Joe Biden achaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Ushindi wake unakuja baada ya kushinda kwa kishindo jimbo la Pennsylvania.

Anakuwa Rais wa kwanza kuingia Madarakani akiwa na umri mkubwa (miaka 78). Pia, Marekani imepata Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke, Kamala Harris.


Screenshot_20201107-200149.png

worldstar_20201107_7.jpg

BIDEN: NITAWATUMIKIA WALIONIPIGIA NA WASIONIPIGIA KURA

Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Marekani katika Nafasi ya Urais, Joe Biden amewashukuru wamarekani kwa kumpa dhamana ya kuongoza taifa hilo

Katika tweet yake amesema atawatumikia wote bila kujali kama walimpigia kura au ambao hawakumpigia kura

Ameahidi kutowaangusha kwa imani ya uongozi ambayo Wananchi wamempa kwa kipindi hiki
nostalgic.videos_20201107_8.jpg

Rais Mteule wa Marekani Joe Biden
radio5tz_20201107_5.jpg

Kamala Harris Mwana Mama wa kwanza katika Historia ya Marekani kuwa Makamu wa Rais.

=====

Joe Biden ameshinda uchaguzi wa rais wa Marekani dhidi ya Donald Trump, vituo vya televisheni vimetangaza -- ushindi ambao umehitimishwa na mgombea huyo wa Democratic kushinda maeneo yote yenye ushindani yaliyochukuliwa na Republican mwaka 2016.

Vituo vya televisheni vya CNN, NBC News na CBS News vimetangaza kuwa mbio hizo zimeisha kwa Biden kuibuka kidedea baada ya kukadiria ushindi katika jimbo ambalo lilitarajiwa kuamua mshindi la Pennsylvania.

Biden, mwenye miaka 77, ni mgombea mwenye umri mkubwa kuwahi kuchaguliwa kuingia ikulu ya Marekani, maarufu kwa jina la White House.

Trump, 74, ametoa malalamiko yasiyo na ushahidi dhidi ya wizi mkubwa wa kura, na timu yake ya kampeni imefungua kesi katika majimbo kadhaa.

Ushindi wa Biden umemaliza utawala wa Trump uliotingisha siasa, kuistua dunia na kuiacha Marekani ikiwa imegawanyika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Vituo hivyo vya televisheni vilimpa ushindi Biden muda mfupi kabla ya saa 5:30 asubuhi baada ya uongozi wa mgombea huyo wa Democratic katika kura za jimbo la Pennsylvania kuwa wa tofauti kubwa isiyoweza kufikika na hivyo kuwa juu katika majimbo yanayoamua mshindi wa uchaguzi wa rais.

Trump hakusema lolote kuhusu tangazo la mshindi, lakini wakati Biden akiongoza wakati wa kuhesabu kura, rais huyo kutoka Republican alitoa tuhuma zisizo na ushahidi za kuwepo na wizi wa kura na kudai kuwa alishinda uchaguzi.

Mapema leo, wakati akielekea katika uwanja wa golf Virginia, alirudia kuandika katika akaunti yake ya Twitter akisema: "Nimeshinda uchaguzi kwa kiasi kikubwa!"

Hata hivyo, matokeo sasa yanamfanya Trump ambaye ana miaka 74 kuwa rais wa kwanza kuongoza kwa muhula mmoja tangu George H. W. Bush aliposhindwa kutetea nafasi yake miaka ya tisini.

Biden, ambaye kura milioni 74 zimeweka rekodi, alikuwa pamoja na mgombea mwenza wake, Kamala Harris, katika mji wa kwao wa Wilmington, Delaware.

Credit: Mwananchi
 
Nimeumia mno, ila ndo hivyo tujipange 24
Mgombea wako alikuwa na character flaws nyingi mno!

Kapata kura zaidi ya milioni 70 na bado kashindwa!

Hakuna mgombea mwingine wa urais aliyewahi kupata kura nyingi namna hiyo na akashindwa.

Biden kapata kura milioni 74.

Nyingi ya hizo kura si za Biden. Ni kura dhidi ya Trump.

Trump angerekebisha tabia yake na kuachana na beef za Twitter na kuacha kutoa kauli za ajabu ajabu, naamini wananchi wangemsamehe licha hata ya janga Corona maana hakulisababisha yeye.

Watu walichoka na drama zake na tabia zake zisizo za ki presidential.
 
Bila shaka wapigakura wa US wanaongezeka kila baada ya miaka 4. Miaka ijayo kunaweza kuwa na mgombea ambaye atapata kura mil 100 na atashindwa, kulingana na population ya wapigakura ya mwaka huo.
Kapata kura zaidi ya milioni 70 na bado kashindwa!

Hakuna mgombea mwingine wa urais aliyewahi kupata kura nyingi namna hiyo na akashindwa.
 
Leo projections zinaonesha Joe Biden ni president Elect wa US

Kama tulivyomsikia na tulivyozoea sera za Democrats kwa mambo ya nje ni kuingilia au kujali sana mambo ya Africa tofauti na Trump alivyoyapa kisogo!!

Biden aliahidi ku deal na democrasia za Africa kama ilivyokua kwa Obama.

Afrika na mafashisti wake wajiandae maana huyu bwana na Chama chake watatuletea tena mambo ya Arab Spring!!
 
Nimeumia mno, ila ndo hivyo tujipange 24
24, mnataka Trump asimame tena, au someone else?!

Kama mnamtarajia Trump tena, then tell that old man to stop being too arrogant!! Arrogance yake towards anyone else imem-cost huku matokeo yake anaelekea kupoteza hata senate majority!
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom