JKT kwa Mujibu wa Sheria: Serikali gharamieni haya mafunzo au yaondolewe. Sipingi kuwepo mafunzo, napinga gharama

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
574
1,000
Nije moja kwa moja kwenye mada,

JKT walitangaza vijana waliomaliza kidato cha SITA kujiunga na mafunzo ya JKT kwa MJIBU WA SHERIA.

JKT walitoa maelekezo vitu wanavyopata kuwa navyo watoto, ajabu unamnunulia Mtoto hivo vifaa walivyotaja wao, baada ya Mtoto kufika kambini anakutana na vitu vingine vya kununua kama buti, begi, nk. Kwa nini hivi vitu visitajwe ama kuorodheshwa moja Kwa moja?

Fikiria Mtoto ametoka Dar au Mbeya kwenda Kanembwa ni zaidi ya laki kadhaa, mzazi amejipiga piga alafu anafika kambini anakutana tena na kutakiwa kununua vifaa vingine.

Baada ya miezi miwili anatakiwa kurudi nyumbani Kwa ajili ya kuja kufanya maombi ya kujiunga na chuo kikuu.

Serikali ama ikubali kugharamia haya mafunzo au yaondolewe, sipingi kuwepo mafunzo napinga gharama anazoingia mzazi ili kufanikisha hili jambo
 

Sam mirror

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
980
1,000
Mwanao anahitaji kukupiga shtuka dingi, sema mtumie ukijua kajiongeza si unajua vijana apate ya kuvimbia kidg

Hakuna kitu kama icho jkt
 

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
574
1,000
Nauli watarudishiwa kuhusu buti beg hakuna kitu Kama hicho maana Kuna raba na buti pamoja na nguo za mazoezi ni bure
Huyo mwanao anajiongeza tu mpe hela ya matumiz kacheza na akili yako huyo
Hakuna nauli inayorudishwa huyu si wa Kwanza kwenda Jkt elfu2018 kijana alienda Mgambo Tanga, alivofika pia kulikiwa na kununua hayo mabegi na yanauzwa hapo kambini, hili la buti ndo halikiwepo, hoja yangu ni Kwa nini hivi vitu havioridheshwi direct?

Pili kijana wangu amesoma boarding tangu primary siyo MTU wa kupenda kuvimba na vijisent vidogo vidogo, ni kijana ambaye hata alipokuwa anafunga shule endapo amebakisha hela hununua zawadi kuwaletea ndg zake au mamake.

Hivo sitarajii kuwa anaweza sema inahitajika buti ili Hali haiitajiki, pia hela yake ya matumizi anayo nilimwambia nenda ukiona mambo magumu sepa na nauli nilimpa kabisa
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,476
2,000
Hakuna nauli inayorudishwa huyu si wa Kwanza kwenda Jkt elfu2018 kijana alienda Mgambo Tanga, alivofika pia kulikiwa na kununua hayo mabegi na yanauzwa hapo kambini, hili la buti ndo halikiwepo, hoja yangu ni Kwa nini hivi vitu havioridheshwi direct? Pili kijana wangu amesoma boarding tangu primary siyo MTU wa kupenda kuvimba na vijisent vidogo vidogo, ni kijana ambaye hata alipokuwa anafunga shule endapo amebakisha hela hununua zawadi kuwaletea ndg zake au mamake. Hivo sitarajii kuwa anaweza sema inahitajika buti ili Hali haiitajiki, pia hela yake ya matumizi anayo nilimwambia nenda ukiona mambo magumu sepa na nauli nilimpa kabisa
Mkuu unabishana na katoto ako hakajui lolote, kanakupotezea muda wako tu
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,476
2,000
Hakuna nauli inayorudishwa huyu si wa Kwanza kwenda Jkt elfu2018 kijana alienda Mgambo Tanga, alivofika pia kulikiwa na kununua hayo mabegi na yanauzwa hapo kambini, hili la buti ndo halikiwepo, hoja yangu ni Kwa nini hivi vitu havioridheshwi direct? Pili kijana wangu amesoma boarding tangu primary siyo MTU wa kupenda kuvimba na vijisent vidogo vidogo, ni kijana ambaye hata alipokuwa anafunga shule endapo amebakisha hela hununua zawadi kuwaletea ndg zake au mamake. Hivo sitarajii kuwa anaweza sema inahitajika buti ili Hali haiitajiki, pia hela yake ya matumizi anayo nilimwambia nenda ukiona mambo magumu sepa na nauli nilimpa kabisa
Mkuu unabishana na katoto ako hakajui lolote, anakupotezea muda wako tu
 

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
794
1,000
Mkuu unabishana na katoto ako hakajui lolote, anakupotezea muda wako tu
Sure hakajui kokote
Mimi nileienda kambi moja huko kaskazini wanakununulisha vitu almost vya laki moja hata kama unavyo eg. Viatu kwa lazima wakiona umeishiwa hela wanakata kwenye posho za 40 huwa wanatoa ko posho ikitoka huna hata mia.
Kama una mtoto wako kule mtumie sents tu maana sio poa
 

kobosir

Member
Jan 10, 2013
27
45
Mambo kama haya ni vema yakaangaliwa kwa kina, na ni vema yakiwa Pre Listed...Ifahamike kuwa mtoto haendi kwenye mafunzo ya kijeshi bali anaenda kukomazwa na kupewa uzalendo...anatoka bado akiwa raia. Hivyo hakuna haja ya kuweka ugumu wowote. Mambo yawe wazi ili sisi wazazi wa kudunduliza dunduliza tuweze kujipanga na kumudu gharama, sio swala zuri kumtia unyonge mtoto kuona Mshua kashindwa au ananicheleweshea kuninunulia hiki wakati wenzangu wote wanavyo.

Kwa upande mwingine yale mafunzo ni mazuri na ya muhimu sana kwa watoto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom