapa ninapoandika ni saa 8.27 asubuhi lakini huko nje ni kelele zao tu hao majogoo,kwa hio wao hawajali muda ule kamili ufike ndo wawika hapana ila ww changanya na zako utapata jibu.shukran

Sent from my HTC Desire 820 dual sim using JamiiForums mobile app
 
Mimi pia nimeona hilo linatokea sana, ila nimewaza kisayansi zaidi. Kule kijijini kuku wanakaa kwenye chumba ambacho ni giza., hivyo asubuhi kukishaanza kupambazuka jogoo anajua kunapambazuka na ni kawaida kuwika saa kumi na moja alfajiri. Sasa huku mijini utakuta banda la kuku lina mwanga (taa) usiku kucha, tena kuku wanakula hadi usiku. Sasa jogoo atatofautishaje mchana na usiku? Ukizingatia hata humtoi nje unamlisha ndani tuu? Mimi nimegundua akiwika saa tano au sita usiku, naenda nazima taa wakae gizani, lazima ataacha kuwika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom