JKT, Mafunzo yenu yamevamiwa na raia wa kigeni bila ninyi kujua

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Mafunzo ya JKT yanalenga kuwanufaisha Watanzania waweze kuilinda nchi yao. Lakini napenda kuwapa alert JKT, JWTZ na POLISI kwamba mmevamiwa na hii nikutokana na kukosa umakini katika kusajili askiri.

Wapo vijana zaidi ya mia mbili wameingia kwenye vyombo vyetu nyeti baada ya kufunguliwa kwa milango ya JKT, wengi wao wamebadili majina ya ukoo na wazazi wao walifanikiwa kuwatengenezea vyeti vya kuzaliwa vya kuthibitisha wamezaliwa DAr, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Mbeya na kupitia njia hiyo hakuna aliyewatilia mashaka.

Hivi vyombo vyetu vinajua kwamba wageni walioingia baada ya machafuko ya nchi jirani miaka ya nyuma sana walisajiliwa mashuleni Tanzania? Wanajua kwamba walifaulu na kuendelea na masomo? Wanajua kuwa watoto na wajukuu wa wageni hao wapo kwenye ajira serikalini? Au wanadhani wageni hawasomeshi watoto wao hapa Tanzania?Je hao watoto Kama wamesoma hawakupelekwa JKT? Kama walikwenda hawakupangiwa kwenye vyombo vya ulinzi? Kama walipangwa tunaamini ni wazalendo kwa nchi hii? Kama siyo wazalendo ni wazalendo wa nchi gani Kama siyo nchi zao za asili?

Je, walipoendesha zoezi la vyeti feki hawakufanikiwa kuwaza kuwa kuna Watanzania mamluki kwenye utumishi wa umma? Kama wapo na wapo sekta nyeti walifanywa Nini? Je, Kama hawakufanywa chochote hawajaingiza watoto wao na watoto wa ndugu zao? Siku akitokea mtu akataka kuwachekecha hayatatokea tunayoyaona S.Afrika?

Tunaweza tukawalaumu S. Afrika lakini na sisi tunatengeneza bomu kupitia mifumo yetu ya mafunzo ya kijeshi ( tunaaandaa wanajeshi bila kuwapa ajira) lakini pia tumewajaza kwenye utumishi wa umma kwa sababu hatuchuji Nani aingie humo.

Wanaoelewa maana ya ulinzi wa nchi wataelewa maana ya kumjua mtu unayemkabidhi utumishi wa umma na nafasi ya kisiasa..S.Afrika wakimalizana sisi tutaanza kutafunana kwa sababu wasio Watanzania wamekabidhiwa dhamana ya Watanzania na Watanzania wamekabidhiwa dhamana ya kuwalipa mshahara wasio Watanzania.

XENOPHOBIA NI UZEMBE WA TAWALA
 
Ni kweli kabisaa zaidi nilichogundua upande wa kuwachukua sidhani kama wengi wanakuwa na vetting ya kutosha na kuthibitisha kama ni wenyewe...
 
Kwahiyo kama wameingia mpaka ndani ya TISS ni vigumu sana kuchomolewa kwa kuwa watakuwa wanafanya sabotage ya mkakati wowote utakaotumika ili kuwabaini.
Nalog off
 
Hy kitu ipo na binafsi niishuhudia nikiwa JKT (naomba nisiitaje kambi)

Nilikutana na vijana wawili, mmoja wa Kisomali na mwingine wa kinyarwanda.. tumepiga kozi mwanzo mwisho...

Baada ya kozi, mie niliamua kujiunga na masomo ya Chuo kikuu, bahati nzuri nikakutana tena na yule Mnyarwanda, anapiga kozi ya Wildlife Management..na Kalamba boom.

Kwa sasa ni miongoni mwa maofisa wa wanyamapori kwenye hifadhi yetu fulani hivi.

Msomali alibakishwa jeshini maana kilikuwa na shabaha kali kweli ,kwenye shabaha kiliingiza zote risasi 10 bila kupoteza hata moja, kikapewa zawadi ya laki moja.

TISS siku hizi nimambugira tu, miaka kadhaa ijayo mbona tutavuna tunachokipanda.
 
Hy kitu ipo na binafsi niishuhudia nikiwa JKT (naomba nisiitaje kambi)

Nilikutana na vijana wawili, mmoja wa Kisomali na mwingine wa kinyarwanda.. tumepiga kozi mwanzo mwisho...

