JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 14, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  [h=3]JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA [/h]

  Na Gladness Mboma, Dodoma
  Majira

  KAMBI ya Upinzania Bungeni, imeshtushwa na kitendo Jeshi la la Kujenga Taifa (JKT) kuingia mkataba na Bw. Jeetu Patel kuingiza matrekta nchini wakati anakabiliwa na kesi ya wizi wa
  mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT) kwenye akaunti ya malipo
  ya nje (EPA) na kesi yake bado inaendelea .

  Kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuwaeleza
  Watanzania juu ya jeshi kumtumia mtuhumiwa wa wizi wa fedha za walipa kodi kuingia
  makubaliano ya kibiashara kwa kutumia udhamini wa fedha za walipa kodi.
  Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani –Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw.
  Joseph Selasini aliyasema hayo bungeni wakati alipokuwa akitoa hotuba kuhusu
  Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012.

  “Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi inayoitwa “Public good,rents and business in
  Tanzania” iliyotolewa na Bw. Brian Cooksey iliyotolewa Juni mwaka jana inasema kuwa
  serikali imetoa udhamini wa sh. Bilioni 40 kwa SUMA-JKT na shirika hili la jeshi
  likaingia mkataba na Bw. Patel kuingiza matrekta hapa nchini , sasa ni kwa vipi
  tena jeshi linaingia nae mkataba wa kufanya mabakubaliano na India kwa udhamini wa
  fedha za walipa kodi,”alihoji.

  Bw. Selasini alisema kuwa taarifa ya Waziri inaonyesha kuwa sh. Bilioni 1.123
  zilitumika kwa ajili ya utoaji wa matrekta hayo bandarini na hadi sasa matrekta hayo
  yamewekwa Mwenge Dar es Salaam na mengine wameyaona hapo maeneo ya Kisasa Dodoma.

  “Swali la kujiuliza ni kweli matrekta haya ni mali ya jeshi au kuna Maofisa wa jeshi
  wanafanyabiashara hiyo kwa kutumia jina la jeshi
  na kama ni mali ya jeshi Waziri
  alieleze bunge hili jeshi lilitarajia kupata faida kiasi
  gani baada ya kufanya hiyo
  biashara ya kuuza matrekta hayo,”alisema.

  Alisema kuwa kitendo cha jeshi kujiingiza kwenye biashara ambayo siyo jukumu lake
  kimsingi linawatia mashaka makubwa sana kama kweli jeshi linatumika kufanya
  biashara na baadhi ya watu.

  “Hoja hii inapata nguvu kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa waziri wakati
  akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya ulinzi na Jeshi la
  Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2010/2011 katika haya ya 24 inayohusu shirika la
  Nyumbu.

  Katika mwaka wa fedha 2009/2010 Shirika la Nyumbu limekamilisha kuandaa mpango
  mkakati wake wa muda mrefu ambao una lengo la kuliganya shirika kuwa kituo maalum
  cha kuendeleza teknolojia za magari, mitambo ya ndani na nje ya nchi, kufanya
  utafiti na uzalishaji mdogo mdogo wa bidhaa na vipuri mbalimbali kwa ajili ya sekta
  za ulinzi na usalama,kilimo, viwanda na usafirishaji,”alisema.

  Alisema kuwa Kambi ya Upinzani ilitegemea kuwa Jeshi la Wananchi lingeingia mkataba
  kwa ajili ya kuimarisha taasisi ya Nyumbu ili iweze kuzalisha vifaa mbalimbali
  vitakavyokuwa vinatoa teknolojia rahisi katika mchakato mzima wa uzalishaji wa mazao
  ya kilimo.

  Bw. Selasini alisema kuwa hiyo sera mpya iliyoletwa na jeshi na kuhalalishwa na
  serikali , yaani jeshi kujiingiza katika masuala ya biashara ya kichuuzi ya kununua
  kwa mkopo na kuuza, badala ya jeshi kuwa Taasisi, mfano kwa kuvumbua na kusambaza
  teknolojia katika Nyanja mbalimbali za uzalishaji na hivyo kuinua uchumi wan chi
  inatia shaka na doa kwa jeshi.

  Alisema kuwa hoja hiyo ya jeshi kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara na matapeli
  wakishirikiana na baadhi ya Makamanda Wakuu wa Jeshini, imejidhihirisha wazi katika
  taarifa iliyotolewa na gazeti la kila siku “Dira ya Mtanzania” la Julai 4-6 mwaka
  huu.

