kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,213
Mwisho wa mwezi July umekaribia, kama utaratibu ulivyo rais huwa analihutubia taifa ingawa siku hizi hujifanya yuko busy na kukwepa.
Naomba nimkumbushe kuwa kuna mambo mengi ya msingi ambayo unatakiwa kuyatolea ufafanuzi kwa kuwa watanzania yanatuchanganya. Kwa hiyo kwenye hotuba yako, pamoja na mambo mengine utakayoyaeleza, ujumuishe na haya.
1. utueleze kuhusu matatizo ya umeme na ufumbuzi wake. Chonde chonde naomba usituambie wewe sio wingu ukanyeshe mtera, maneno haya huwa yanatuudhi sana. Tunataka kusikia ufumbuzi wa haraka wa tatizo la umeme, hali ikiendelea hivi hata wewe utashindwa kusafiri nje, serikali itakosa mapato.
2. utueleze kuhusu hatima ya Ngeleja na Malima, watu wanawaomba wawajibike wao wametia pamba masikioni, wewe kama mwajiri wao unatuambia nini? Mimi siamini kama tatizo sio wao, hata huyo Jairo ni mbuzi wa kafara, naamini ule mchango wa pesa za "kuwarushwa" wabunge ulikuwa na baraka zao.
3. ule mpango wenu wa kupunguza bei za mafuta umefia wapi, mbona bei hazishuki, tatizo ni nini? mmewapandishia watu mafuta ya taa huku mkijua wale watoto mliowatelekeza kwenye shule za kata wanasomea vibatali ambavyo vinatumia mafuta ya taa. walimu hawana na sasa mnawaondolea hata uwezo wa kujisomea wenyewe, angalieni hilo bomu litawalipukia. Naomba ufafanuzi.
4. Pia naomba uzungumzie juu ya kuzidi kupanda kwa bei za bidhaa na kushuka kila siku kwa thamani ya shilingi, mmeshindwa kudhibiti?
5. La mwisho tuambie mafanikio uliyoyapata kwenye ziara zako tano za mwisho nje ya nchi, na ziara hizo zimeligharimu taifa kiasi gani.
Najua utakuwa na mengi ya kutueleza lakini haya yangu matano naomba uyatolee ufafanuzi, kwani yananikera, naamini kuna watanzania wengi pia yanawakera.
Naomba kuwasilisha