Joe Biden na Donald Trump, ni nyoka wa aina moja wenye rangi tofauti

Tmainitvp

Member
Mar 25, 2019
64
119
Kwanza nianze kwa pongezi safi kabsa kwa mshindi wa 46 wa kiti cha urais wa Marekani Joe Biden wa Democratic party, si jambo la mchezo mchezo kuingia Ikulu kwa nchi yenye nguvu duniani kama Marekani yenye demokrasia kwa 77%.

Wengi wetu hasa waafrika tulitegemea na tulikua tukisubiri mabadiliko ya kiti hicho cha urais kutokana na baadhi ya kauli mbaya na chafu zilizo kuwa zikitolewa na rais alie maliza muda wake Donald Trump. kwa mfano "Africa ni kama tundu la choo" nk.

Kulikua na ubaguzi wa rangi kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani kiasi cha waafrika waishio huko 'diaspora' kitoridhishwa na mwenendo wa rais Donald Trump, leo tumepata rais mwingine, at least kuna mabadliko madogo huenda yakajitokeza.

Lakini tutajidanganya mpaka lini, kamwe tusije kutegemea mafanikio ya mwafrika yakaletwa na mzungu, hata siku moja. tutambue tu kua wale wote( Biden na Trump) ni wamarekani weupe ingawa mmoja wao ana makamu mwenye asili ya weusi, ubaguzi utabaki pale pale ita kwa namna tofauti

Wote wale ni nyoka, tena sumu kwa bara la africa, unyonyaji utabaki pale pale, ukandamizaji na ukoloni maomboleo, wote lengo lao ni kuifanya America kua nchi yenye nguvu zaidi ukizingatia ushindani uliopo kati ya Marekani na nchi kama China na Korea.

Huwezi waahidi wamarekani barabara wala umeme, sijui maji , zaidi watataka kua taifa kubwa zaidi, watakuaje taifa kubwa?
kwa kuwatawala Uingereza?!, Urus au Ujeruman?, that is a big NO,
tusitegemee makubwa kutoka kwa Biden Africa

Asanteni
 
Unataka kushauri nini mkuu.
Sisi waafrika ya marekani yanatuhusu nini
Hata hvyo ilitakiwa tu atokee rais 1 kati ya wawili hao.

Biden atakuwa kiongozi mzuri zaidi kuliko yule mwenye druma nimezungumuzia kwa kuhusianisha na Trump na sio Obama wala Bushi. only Trump alikuwa hafai hata kuwa kiongozi wa nyumba kumi
 
Yeah, ni kweli
lakini kumbuka kampeni za Biden zili base sana maswala ya ubaguzi na janga la corona, kupitia kampeni hizo hizo, unadhani kwel Biden atakua suluhisho la ubaguzi wa rangi Marekani?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani kuna chama kimoja kinaitwa REPU-DEMO! Marais wao wote utekeleza ilani za chama hicho!
 
Unataka kushauri nini mkuu.
Sisi waafrika ya marekani yanatuhusu nini
Hata hvyo ilitakiwa tu atokee rais 1 kati ya wawili hao.

Biden atakuwa kiongozi mzuri zaidi kuliko yule mwenye druma nimezungumuzia kwa kuhusianisha na Trump na sio Obama wala Bushi. only Trump alikuwa hafai hata kuwa kiongozi wa nyumba kumi
Not true. Biden atakuwa kiongozi mbadala wa Trump kwa sababu tu ya korona. Na ugonjwa huu ukitoweka, au JB akafanya mafyongo, Trump ni Rais 2024.
 
Biden anakuwa rais wa 46 wa Marekani sio wa Afrika hivyo atapigania maslahi ya wamarekani na sio ya waafrika.

Sisi tuna bahati mbaya sana kuwa na jadi ya kuwa na watawala wa kiimla hali ambayo itaifanya Afrika abaki kuwa hivi ilivyo siku zote kwani hata uchaguzi tu wa maana hatuwezi kufanya.
 
Biden anakuwa rais wa 46 wa Marekani sio wa Afrika hivyo atapigania maslahi ya wamarekani na sio ya waafrika.

Sisi tuna bahati mbaya sana kuwa na jadi ya kuwa na watawala wa kiimla hali ambayo itaifanya Afrika abaki kuwa hivi ilivyo siku zote kwani hata uchaguzi tu wa maana hatuwezi kufanya!
Nini maana ya kuwa rais wa taifa kubwa kama Marekani?

Ni kwanini marekani alikua na ni mfadhili mkubwa wa taasisi za kiraia dunian kama WHO, IMF, WB, UNICEF, WLO nk.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani kuna chama kimoja kinaitwa REPU-DEMO! Marais wao wote utekeleza ilani za chama hicho!
Marekani kuna vyama viwili tu
Republican na Democratic party
vyo lengo lao ni ku make America a great Nation zaidi ya hapo ilipo. na ili ifanikiwe adhima yake hiyo, ni lazima kuwepo tabaka la chin ambalo litanyanyaswa. Tabaka hilo si jingne bali ni Africa. kamwe huezi tegemea marekani ikaja kuwanyanyasa wazungu, sahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi sijakuelewa kabisaa...hili bandiko lako..na sijajua ni kwa nini umeliandika hivi.

Huenda wewe nae unafirikiria ukombozi kutoka marekani.

Uchaguzi wa USA unatuhusu nini sisi?
 
Back
Top Bottom