  Bw. Selasini alisema kuwa kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani imeitaka serikali
  kutoa taarifa ya kina kuhusiana na taarifa hiyo na ni hatua gani za kinidhamu
  zimechukuliwa kwa Maofisa hao wa jeshi.

  Alisema kuwa taarifa hiyo ni mwendelezo wa taarifa ambazo zilikwisha lalamikiwa na
  jamii jinsi ambavyo Bw. Visran Sileshi alivyokuwa akifanya biashara haramu na
  baadhi ya makamanda wa jeshi na mwisho ilikuwa kwa jeshi kununua vifaa vibovu kwa
  bei kubwa sana.

  Msemaji huyo wa kambi ya upinzani aliongeza kuwa kwa hali ya kawaida kuna wananchi
  ambao kutokana na utundu wao wa asili wanatengeneza silaha kama magobore, lakini
  badala ya jeshi kuwachukua wananchi hao na kuwaendeleza, serikali inawafungulia
  mashtaka .

  Alisema hali hiyo ni kuwafanya wananchi wenye uwezo wa kubuni na kutengeneza baadhi
  ya vifaa kuogopa na hivyo vipaji vyao kupotea kabisa jambo ambalo alidai kuwa ni
  hatari kwa Taifa dogo kama Tanzania.

  Bw. Selasini alisema kuwa usiri ambao unaendelea katika miradi , kampuni ya jeshi
  umeendelea kuitia hasara nchi, kwani Kambi ya Upinzani kwa miaka mitano iliyopita
  imekuwa ikihoji umiliki wa mgodi wa meremeta na serikali imeshindwa kutoa majibu
  sahihi,ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda aliamua kulieleza Taifa kuwa Meremeta ni
  suala la ulinzi na usalama na hivyo ni siri na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji
  tena na mjadala ulifungwa.

  “Usiri huu umewaacha wananchi wa Buhemba ambao hadi muda huu bado walikuwa na madai
  mbalimbali dhidi ya kampuni hiyo ya Meremeta . Kambi ya Upinzani inasema kuwa
  kampuni hiyo ilikuwa ni ya kibiashara na hivyo bado tuna haki kabisa ya kuendelea
  kuhoji ubadhirifu wote uliofanywa na baadhi ya watendaji jeshini kwa mgongo kuwa
  kila jambo ambalo liko chini ya jeshi ni siri na hakuna mamlaka ya kohoji jinsi
  linavyoendeshwa,”alisema.

  Alisema kuwa kuna usemi unaosema kuwa “no taxation without representation” kama
  ulivyotolewa na Katibu Mkuu wa Inte-Parliamentary Union, Bw. Anders John pamoja na
  Mkurugenzi wa Geneva Center for Democratic control of armed forces, Balozi Dkt.
  Theodor Winkler .

  Bw. Selasini alisema kama bunge linapitisha fedha za walipa kodi kwa matumizi ya
  taasisi za jeshi, ni lazima wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge waelewe nini
  kinafanyika na wawe na mamlaka ya kuhoji matumizi ya fedha hizo.

  “Hivyo basi kaulia aliyotoa Waziri Mkuu bungeni kuwa suala la Meremeta limefungwa
  na halitakiw kuhojiwa tena kwa kuwa ni siri ya jeshi halina mashiko na ni utetezi
  dhaifu, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya jeshi ilianzishwa kwa
  fedha za wananchi na wabunge ni wawakilishi wa wananchi.

  Bw. Selasini alisema kuwa pia kumekuwepo na matumizi mabaya ya vifaa vya jeshi kwa
  matumizi ya kisiasa na binafsi ya wanasiasa, jambo ambalo limeendelea kuongeza
  gharama kwa jeshi hilo na kwamba mifano hai ni mwaka juzi zilitolewa taarifa za
  kuanguka kwa helikopta ya jeshi mkoani Manyara iliyokuwa imebeba wazungu waliokuwa
  kwenye ziara binafsi kwa idhini ya ya Waziri wakati huo Professa Juma Kapuya.

  Alitoa mfano mwingine ni ule wa juzi, ambapo ndege ya jeshi ilitumika kumsafirisha
  Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw, Freeman Mbowe kwenda Arusha kutekeleza amri ya mahakama
  na ndege hiyo ilirudi ikiwa na rubani pekee , kwamba hayo ni matumizi mabaya ya
  rasilimali za Taifa na halikubaliki.

