JKT - Makutupora - OP Vyama VINGI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JKT - Makutupora - OP Vyama VINGI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Dec 3, 2009.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  JF

  Nafungua mjadala wetu hasa tuliopita JKT miaka ile ya 90. ni kukumbushana tu na kutafutana tupo wapi - Kifupi mimi nilikuwa mlinzi wa kuni pake makutu na jamaa mmoja myamwezi wa sikonge kwenye kile kibanda chetu pale.

  Kwa wana Makutu hasa D. Coy mnamkumbuka Matondo au shemeji? na je mnakumbuka misemo hii
  1. Doso kafie kwenu
  2. Kindipundipu
  3. Usawa wa Guduria
  4. Mzakwe ( kwa wale walikuwa wanapiga mnazi wa dodoma)
  5. Kupiga Tosi
  6. Kichele
  7. Mitunduruni
  8. Madikokiko
  9. Kupiga Burst
  10. Kalinye-Kalinye
  11. Songombingo
  12. Kujongo
  13. Kurutuuuuuuu...

  Misemo hii ina ilikuwa na maana yake, kwa wale waliopitia Makutu watafurahi na wanayo mingi

  Jamani tukumbushane enzi zile za kina afande Mwiba, Zimwi etc mfano palikuwa hapatoshi kama unajongo (unatoroka) then ukutane na Zimwi ha ha ha
  Manake ataanza Kalinye-kalinye then songombingo harafu anamalizia na doso kafie kwenu...nafikiri ukitoka hapo hutatamani kula
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Mkuu kwa kunikumbusha enzi hizo. Mimi nilikuwa B Coy na mshikaji wangu Masanilo. Nimemkumbuka sana CPL Kimbunga aliyekuwa anatamba kwamba amesoma hadi Std 7 (form seven) lakini anachukua mabinti wa nguvu, form 4 na 6!! Usimsahau adjutant (Kingu) aliyekuwa na rekodi ya kupitia hadi wasichana 80 kwa mwaka na anatunza rekodi zake kwa kila mwaka!!!

  Halafu nimekubuka kuwa tulikuwa tunatesa sana na Zabibu. Usiku tunakwenda na viroba na kuvijaza (not stealing, just taking some). Washikaji akina Kwame Makame, Jenge na TT wanawatumia wake zao huko Serengeti!!!!!
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  Hayo maneno mimi naona yalikuwa karibu JKT zote isipokuwa machache machahe tu kama Mitunduruni na wakati tukiwa ruvu tuliita Vibwende.

  Neno nililolipenda ni USAA A GUDURIA na kuna neno hapo umelisahau POLOLO.

  Mimi nilikuwa RUVU kama kuruta na Service nilikuwa Mgulani.

  Kweli **** mengi tulijifunza huko ambayo sio rahisi kuyaeleza.
   
 4. C

  Chechenya Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wale wa VIBWENDE KWA BABU MPO? Nakumbuka tulipokuwa tunaenda kuhamia ndenge kwenye shamba la mpunga Ruvu. Tulikuwa tunallala tu tukisema wacha ndege wale mpunga kwani walikuwa hawaji na magunia ya kubebea.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sisi tulikuwa phase A kula mayai tu.
   
 6. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Ndani ya Makutu mi nilikuwa E-Coy (Eagle Coy).
  Nilikuwa na messtin mbili, kubwa na ndogo. Ile kubwa niliikarabati ikawa supersize, usawa wa gudulia inapakia si mchezo.
  Ilikuwa vurugu na maafande NCOs akina Mwiba, Matondo, Kimbunga, Mwashambwa, n.k.
   
 7. m

  madule Senior Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! iI wish wasingefuta JKT, habari hizi nzuri nimezikosa! Jamani sikufanikiwa kwenda JKT kipindi namaliza chuo nilikuwa tayari nimejiandaa kujiunga JKT mara likafutwaaaaa! na sasa tunapata historia kama hizi FOR sure I missed somthing
   
 8. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du!!!,Kiongozi umenikumbusha mbali sana,Mie nilikuwa Eagle coy Mafinga,Then Chale Coy Itende JKT operation miezi sita,unanikumbusha mwendo wa kuruta ni kunyakua!!
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka zangu wawili na dada yangu mmoja walipita jeshini, mie wakati nipo frm five wakaifuta. kweli wote walikuwa wakisimulia mpaka utafurahi. my bro wa kwanza alikuwa oljoro jkt, anasimulia kuna siku alikuwa anajongo saa kumi usiku ili aende morogoro idm kurudisha form za chuo akakutana na watu km saba hivi wana jongo wakaungana basi mwendo km wa nusu saa hivi wakakutana na afande duh ilikuwa balaa waliruka kichura na kukwepa ndege for 2hrs, funny enough kati ya watu aliokuwa anakwepa nao ndege siku hiyo sasa hivi ni shemeji yetu hahaa wakikutana utacheka mpaka mbavu zichanike, pamoja na kukamatwa kesho yake akajongo vile vile. sister wangu alikuwa mafinga jkt six months halafu akamalizia itende mbeya anakuambia mkwara wa afande mafinga hapo alitishia kumzika mtu mzima mzima, jamaa alikuwa mtoto wa kibosile katoka dar anajifanya eti mayai akapewa adhabu ya kuchimba handaki la afande jamaa 2days akamaliza alipomaliza afande akamwambia wewe ndo afande ingia kwenye makao ya milele, jamaa hajui nini kinaendelea akaingia afande akamfukia jamaa kikabaki kichwa alafu alaletewa simu ya ttcl ampigie baba yake ampe hi, unaambiwa jamaa kesho yake akajongo. bro wangu mwingine alikuwa mgambo jkt tanga anakuambia maafande walikuwa wakifa sana na ngoma coz wanawarubuni mademu hawatawapangia kazi ngumu, basi ni kumega kwa kwenda mbele. anakwambia mademu wakipewa bukta na green vesti ya kijani km maafande walivyokuwa wakiziita,siku za kwanza wanaona aibu vibukta vifupi lkn kwata likishika hatamu wanazoea hata hawakumbuki tena ule ufupi. all in all sisi ambao hatukupitia gesh, tumekosa mambo mengi sana hata dada zetu wa siku hizi si wakakamavu tena
   
 10. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekugongea thenks mkuu,umenikumbusha GREEN VEST YA KIJANI!!!
   
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Naukumbuka uwanja wa damu pale makutupora. Mwendo wa kunyakua usawa wa gudulia . . . utakula kwa jasho lako mwenyewe! Nakumbuka kwenda porini "kukata" kuni bila panga wala shoka. Na lazima urudi na kuni zilizokatwa. Na zilkuwa zinakatwa kweli na kuepelekwa kwenye Coy bila panga wala shoka . . . akil kichwani! Nakumbuka ile mitunduru. . . kujongu mbele kwa mbele. Bigula likilia tu ... haooo mitunduruni! Nakumbuka disko a.k.a chenja: mara ya kwanza nilidhani ni disco la kweli kumbe ni kwenda kuimba nyimbo za kijeshi mpaka usiku kati. Jeshi acha bwana! Aliyelifuta amefuta kitu cha thamani.
   
 12. kilema

  kilema Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ha sisahau! Niliambibiwa na afande niazime apetite kwa mwenzangu kama sina
   
Loading...