Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
JKT ilinipotezea muda wa mwaka mzima kabisa. Vile vile ilinifanya nikosane na kimwana wangu tuliyekuwa tumekutana high School na kuahidiana kuoana (kama kweli ahadi hiyo ilikuwa serious). Jambo nililochukia JKT zaidi ilkikuwa ni ile discipline ya woga na unafiki ambao ulikuwa unatokana na yale mafunoz ya msuli yaliyokuwa yakitolewa.
Hata hivyo JKT ilinikutanisha na watu wengi sana na kunifanya nijifunze mengi sana kuhusu jamii yetu. Ingawa sasa hivi sikumbuki hata mtu mmja kati ya marafiki hao niliokutana nao JKT, kwa miaka mitano ya kwanza tangu kumaliza JKT nilikuwa nakutana nao na walinisaidia sana kujenga network yangu hapo Dar.
Jambo ninalokumbuka sana ni pale nilipomaliza mafunzo ya ukamnada pale Ruvu na kupewa tepe moja ya kijani na kupandishwa cheo kutoka Serviceman na kuwa "Volunteer Lance Corpolar" au "Green Kwanja." Kwa miezi sita niliyotumia cheo hicho cha V-L/Cl niliwafanya kuruta walioningia Januari waione JKT kama sehemu ya mafunzo zaidi ya mateso; sikuhimiza discipline ya woga na nilikuwa mkali sana ninapopewa nidhamu ya ya kinafiki. Kwa bahati mbaya juhudi zangu zilikuwa ni kama punje ya mchele kwenye gunia zima; laiti wale makamanda wengine nao wangejifunza kwangu namna ya kuwatraini kuruta wale kiakili na kijamii.
Inawezekana ulikuwa na muono (vision) lakini hukujua jinsi ya kuigeuza iwe kweli na endelevu. In short you failed.