Jogoo mwenye shanga na hirizi azua kizazaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jogoo mwenye shanga na hirizi azua kizazaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Jul 30, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  WAKAZI wa Mtaa wa Nyanchenche Road mjini Sengerema juzi walifurika kushuhudia tukio la kuonekana jogoo asiye na manyoya akitembea huku akiwa amefungwa shanga na hirizi mbili shingoni na mabawa yake yakiwa yamechanjwa chale na kupakwa dawa nyeusi.

  Tukio hilo lililovuta umati wa watu lilitokea juzi saa 7:00 mchana kwenye moja ya familia ya mtaa huo ambaye alidai kwamba kuku huyo alijitokeza nyumbani kwake bila kufahamu alikotokea.

  Kuku huyo wa ajabu alikutwa na wananchi katika mji huo ulioko kando kando ya barabara, jambo lililowashtua wakazi wa Sengerema waliofika kulishuhudia huku wakilihusisha na imani za kishirikina.

  Katika tukio hilo hakuna mwananchi aliyejitokeza kumshika kuku huyo, huku wenyeji wa mji husika wakiendelea na shughuli zao licha ya kuonyesha mshituko.

  Akizungumza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa kitongoji hicho Leah James alieleza kushangazwa na tukio hilo aliloliita la ajabu, na kwamba halijawahi kutokea katika kitongoji hicho kwani limeibua hisia tofauti miongoni mwa wanajamii.

  Nimepata taarifa za tukio hili ilikuwa mchana muda wa saa saba na tumefika mpaka eneo la tukio, kwa kweli inashangaza na kusikitisha, huyo kuku wa ajabu hana nyoya hata moja wala alama ya kidonda na amechanjwa chale kwenye mbawa zake,kavishwa hirizi mbili shingoni na amefungwa shanga kwenye mbawa zake alisema mwenyekiti.

  Baada ya tukio hilo uongozi wa eneo hilo na sungusungu uliamua kuitisha mkutano siku iliyofuata ambapo walifuatilia na kumbaini mmiliki wa kuku huyo kuwa ni Leticia Makoye ambaye alidai kuku huyo ni wake na humtumia katika shughuli za uganga wa kienyeji .

  Kikao hicho kiliamua kumrudishia kuku huyo ingawa alikuwa tayari amekufa kutokana na kupigwa baridi usiku kucha,maamuzi yaliyopingwa na wananchi na hivyo kulazimika kumshambulia kwa mawe hadi nyumbani kwake huku viongozi wa mtaa huo wakimpatia ulinzi hadi alipoingia ndani ya nyumba.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Ningelikuwa ni mimi ningemkamata huyo kuku na kumchinja na kumla ina siwe kitu chochote kile imani za kishirikina hizo. Mkuu Young_Master
   
 3. paty

  paty JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,251
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  sisi ndo maana hatuendelei , tunaishi karne 15,
   
 4. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni.
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Unamlaje kuku wa hivo? Hana manyoya....
  Akiwa sio kuku je?
  Usije kula mtu.
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Duniani kuna mambo! lol
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu Young_Master hapo hakuna kitu cha chale wala nini
  Unamkamata na kumla tuone kama kuna chochote tena unaweka na sala kabisa wakati unamla
  Bado watu wana imani za ajabu sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Ndio hapo sasa.. MziziMkavu angalia usije kula visivyoliwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mr Rocky embu kajaribu kwanza wewe...ukifanikiwa kumla bila kudhurika basi na mimi ndio nitaenda kujaribu.
   
 10. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Huyo angekamatwa tuu achinjwe....hakuna kitu cha kalumanzira wala nini...nadhan ni jiran anampima mwenzake imani.anamtishia nyau. baadae atamtumia paka aliemvalisha shanga:shetani:
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh!!! Haya bwana.
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Haya mambo bwana ndio maana hatuendelei.
   
Loading...