Jogoo Unayemshabikia Anapogalagazwa Unafanyaje?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Wengi wetu tumekutana na hali ya kuwaona jogoo wawili wakipambana. Kawaida ya mpambano wa majogoo ni kuvutia watazamaji.

Na kila mtazamaji huwa na hulka ya kuchagua jogoo wake wa kumshabikia; kama ni jogoo mweusi na mwekundu, basi, kutakuwa na mashabiki wa jogoo mweusi na wale wa mwekundu; makundi.

Na hutokea, kwa yule ambaye jogoo wake ameshindwa pambano, basi, atatoka mahali hapo kwa masikitiko, akiwa na unyonge. Kisa? Jogoo wake kashindwa! Ni hulka ya mwanadamu.

Lakini, wanadamu tunapaswa pia kutumia bongo zetu katika kutoa hukumu, na si kuongozwa na mapenzi ya moyoni tu. Hivyo ndivyo wafanyavyo mahakimu na majaji wanapoamua mashauri mahakamani.

Naam, usiishie tu kumlaani jogoo mwekundu anayeonekana kuwa na maumbile makubwa kwa kumtwanga jogoo wako mweusi mwenye maumbile madogo.

Ukiumiza sana kichwa kwa kufikiri, basi, unaweza kubaini, kuwa jogoo mwekundu alikuwa na sababu, na haki pia, za kumtwanga jogoo wako mweusi.

Ufanyeje basi?

Ndio, unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuyaangalia mapungufu ya jogoo wako mweusi, kuikubali hali halisi.

Bahati mbaya, si wengi wenye kutaka kuifanya kazi hii ya kuumiza vichwa. Kutafakari mapungufu yao na yale ya wanaowashabikia.

Na hilo ni Neno La Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom