Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,805
- 4,484
Picha: Kushoto Rais wa Marekani Joe Biden. Kulia rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Marekani Joe Biden ameapa kufunga bomba muhimu la gesi la Urusi kuelekea Ujerumani iwapo Moscow itaivamia Ukraine.
Akizungumza baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Washington, Biden amesema Marekani "itamaliza" bomba la Nord Stream 2.
Mazungumzo yao yamekuja wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow na kuelezea matumaini kwamba vita vinaweza kuepukwa.
Kwa sasa Urusi ina zaidi ya wanajeshi 100,000 waliokusanyika kwenye mipaka ya Ukraine.
Katika wiki za hivi karibuni, Moscow imetaka muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi NATO kupiga marufuku Ukraine kuwa mwanachama, na kwamba kundi hilo lipunguze idadi ya wanajeshi wake mashariki mwa Ulaya.
Mvutano kati ya Urusi, Ukraine na nchi za Magharibi unakuja karibu miaka minane baada ya Urusi kuiteka rasi ya Crimea kusini mwa Ukraine na kuunga mkono uasi katika eneo la mashariki la Donbas.