JKT inakanusha tangazo la kazi lililobandikwa hapa JamiiForums

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
c40908b4854d96697b5b4b4facfe7b13.jpg
d9095dbe6e0cd42d9ebf9bd79032f5e5.jpg


==============

Habari iliwekwa kwenye hii thread=>Nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT 2016
 
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la kujenga Taifa (JKT), linakanusha taarifa zilizotolewa kwa umma kupitia mtandao wa Jamii Forum, tarehe 11 machi 2016 kuwa, JKT limeanza mchakato wa kuchagua vijana mikoani na wilayani kujitolea kwa nia ya kujiunga na mafunzo ya JKT.
Aidha tangazo hilo linasomeka kuwa mwombaji awe mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 23 kwa wenye elimu ya kidato cha saba hadi cha sita, miaka 18 hadi 26 kwa wenye stashahada na miaka 18 hadi 35 wenye shahada na kuendelea. Pia asiwe ameoitia chombo chochote cha ulinzi na usalama.

Tangazo hilo kwa umma sio sahihi na halijatolewa na uongozi wa JKT kama linavyosomeka na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hadi tarehe 15 Machi 2016 JKT halijaanza mchakato wa kuchukua vijana wa kujiunga na mafunzo ya kujitolea. Muda mwafaka utakapowadia , wananchi watajulishwa rasmi kupitia vyombo vya habari vitakavyoainishwa.
Aidha JKT linazidi kuwakumbusha wananchi kuwa utaratibu wa kuwapata vijana wa kujiunga na JKT haujabadilika. Maombi yanaanzia wilayani na mikoani kwa kutoa uteuzi wa vijana,
Kulingana na nafasi zitakazotolewa kwa kila mkoa. JKT linawaomba wananchi wote kuzingatia utaratibu huo muda utakapowadia.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 15 Machi 2016
 
jamani tuwe makini na kila tunachopost, humu JF kuna wakuu wanafuatilia mambo yote...
 
Napenda forums baadhi nchi za watu, habari nyeti bila source reliable = BIG BAN na INAKUWA DELETED.
 
Sasa mbona jamiiforums hawaja wajibika kutupasha habari hii?
Kwani wewe ndio msemaji wa jamiiforums?
Au nawewe ni mmoja kati ya mods?
 
"wa miaka 18 hadi 23 kwa
wenye elimu ya kidato
cha saba hadi cha sita,"...hapa ndipo napoamini hii imetokea geshi
 
Umesomeka,uku kwangu Tulya,vijiji vyote vilishaanza nisumbua:kule migilango,doromoni,tulya!walishaanza nisumbua kwa maswali ya lini nafasi za jkt zitatoka!nashukuru kwa ufafanuzi?
 
Back
Top Bottom