Baada ya kozi, mie niliamua kujiunga na masomo ya Chuo kikuu, bahati nzuri nikakutana tena na yule Mnyarwanda, anapiga kozi ya Wildlife Management..na Kalamba boom.

Kwa sasa ni miongoni mwa maofisa wa wanyamapori kwenye hifadhi yetu fulani hivi.

Msomali alibakishwa jeshini maana kilikuwa na shabaha kali kweli ,kwenye shabaha kiliingiza zote risasi 10 bila kupoteza hata moja, kikapewa zawadi ya laki moja.

TISS siku hizi nimambugira tu, miaka kadhaa ijayo mbona tutavuna tunachokipanda.
Kweli mkuu.
Ajira za kujuana huko TISS na elimu yetu pia ni magumashi (kuokotana majalalani).
 
hata wewe unayo haki ya kwenda kupata ajira kokote ulimwenguni, kuna watanzania ambao ni maaskari wameajiriwa huko marekani, sudani, kuna wanajeshi wameajiliwa nchi mbali mbali huku wakiwa ni watanzania kabisa...na wengine wameajiliwa sekta nyeti kabisa huko kwenye nchi za watu...sisi sio wa kwanza kuajili wageni.

kwa kifupi serikalini kuna vetting nzuri tu inayofanywa ili kumtambua mzalendo ama sio mzalendo....kwenye majeshi yetu vile vile sio kila mwanajeshi anaaminiwa anaweza kuajiliwa na bado akawa hana madhara kwa nchi kwasababu mafunzo na siri za nchi hubadilika na kupanda kutokana na mtu anavyopanda cheo.., hapo huwezi kunielewa kipindi najiunga na kikundi fulani cha ulinzi hapa Tanzania mafunzo yangu ya kwanza niliyachukua kwenye mkoa mmoja hivi....miaka 20 iliyopita kunasehemu tulikuwa tunapitaga tukikimbia mchaka mchaka miaka hiyo...

mwaka jana nilibahatika kurudi pale chuoni nilipo pata mafunzo ya ulinzi...tukapelekwa sehemu ile ambayo tulikuwa tunapita tu ambako miaka ya nyuma hatukujua kuwa pale kuna hadhina kubwa sana ya nchi....miaka 20 nyuma tulivyokuwa tunaanza kuchukua mafunzo tulikuwa zaidi ya 4000 tuliobahatika kurudi pale na kuonyeshwa kilichopo pale hatuzidi 20...

nadhani umeona interval ilivyo hapo...ndio maana kuna watu wanazeeka bila kupata vyeo majeshini ni kutokana na jeshi kutokuwa na imani na baadhi ya wanajeshi wake...jeshi likikutilia shaka tu kama ukibahatika kuendelea kulitumikia hutopanda cheo...

sasa niambie ni waziri gani unamashaka nae kuwa si mtanzania..? nitajie askari yeyote mwenye cheo kuanzia nyota moja ambaye unashaka na uraia wake...?
 
Kunakitu wewe na mwanzisha uzi hamkijui: USA+UK+FRANCE huaingiza wageni kwenye majeshi yao(legions) straightaway kutoka kwenye nchi zao
mzee usibishane na wasio jua wanachokiandika, wanaleta story za kwenye vijiwe vya kahawa...wanachojua wao kila mwanajeshi anajua siri za nchi jambo ambalo sio ukweli kabisa...kuwa mwanajeshi na kujua siri za nchi ni vitu viwili tofauti...na ata ukiwa raia wa kigeni hakuna madhara kwani kuna vyeo kamwe mtu mwenye uraia pacha hawezi kufikia
 
Huyu alieandika hii posti kwanza aanze yeye kutudhihirishia uraia wake. Maana anaonesha kiasi gani Ana akili fupi.
 
Watu wengine akili zao zimeganda,kama baba kazaliwa Tanzania ni Mtanzania huyo, kama baba kazaa mtoto Tanzania, mtoto ni mtanzania huyo..
Angalizo zuri sana hili japo watakuja wajuaji kuhoji na kubisha lakini ukweli utabaki pale pale. Hali hii ni hatari kwa usalama wa taifa.
 
Back
Top Bottom