  Bw. Selasini alisema kuwa Kambi ya Upinzani inaamini kwamba kwa njia ya utunzi wa
  sera na sheria za ulinzi zitakazotungwa zitakuwa zimewahusisha wanachi kwa kiasi
  kikubwa na zitasaidia kuondoa migongano isiyokuwa na tija kati ya jeshi na wananchi
  ikiwa ni pamoja na kuondoa kabisa matumizi mabaya ya askari wa jeshi katika
  kushughuli za kisiasa kama ambavyo imekuwa ikijitokeza katika hatua mbalimbali za
  mchakato wa uchaguzi.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, Taarifa ya wizara kama ilivyowasilishwa kwenye kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, inaonyesha kuwa katika utekelezaji wa miradi yake ya kuendeleza utafiti, ni jeshi kukamilisha utafiti wa "power tiller", kukamilisha utafiti wa gari la Nyumbu. Kambi ya Upinzani inauliza hili gari la nyumbu ambalo mwaka 2004 lililetwa hapa katika viwanja vya Bunge kuwaonyesha waheshimiwa wabunge likiwa limekamilika, leo tena tunaambiwa bado, kuna nini kinaendelea?
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, Makampuni haya yote ni makampuni ya kibiashara na tunatarajia kwa kuwa yanafanya biashara, hivyo ni wajibu wake kuweka kumbukumbu za taarifa zake wazi na hivyo kuondoa dhana ya usiri iliyokithiri katika jeshi la wananchi. Katika takwimu zote ambazo Bunge hili limekuwa likizipokea toka wizarani hatujawahi kuletewa taarifa za uendeshaji wa hotel ya Ndege Beach.Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kuelewa hotel hiyo inaendeshwa kibiashara au inafanywa kama sehemu ya viongozi wa kijeshi kupumzikia kwao na familia zao tu? Kuendesha hotel kunahitaji taaluma ya uendeshaji wa mahotel na kama ndio hivyo, waajiriwa katika hotel hiyo wanapatikana kwa mfumo upi? Tukumbuke kuwa mali za jeshi ni mali za walipa kodi na sio mali binafsi za maafisa wa jeshi.
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Chang'ombe furniture Ltd hutengeneza samani za mbao za aina mbalibali kulingana na mahitaji ya mteja, samani ni pamoja na zile, za Majumbani, Maofisini, Mashuleni na Makanisani. Waheshimiwa wabunge, kupitia vikao mbalimbali wamekuwa wakitoa ushauri mbalimbali kwa Serikali kuhusiana na umuhimu wa Serikali kununua samani za majumbani na maofisini zinazotengenezwa na viwanda vyetu vya ndani badala ya kununua samani hizo toka nje ya nchi.
  Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasema hivyo kutokana na mapato yasiyoridhisha yanayotokana na makampuni saba ya jeshi kwa fungu 39 na fungu 57 ya shilingi milioni 71.7 tu wakati fedha zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo kwa mafungu hayo ni shs. Bilioni 132.18 Kwa kuangalia uwiano uliopo kati ya mapato na uwekezaji (pesa zinazotengwa). Kambi Rasmi ya Upinzani inasema hayo kutokana na ukweli kuwa mapato yanayotokana na mashirika hayo hayaoani na matumizi yake (kiasi ambacho kinatengwa na serikali katika kuendesha mashirika hayo). Bado tuna kumbukumbu ya ni mambo gani hasa yaliyosababisha Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria kukwama. Hili halikuwa siri bali ni kutokuwapo kwa nidhamu ya matumizi na usimamizi wa bidhaa zilizokuwa zinazalishwa na taasisi hiyo. (POLOLO)
   
 5. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika, kuna usemi unaosema kuwa "no taxation without representation" kama ulivyotolewa na Katibu Mkuu wa Inter-Parliamentary Union, Mr. Anders B.John pamoja na Mkurugenzi wa Geneva Center for Democratic control of armed forces, Balozi Dr. Theodor Winkler. Kama bunge linapitisha fedha za walipa kodi kwa matumizi ya taasisi za jeshi, ni lazima wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge waelewe nini kinafanyika na wawe na mamlaka ya kuhoji matumizi ya fedha hizo.

  Hivyo basi,Kambi ya Upinzani inasema kauli aliyoitoa Mhe. Waziri Mkuu bungeni kuwa suala la MEREMETA limefungwa na halitakiwi kuhojiwa tena kwa kuwa ni siri ya jeshi halina mashiko na ni utetezi dhaifu, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya jeshi ilianzishwa kwa fedha za wananchi, na wabunge ni wawakilishi wa wananchi.
   
Loading...