JMT: Double standards na kids gloves katika Muungano hazitatufikisha mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JMT: Double standards na kids gloves katika Muungano hazitatufikisha mbali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, May 31, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wote ni mashahidi wa jinsi viongozi wetu wanavyotumia double standards na ‘kids gloves' katika kushughulikia mambo mengi yanayoihusu Zanzibar.

  Iko mifano mingi, lakini kwa hivi karibuni kumbuka:
  · Mchakato wa mabadiliko ya katiba ya Zanzibar 2010.
  · Swali lililoibuka bungeni kuwa Zanzibar ni nchi au la
  · Muafaka wa Zanzibar(serikali yakitaifa)
  · Mchakato wa kuunda katiba mpya ya JMT na nafasi ya Zanzibar

  Mara zote viongozi wa JMT wamekuwa wakijiumauma na kupata kigugumizi – hujaribu kuizima hoja haraka iwezekanavyo lakini kwa kufunikafunika na siyo mjadiliano ya wazi. Hii inaashiria jambo na wengi wamekuwa wakisema jamani mambo sii sawa tusemezane kwa uwazi yaishe..hii ni ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Huhitaji kuwa mtaalam wa mambo ya mahusiano kujua iko shida. Nakumbuka miaka ile Rais wa JMT Mh Mkapa alipoulizwa kuhusu hali ya kutkuelewana kule Zanzibar kulikotokana na uchaguzi aksema waache wayatatue wenyewe na yeyé hayamhusu – hupati jibu.

  Tanzania tunafahamu Polisi walivyo ‘makini' kudhiti mara moja mihadhara inayopotosha, na matamko na matendo ya uvunjifu wa amani kwa upande wa bara.Kwa upande wa Zanzibar hali ni tofauti tunakaa kimya na kupuuzia – tumeskia mara nyingi mabaa, makanisa na mal iza wasio wenyeji wa Zanzibari kuchomwa moto, lakini juzi hatusikii yalivyoshughulikiwa na kumalizwa.. tunatumiaa ‘kids gloves'

  Juzi nimeshangaa kumsikia Waziri wa mambo ya ndani Mh Nchimbi akikiri kuwa kikundi cha Uamsho kimekuwa kikiendesha mihadhara ambayo haijengi ila kubomoa kwa mwaka mzima na huku wakilindwa na polisi … unajiuliza iliwezekanaje? Kila mara kuhusu Zanzibar tunafumba macho halafu yakiwa mabaya tunakurupuka na kutaka kuyashughulikia kama dharura, hali ya hatari.

  Tujifunze kuweka mambo wazi ruhusuni watanzania wasemezane kwa uwazi hii itatuletea muafaka, utengemano na amani ya kweili siyo ya shurti.

  Usiri na woga wa JMT ndiyo unatuletea haya tunayoyaona na wasipokuwa makini watauvunja muungano kwa mikono yao wenyewe

  wanasema:

  • ..... mwana kulia .....
  • ...... guu huota tende


  Nawasilisha
   
 2. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka nyimbo za mchakamchaka ..
  ..Thinkers mmechoka??
  ..Bado
  ..Mbona hamuimbi?
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  serikali haijakaa kimya. inachunguza kwa makini swala hili. ni swala ambalo ufumbuzi hauji baada ya siku moja tu.

   
Loading...