yutong
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 1,601
- 338
Wazee natizama bunge sasa,hali ni shwari hakuna vurugu wala kelele na kikao kiko chini ya Job Ndugai-Naibu Spika.Wabunge wanasimama kwa heshima bila kugusa Mic,anawachagua kisha anatoa ruhusa kwa kila mmoja kuuliza ama kuchangia bajeti hii ya Mambo ya Ndani.
Hakuna kubwata na kwakweli nimeona Tundu Lissu kwa unyenyekevu kasimama N/Spika kamuona na baadae kapewa ruhusa ya kushika Mic.Tundu Lissu si yule ninaemfahamu leo ananidhamu ya juu na Wabunge wote.Mpaka sasa Mnyika anaongoza kwa hoja nyingi na anazitoa kwa heshima bila kubwabwaja.
Hiyo nidhamu angeanza kuonyesha ndani ya chama chake dhidi ya mafisadi wakubwa. Asilete unafiki bwana anampepea mgonjwa ambaye yuko mahututi lkn ndo hivyo walishamchelewesha haponi tena.
Hii ni sawa mtoto mdogo anamwambia baba yake 'baba mbona umelewa sana?' baba lazima atajibu we mtoto huna adabu siku hizi eh? Ndugai hawataki kuambiwa ukweli na hao waliomtuma kama ndo waliamini kuwa anaweza kachemsha maana mwisho wa siku Ndugai ni aibuu. Hata hakiwatoa nje hawezi rudisha imani kwa watz tena.