JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

Bradson

Member
Dec 26, 2019
66
89
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2020, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai 2020. Aidha, mafunzo hayo yatafunguliwa kuanzia 01 Agosti 2020.

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha, kutokana na ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID-19) Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo zitachukuliwa kipindi chote vijana watakapokuwa makambini.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.

2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)

3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.

4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

7. Track suit ya rangi ya kijani au blue

8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye jina la kambi hapo chini.

BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2020

Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako

 
JKT ni kuwapotezea muda vijana.

Mafunzo ya JKT hayajawahi kua na maana yoyote.

Kwenda kufundishwa kukesha usiku kucha, sijui kugalagala kwenye matope eti ndio uzalendo sijui ukakamavu.

JKT kuwapotezea muda vijana, muda amvao wangeweza kuzalisha au kufanya mambo ya maana kwenye maisha yao.

JKT badala ya kufundisha watu ujuzi wanaenda kufundisha watu kukesha, kumwagilia bustani, sijui kufanya ujinga gani mwingine eti ndio uzalendo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom