JOB NDUGAI: 'Hukumu' ya wabunge wala rushwa wiki ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JOB NDUGAI: 'Hukumu' ya wabunge wala rushwa wiki ijayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]IJUMAA, OCTOBA 26, 2012 12:01 NA DEBORA SANJA, DODOMA


  NAIBU Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ripoti ya tuhuma za ufisadi, iliyowahusisha wabunge wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, inatarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo.

  Lakini pia, Ndugai amevionya vyombo vya habari, kutoendelea kuiandika habari zozote zinazohusiana na mwenendo wa shughuli za Bunge.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, alisema kutokana na unyeti wa shughuli za Bunge, suala hilo lipo kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye atatoa utaratibu wa namna ya kuwasilisha ripoti bungeni.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Kanuni za Bunge toleo la 2007, vifungu 114(17) na 119 (1) hadi (6) kwa pamoja vinampa madaraka Spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni.

  “Spika wa Bunge letu, ndiyo anatakiwa kutoa uamuzi ama kamati, kuwasilisha taarifa hiyo bungeni au vinginevyo, lakini pia spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo bungeni, katika mkutano wa tisa wa bunge, unaotarajia kuanza Oktoba 30 mwaka huu,” alisema Ndugai.

  Alikemea hatua za baadhi ya watu na vyombo vya habari, kuendelea kuandika na kuchapisha juu ya kilichomo ndani ya ripoti hiyo, huku akisisitiza kufanya hivyo ni kosa kisheria.

  “Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hii katika vyombo vya habari, ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa kifungu cha 31 (1) (g) cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya bunge sura 296.

  “Kifungu hicho, kinataka mtu yeyote kuchambua taarifa ya kamati kabla ya taarifa hiyo kuwasilishwa bungeni,” alisema Naibu Spika Ndugai.

  Alisema kamati hiyo, ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa Spika tangu Septemba 20, mwaka huu.

  Alisema endapo itabainika taarifa yoyote, imechapishwa wahusika wanaweza kulipa faini isiyozidi Sh 5,000,000 au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

  Kamati ya kuchunguza tuhuma za wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini, kuhusu kujihusisha na vitendo vya rushwa, iliundwa na Spika Makinda, wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge.

  Makinda alichukua hatua hiyo kutokana na tuhuma zilizokuwa zimezagaa karibu nchi nzima, kuwa wabunge hao wamekuwa wakijihusisha na rushwa.

  Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy Mohamed (CCM), ndiye alikuwa wa kwanza kuanzisha mjadala huo, huku akimtaka Spika Makinda, kuchukua hatua stahiki, ikiwemo ya kuunda kamati ya uchunguzi, hali iliyowafanya wabunge wengine kuungana naye kila walipopata nafasi ya kuchangia.

  Kamati hiyo, ilikuwa chini ya Mwenyekiti na Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi (CCM), Said Arfi (CHADEMA ), John Chiligati (CCM), Godbless Blandes (CCM) na Ridhiki Juma (CUF).


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hakuna CHOCHOTE; Wengi Wao Wamegombea U-CCM-NEC; Na cha ajabu Wameshinda...
   
 3. Kankwale

  Kankwale Senior Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni unyeti gani kwa wezi wa mali zetu?ingefaa ripoti hiyo wapewe polisi(sijui wataiweza!!!),wachunguze wawafikishe mahakamani kuliko kusubiri vikao vya Bunge visivyoweza kumuwajibisha mbunge kwa kuwa na kinga akiwa bungeni.
   
 4. m

  malaka JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hapo inabid wafunike kombe tu maana wakisema wawatimue wabunge watakaopatikana itakula kwa CCM. Ni bora wabebane mpaka 2015 hasa wakijua ni ngumu kurudi bungen. Hakuna jipya hapo zaidi ya yale tuliosikia awali.
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwani TAKUKURU hawakuwepo huko?? Tangu lini BUNGE likaanza kushughulikia waalifu wa RUSHWA. Tulitarajia wao wawape nguvu za kisheria TAKUKURU. Mimi naona kama BUNGE linataka kurukia kazi ya taasisi nyingine, ningesikia wanataka kuwawajibisha TAKUKURU kwa kutowajibika vizuri nigemuelewa angalau.
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sioni unyeti kwenye bunge letu chini ya maspika Dhaifu wa ccm
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hiyo report spika makinda ataizima...kumbukeni makinda alipewa uspika ili kazi yake iwe kutetea serikali na wabunge wa ccm....ndio maana ninammiss samwel sitta...sitta angekua spika wa bunge leo hii ungekuta wabunge/mawaziri wengi washaachia ngazi siku nyingi....yule bwana alikua hakopeshi ndo maana wakampiga chini..msitegemee chochote kwa makinda maana yule anapewa order na ikulu/mwenyekiti wake
   
 8. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wabunge wa ccm ni rubber stamp ya kuidhinisha ulaji haramu wa fedha za nchi.
   
 9. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  hapa sikwamba hatupendi kufuata kanuni, sheria na taratibu. tatizo nikwamba zimekuwa uchochoro wa kufichia waovu.
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kosa la kuripoti taarifa ya uchunguzi ni laki tano au kifungo cha miaka mitatu.
  vyombo vya habari vyote vianaweza kulipa hiyo faini naomba vitudadavulie kilichomo ndani na hila za ccm juu ya hilo.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kama kawa kama dawa. Tumeona ripoti ya mauaji ya mwangosi, ambayo kuna exhibit hadi za video na eye witnesses. Seuze hiyo isiyo na video na eyewitnesses? Usikondo baba, hatutegemei lolote jipya.
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Buzi wa bwana heri,kala shamba la bwana heri,anaenda kuhukumiwa kwenye mahakama ya bwana heri......mbunge wa ccm,kaiba kwenye sirikali ya ccm anahukumiwa na wanaccm,hapo hakuna hukumu ya haki,yale yale ya KAMATI YA HARUSI YA NCHIMBI NA KIFO CHA DAUD MWANGOSI
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  kama kamati imeshachunguza kuna haja gani ya polisi kuchunguza tena? hii ripoti itumike kama ushahidi kuwaburuza watuhumiwa mahakamani!
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama kina lowasa wanapeta hadi leo,hao wabunge watafanyajwe?
   
 15. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Wanipe mimi hiyo Ripoti nitaiweka hadharani bila kujali segerea. Kama nia yao ilikuwa ni siri kwa nini watu wanaipata, na hawa waandishi wetu wa habari vilaza kweli, sio kazi yao kulinda siri za bunge au kamati za bunge wao wakipata habari lazima waziripoti ni kazi ya mhusika kulinda siri zake.

  Huu wizi unaofanywa na vyombo vyote vya serikali kwa kisingizio cha siri au nyara za Taifa have to stop. Kuibia watuibie halafu wezi watutishe kweli nchi hii kiboko.

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Machozi yangu karibu yatakauka.
   
Loading...