JKT kupewa tenda ya ulinzi kivuko feri ni sawa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Ktk hali iliyojaa utata jeshi la kujenga taifa limepewa kazi ya ulinzi katika vivuko vya kigamboni feri!
Tenda hiyo imejaa utata kwakuwa haikufuata taratibu za manunuzi na mkataba wao umekuwa ni siri kubwa!

Nachelea kuhoji why jkt walipwe kwa huduma ya jamii iliha nalo ni chombo cha umma na ndiyo kazi mahususi tulilipatia?

Hebu wadau wenzangu ni saidieni kufahamishwa ktk hili
 
JKT wanajitegemea kupitia shirika lao la uchumi suma jkt,si mbaya sana labda itasaidia kupunguza rushwa na kuongeza kipato ndani suma jkt!!
 
Na ndio maana foleni haiishi, wanajeshi wenyewe kwa rushwa wanaongoza, wakipewa buku mbili unapitisha no entry. Hapo unadhani wataacha kusababisha foleni ili mdfuko unone. Mie nimeshajichokea na hii Nchi unakaa kwenye foleni tangu kumi na mbili unavuka saa mbili na nusu, hizi kazi si tutafukuzwa sasa kila iku udachelewa kisa kivuko
 
kaka there is a day hila zao zitafichuka na watahaibika peupe!tunaona, tunashauri wanadharau!
 
Ktk hali iliyojaa utata jeshi la kujenga taifa limepewa kazi ya ulinzi katika vivuko vya kigamboni feri!
Tenda hiyo imejaa utata kwakuwa haikufuata taratibu za manunuzi na mkataba wao umekuwa ni siri kubwa!

Nachelea kuhoji why jkt walipwe kwa huduma ya jamii iliha nalo ni chombo cha umma na ndiyo kazi mahususi tulilipatia?

Hebu wadau wenzangu ni saidieni kufahamishwa ktk hili

yani wewe sikuelewi kabisa , unataka kazi ya ulinzi wapewe kampuni za kigeni ? wakipewa jkt unanuna nadhani unatatizo kubwa sana
 
yani wewe sikuelewi kabisa , unataka kazi ya ulinzi wapewe kampuni za kigeni ? wakipewa jkt unanuna nadhani unatatizo kubwa sana
Huja nielewa kabisa! Dhana yangu ni mazingira ya upataji wa tenda! Vilevile najawa na utata juu ya jeshi kugeuzwa kampuni ya ulinzi na kupewa kazi ya ulinzi ktk maeneo ya HUDUMA kwa jamii ambapa walistahili kuifanya bila malipo kwa kuwa ni jeshi letu tuliloliajiri!!
 
SUMA JKT ni shirika la jeshi la kujenga taifa si wanajeshi bali ni askari waliopitia jeshi kwa kujitolea na hawalipwi kama wanajeshi,suma jkt wana miradi mingi tu kama kushona nguo,kupaka rangi, ufundi ,na nk.na wanahaki ya kuomba tenda kama taasisi nyinginezo si vibaya ,ila tenda board za mashirika Tanzania huwekwa wazi kwa wote wanaoomba na siku ya kufungua wote mnatakiwa muwepo,baada ya mshindi wa tenda kupata mkataba wewe unautaka wa nini ?
 
Kama taratibu hazikufuatwa basi walaumiwe lakini km zilifuatwa basi tuangalie mission na vision za JKT na hapo 2tapata jawabu1
 
Ktk hali iliyojaa utata jeshi la kujenga taifa limepewa kazi ya ulinzi katika vivuko vya kigamboni feri!
Tenda hiyo imejaa utata kwakuwa haikufuata taratibu za manunuzi na mkataba wao umekuwa ni siri kubwa!

Nachelea kuhoji why jkt walipwe kwa huduma ya jamii iliha nalo ni chombo cha umma na ndiyo kazi mahususi tulilipatia?

Hebu wadau wenzangu ni saidieni kufahamishwa ktk hili

Ulitaka apewe nani? Pili ni vizuri ukaelewa kwamba ndani ya JKT kuna SUMA JKT ambalo ni shirika la uchumi na ndilo commercial arm ya JKT. Huu msisitizo wa sheria ya manunuzi ya umma umezidi sasa na watu hawajui kwamba si kila kitu kinatakiwa kifuate sheria ya mununuzi.
 
Back
Top Bottom