Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,076
- 7,855
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

PRESIDENTS OFFICE, THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania.
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania.
Fax: 255-22-2113425 E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imetenga sh bilioni 31 kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha (2008/09) kwa ajili ya ruzuku ya mbolea ili kuwezesha upatikanaji wa uhakika zaidi wa bidhaa hiyo katika jitihada za kuwaondolea makali wakulima nchini na kuwawezesha kuongeza uzalishaji.
Hayo yameelezwa leo (Ijumaa, Agosti Mosi, 200 asubuhi na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anazungumza na wananchi wa eneo la Ifunda katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku nane mkoani Iringa.
Rais Kikwete amesema kuwa kiasi hicho cha ruzuku ni ongezeko la kiasi cha mara nne tokea Serikali yake ilipoingia madarakani Desemba, mwaka 2005
Tuliahidi kuongeza fedha kwenye mfuko wa mbolea; wakati tunaingia madarakani ilikuwa ni Sh bilioni 7 tukaongeza ikafika Sh bilioni 21, mwaka huu tumeongeza hadi Sh bilioni 31, Rais amesema
Hata hivyo, Rais Kikwete amewaambia wananchi wa Ifunda kwamba upatikanaji wa uhakika wa mbolea nchini utawezekana tu kwa kuongeza uzalishaji mbolea katika kiwanda cha mbolea cha Minjingu na kujengwa kwa kiwanda kipya Mtwara.
Tunafanya jitihada ya kuongeza upatikanaji wa mbolea zaidi kwa kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha mbolea cha Mijingu, ambako uzalishaji kwa sasa ni tani laki moja kwa mwaka; tunataka zifikie laki tatu. Jitihada zingine ni kujenga kiwanda cha mbolea kwa kutumia gesi asilia Mtwara. Tunategemea baada ya miaka mitatu tutakuwa tumetatua tatizo la mbolea, Rais ameongeza
Serikali itakuwa inaongeza ruzuku pale inapobidi lakini pia ameonya kuwa unafuu huo wa kuongeza ruzuku unaweza usionekane kutokana na kupanda kwa bei ya mbolea duniani.
Asubuhi hii, Rais pia amewasiliamia na kusikiliza matatizo yao wananchi katika miji ya Nyololo, Makambako, na Njombe. Rais pia atakagua Shule ya Wasichana ya Anna Makinda na kisha kuelekea Mlangali, Ludewa ambako atapokea taarifa ya wilaya.
Mwisho
Imetolewa na:
Premi Kibanga
IRINGA
01 Agosti, 2008
NB: Press Release attached.