The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
- Thread starter
- #41
Hakika umenena vyema...Kuna haja ya kuujengea hoja huu mstari mmoja na nusu, kwa sababu ndio ukweli wenyewe.
Mkuu 'Chige' upo tayari kufanya hivyo. Kwa nini inakuwa hivyo!
Mimi ntasema "It all boils down to self interests and the pressure groups behind the subject of interest" Mugabe aliwekewa hadi vikwazo vya kiuchumi, kwa sababu wale mashoga walichachamaa ile mbaya.
CHADEMA , na sisi wengine wote tunaochukizwa na manyanyaso na kunyimwa haki ni wajibu wetu kutambua kwamba kazi ya kujiondoa kwenye hali hiyo ni yetu sisi wenyewe.
Uwanja wetu muhimu sana wa kuyapata mafanikio hayo upo hapa hapa nyumbani sio kwingine kokote.
Huko nje tukitaka msaada ni kushirikiana na 'pressure groups' wa huko ili na wao wawalalie viongozi wao na serikali
Usitegemee serikali za huko kufanya lolote bila ya kusukumwa na wananchi wao huko huko kwao.
Wengine wanadhani kelele zetu hizi ni eti mwisho wa siku serikali za magharibi ziingilie tawala za nchi zenye uongozi wa chembechembe za uimla kama inavyofanyika huko Syria, Afghanistan, Somalia au DRC na kwingineko...
Lakini ulichokieleza hapa hakika ndivyo inavyopaswa kuwa...
Na uzuri wa serikali za wenzetu zinaheshimu na kusikiliza sauti za RAIA wao na kuzifanyia kazi sawia...
Tuendelee kupiga kelele za mabadiliko na tushirikiane na pressure groups za mataifa mengine na za kimataifa kuzishawishi nchi zao kuacha kushirikiana na serikali zisizoheshimu demokrasia, utawala wa sheria na haki za watu kama Tanzania..