Job Ndugai achukua fomu kugombea Uspika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Job Ndugai amechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la 11 amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika ofisi makao makuu ya CCM jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.

Aidha Itunda amesema kuwa fomu hizo zinatolewa kwa gharama ya Sh 500, 000 na zoezi hili litafikia kikomo leo saa 10 jioni.
 
Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo
Huyu Ndugai hana adabu. Awaombe hao wabunge wa CCM watakaopiga kura.

Mkimuona bibi Tulia na yeye kachukua form then itakuwa wazi kabisa atakayeamua nani awe Speaker ni JPM
 
Ni utaratibu wa kawaida wa CCM! Waulize chandimu Mbowe akisema Fulani ndo huyo huyo anakuwa mgombea! Yaani upinzani democracy ni sifuri kabisa!
 
Itapendeza sana kama

Moja: Chama kikimwacha Job Ndugai akamalizia muda wake

Mbili: Tulia Ackson wakamwacha naye atumikie kwa term mbili (kumtengenezea sifa zaidi ya kuwa Spiker huko mbeleni)

Tatu: Wakati wa kuwachagua wenyeviti wa bunge 'wale wasaidizi wa speaker' chama kikapendekeza watu wenye uwezo mkubwa na wazalendo kweli kweli (chama kisikae pembeni uongozi ukaangukia kwa wabunge wakawaida), pia chama kitumie nafasi za uenyekiti wa bunge kama nafasi ya kuwaandaa spiker na naibu speker wa miongo inayokuja
 
angeendelea kujiuguza uguza na matibabu..maana naona ka fangasi zimepanda kichwani tayari
 
BW supika ndugu Waziri Mkuu ndugu mabunge menzangu sikubaliani na hoja za serikali hata kidogo.........Ole Lemasho...MB...1987
 
Bwana yule ndio anamuua na hakuna ataejitokeza kum-challenge Ndugai wala Tulia unless wawapange wa kutuzuga.

Hata hivyo,holi Bunge sio halali kutokana na uchaguzi wa magumashi uliofanyika.
 
Now Ndugai officially out, huyo kipenzi cha baba hakuna wa kumshinda.

Mihimili yote ya nchi sasa imeshikiliwa na mtu mmoja, amewaweka wabunge wote wa chama chake bungeni illegally, then anamuweka spika anaemtaka, then akimaliza hapo anaenda kujiongezea miaka ya kuitawala nchi.

Mbunge gani atakaenyoosha mdomo kuipinga hiyo hoja ya kumuongezea muda kule bungeni?

Hakuna.
 
Spika na Naibu spika wa nini..Wakati wanaweza Kujifungia popote wakatuamlia na Hatuna Namna Tutapokea tu...hata Msukuma,Kibajaji na yule sijui nani Safari hii Wanaweza kuongoza Bunge la CCM tena kwa Kishindo. Ndiyooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom