Joel Bendera atunukiwa shahada ya uzamivu, sasa kuitwa Dakta Bendera

HONORIS CAUSA!Waacheni wafu wazike wafu wao,bali ninyi jiandikisheni SOKOINE,MZUMBE,UDSM,ARDHI,NAIROBI UNISA kupata SHAHADA ALII ZA UZAMIVU na tafiti ziwe za kuweza kusukuma hili gurudumu la kusaka tonge hapa TZ!
 
Kwa taarifa yako unatakiwa uitwe doctor na yule tu aliyekupa huo use...ge [udoctor] tena awe anakuitia hukohuko mlikopeana!! ie. sebuleni, bar, guesthouse etc. usithubutu kuitws mbele ya wanaume!
 
Na mtu anatembea kifua mbele akiitwa dr kwa phd ya kupewa, jaribu kwenda class muone ugumu wake, mnaidharirisha phd bana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na mmoja wa wanasiasa machachari nchini ndugu Joel Bendera, siku ya jana ameweza kutunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha California State University cha nchini marekani (USA) Makamu mkuu wa chuo hicho alimtunuku ndugu Joel Bendera phd hiyo katika tafrija ndogo iliyofanyika viwanja vya ikulu ndogo mjini Morogoro! sambamba na hilo ndugu Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Goodluck Ole Medeiy naye pia alitunukiwa shahada hiyo ya heshima ya uzamivu.
Hongera sana Dakta Joel Bendera
source: Abood Tv
Mshaija
Yaani anaenda kufanyia tafrija binafsi IKULU ndogo? duuuuu
 
Kwa taarifa yako unatakiwa uitwe doctor na yule tu aliyekupa huo use...ge [udoctor] tena awe anakuitia hukohuko mlikopeana!! ie. sebuleni, bar, guesthouse etc. usithubutu kuitws mbele ya wanaume!
Mkuu punguza hasira, ila nimecheka sana kwa hii comment yako.
 
Labda tueleweshane kuhusu degree za heshima. Heshima kwa njia mbalimbali zinatolewa kwa watu kutokana na michango yao katika nyanja mbalimbali k.m.f. michezo - Sir Alex Ferguson, huku Afrika kuna Uchifu wa heshima , wengine kupewa ufunguo wa jiji, hata uraia wa heshima unatolewa.
Si vizuri kuchanganya degree za heshima na degree za kusomea na kufanya mitihani. Wengi wanaopewa shahada za heshima hawazihitaji kwa kutafutia kazi . Hata wasomi wanasayansi wenye shahada lukuki wanapewa shahada za heshima katika taaluma kama sheria, tofauti na fani zao.
Kuwapongeza watanzania mwenzetu wanaopewa shahada za heshima na vyuo maarufu nchi za nje au hapa nchini ni jambo la uungwana na mara nyingi ni heshima kwa Tanzania.

ok sawa tumekuelewa! sasa tuambie ni amepewa kutokana na kipi alichokifanya? harafu tu judge
 
Back
Top Bottom