*JKT yatangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi

moyafricatz

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Messages
1,378
Points
2,000
moyafricatz

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2015
1,378 2,000
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) anawatangazia Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2019.

Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambapo muombaji anaishi.

Zoezi la kuchagua vijana linaanza mwezi Juni 2019. Vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa mwezi Agosti 2019.

Aidha, kwa upande wa vijana wa Mujibu wa sheria, Jeshi la Kujenga Taifa limetoa orodha ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita 2019 kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa kuanzia tarehe 11 Juni 2019 hadi tarehe 16 Juni 2019.

Orodha kamili ya majina ya vijana wa mujibu wa sheria waliochaguliwa awamu pili na makambi ya JKT waliopangiwa na aina ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go tz.

Mkuu wa JKT anawaalika vijana wote waliopata fursa hiyo kuja kujifunza Uzalendo, Ukakamavu, Stadi za kazi, na stadi za maisha zitakazowasaidia kujiajiri mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.

Sifa za Muombaji ni kama ifuatavyo-:
1. Awe raia wa Tanzania

2. Umri
a. Kwa kijana wenye elimu ya darsa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
b. Vijana wenye elimu ya kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20

c. Vijana wenye elimu ya kidato cha sita umri usizidi miaka 22.

d. Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usizidi miaka 25

e. Wenye elimu ya Shahada umri usizidi mika 26.

f. Shahada ya uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 30.

g. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu umri usizidi miaka 35.
3. Awe na afya njema,akili timamu na asiwe na alama yoyote ya mchoro mwilini (Tatto)
4. Mwenye tabia na nidhamu nzuri na hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
5. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha Nnne awe waliomaliza 2016,2017,2018 na wenye ufaulu ufuatao.

a. Wawe wamefaulu na wawe na alama(Points zisizopungua 32)
b. Kidato cha sita wawe na ufaulu daraja la kwanza hadi daraja la Nne.

6. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

7. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa shule (Original Birth Certificate).

8. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving).

9. Awe na cheti cha matokeo (Original Academic Certificate /Transcript.

10. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi,Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuariliwa na Idara nyingine Serikalini.

11. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

12. Asiwe amejiushisha na matumizi ya madawa ya kulevya bangi, na yanayofanana na hayo.

13. Kwa wale wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali na Sanaa sifa za elimu nia sawa na zilizotajwa hapo juu.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-
1. Bukta ya rangi ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu.

2. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
4. Soksi ndefu za rangi ya nyeusi.
5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
6. Truck suit ya rangi ya kijani au blue.
7. Flana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.( dark green Tshirt with round colar).
8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
 
Bonde la Baraka

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Messages
3,192
Points
2,000
Bonde la Baraka

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2016
3,192 2,000
Zamani sisi tulibeba tranka au begi la nguo tu siku hizi vifaa unabeba toka home, zama zinabadilika kwa kasi.
Vijana kwa utawala huu wa mzee Magu kabla hamjaenda kujitolea tafuteni angalau takwimu za Opereheni Kikwete mpaka ile ya mwisho ya mwaka juzi wameajiriwa kwa % ngapi.
Ila kama mnataka kwenda kujitolea kama ilivyoandikwa nendeni.
 
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2014
Messages
13,700
Points
2,000
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2014
13,700 2,000
Wiiiii waaaaah x2
Tunaondokaa ahayaa twendee x2
Chini kuna motooo kanyangaa

Cindera cindera mama weeee,waambie raha ya depo mama weee
Ila daah nashangaaa katoto kadogo kana bambataaa
 
nasry9819

nasry9819

Member
Joined
May 16, 2016
Messages
61
Points
125
nasry9819

nasry9819

Member
Joined May 16, 2016
61 125
Zamani sisi tulibeba tranka au begi la nguo tu siku hizi vifaa unabeba toka home, zama zinabadilika kwa kasi.
Vijana kwa utawala huu wa mzee Magu kabla hamjaenda kujitolea tafuteni angalau takwimu za Opereheni Kikwete mpaka ile ya mwisho ya mwaka juzi wameajiriwa kwa % ngapi.
Ila kama mnataka kwenda kujitolea kama ilivyoandikwa nendeni.
sahh bro. tuliopo huku tupo njian kuachia nyoya.
ushauri. kma mtu unadil zako ni bora kukomaa nalo. jkt hii sio jkt ile.....
 
The Crushing

The Crushing

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Messages
575
Points
1,000
The Crushing

The Crushing

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2018
575 1,000
hebu nipeni ushauri wa mwisho kuna mdogo wetu alimaliza mwaka jana jiwe anawashwa sana kwenda huko .Nipeni maneno mawili matatu nikate mzizi wa fitina kwake
 
mchana kweupee

mchana kweupee

Senior Member
Joined
Apr 18, 2019
Messages
172
Points
225
mchana kweupee

mchana kweupee

Senior Member
Joined Apr 18, 2019
172 225
nmekwenda kujiandikisha na jkt nina cheti cha lasaba cha form4 nina cheti cha kompyuta cheti cha umeme na cheti cha ujasiliamali kisa cheti cha kuzaliwa sijakiona nmepeleka affidayit of birth wamenkatalia
 
uswaswa

uswaswa

Member
Joined
Mar 10, 2019
Messages
41
Points
125
uswaswa

uswaswa

Member
Joined Mar 10, 2019
41 125
dah hivi hilo la kuandaa nauli ni kweli nauli wanajitegemea?nakumbuka enzi zangu tulipelekwa kwa gharama zao ni tranka tu ndio tulibeba,Leo hadi shuka munabeba home?dah!pumzika kamanda wangu lut kanal mmari,sijui yupo wapi meja mzee,adjutant Lut Tesha, RSM erick mundeba, dah salaam nyingi kwa wote waliopigia kozi 833kj,nayamis Yale maisha ila madogo saivi wako busy kubadili umri ili wapate kwenda wanadhani kuna ajira.
 
M

Mpombote

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Messages
1,200
Points
2,000
M

Mpombote

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2017
1,200 2,000
nmekwenda kujiandikisha na jkt nina cheti cha lasaba cha form4 nina cheti cha kompyuta cheti cha umeme na cheti cha ujasiliamali kisa cheti cha kuzaliwa sijakiona nmepeleka affidayit of birth wamenkatalia
Kafatilie Kama upo mkoani ukija Dar utapata Fasta withi 7 au 14 days gharama ni 20,000 kama sikosei.
 
M

Mpombote

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Messages
1,200
Points
2,000
M

Mpombote

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2017
1,200 2,000
Hali ikoje huko jkt mtujuze jamani tusije kupoteza nguvu na muda.
Nenda tu mkuu ila kuna OP kama 3,4 hivi pia juzijuzi nilikutana na jamaa kwenye USAILI alikuwa ni wa OP iliyotemwa mtaani ya 2016.

Kila la kheri kapambane mkuu.
 
ip_mob

ip_mob

Member
Joined
Nov 14, 2016
Messages
38
Points
95
ip_mob

ip_mob

Member
Joined Nov 14, 2016
38 95
Wiiii waaa, yanyukwe yakobolewe...
Jambo afande, jambo kuruti (u)..
Kipindi kile tulikuwa tunapewa kila kitu aisee.
Nakumbuka msaga sumu (vampire) wa danger coy alivyokuwa anasulubisha vijana combine d..
Kipindi kile CO alikuwa Captain Mbugi, nadhani siku hizi atakuwa kanali.
 

Forum statistics

Threads 1,303,744
Members 501,077
Posts 31,490,832
Top