JK yuko Ufaransa ziarani

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
JK Ameondoka nchini Tanzania jana usiku kwa mwaliko wa Rais Hollande ili kuhudhuria mikutano miwili itakayofanyika nchini Ufaransa.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wiki hii atahudhuria mikutano miwili mikubwa ya kimataifa ukiwamo wa kujadili amani na usalama Barani Afrika kwa mwaliko wa Rais Francois Hollande wa Ufaransa.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumatano, Desemba 4, 2013, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika ambao watahudhuria Mkutano Kati ya Marais wa Afrika na Ufaransa, ambao utafanyika kwa siku mbili katika Kasri ya Elysee mjini Paris kuanzia keshokutwa Ijumaa, Desemba 6, 2013.

Mkutano huo uliopewa jina la Elysee Summit utakuwa ni mkutano wa 26 wa Mikutano ya Wakuu wa Nchi za Afrika na Ufaransa ambao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1973 kwa madhumuni ya kuzikutanisha Ufaransa na makoloni yake ya zamani katika Afrika.
Kwa mikutano miwili ya kwanza, washiriki walikuwa ni marais wa nchi za Afrika zilizokuwa makoloni ya Ufaransa lakini mwaka 1976 zilialikwa nchi zinazozungumza lugha ya Kireno katika Afrika kama watazamaji tu.

Mwaka 1981 jina na madhumuni ya mkutano huo yalibadilika na ukaanza kuitwa The Conference of Heads of States and Government of Africa and France na mwaka 1996 mkutano huo ulifunguliwa kwa nchi zote za Afrika bila kujali zinazungumza lugha gani. Awali mkutano huo ulikuwa unafanyika kila baada ya miaka miwili, sasa ni kila baada ya miaka mitatu.

Kama ilivyokuwa mkutano uliopita uliofanyika mwaka 2010 mjini Nice, Ufaransa, mada kuu ya Mkutano huo ni kujadili amani na usalama katika Bara la Afrika vikiwemo vita ndani ya nchi mbalimbali, uharamia kwenye bahari, biashara ya dawa za kulevya, ugaidi na ujambazi wa vikundi na jinsi mambo hayo yanavyoathiri Afrika na Ufaransa.

Aidha, Mkutano huo utajadili mada nyingine mbili ambazo ni Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo na Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Rais Kikwete na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Hollande watakuwa Wenyeviti-Wenza wa kikao kitakachojadili madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi. Rais Kikwete atakuwa Mwenyekiti-Mwenza wa kikao hicho katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) Juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).

Rais Kikwete anatarajiwa kuwaeleza viongozi wenzake matokeo ya Mkutano wa COP19/CMP9 uliofanyika karibuni mjini Warsaw, Poland kujadili suala zima la Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Mkutano mwingine mkubwa ambao Rais Kikwete atahudhuria ni ule wa marais wa Afrika utakaojadili jinsi ya Jumuiya ya Kimataifa inavyoweza kushirikiana kukomesha ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo na faru.

Katika Mkutano huo utakaofanyika Hoteli ya de la Marine, Rais Kikwete aanatarajiwa kuwaeleza viongozi wenzake kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali yake kukabiliana na ujangili nchini chini ya Operesheni Tokomeza.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

4 Desemba, 2013
 
Hivi nauliza, kwani vingozi wengine wakuu waliomtangulua JK mbona walikuwa hawasafiri mara kwa mara kama JK? Yeye ana nini na hizi safari? Kuna mtu mmoja aliwahi kusema eti bado anajiona ni Waziri wa Mambo ya nje!!!! Je kuna ukweli?

Tiba
 
Hapa naweza kupata ban..Ahsante Mkuu kwa taarifa..
 
CCM ni CHAMA CHA WAISLAMU

Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),

1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu
 
Hivi nauliza, kwani vingozi wengine wakuu waliomtangulua JK mbona walikuwa hawasafiri mara kwa mara kama JK? Yeye ana nini na hizi safari? Kuna mtu mmoja aliwahi kusema eti bado anajiona ni Waziri wa Mambo ya nje!!!! Je kuna ukweli?

Tiba
Jamaa naona alihajipangia kila mwezi lazima asafiri nje,na hakuna rais duniani ambaye nmeona amesafiri km huyuukizingatia na ni yetu ilivyo masikini,njiuliza sijui wanatumia pesa ngapi iyo entourage yake per trip walipa kodi?
 
CCM ni CHAMA CHA WAISLAMU

Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),

1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu

We jamaa/dada unanikosha, kila thread lazima nilikute hii post yako, kweli umezamiria! Kula like!
 
Hawa jamaa wanaudhi sana kama si kukera, wao kila siku kushadadia CHADEMA wakristo wkt wanajua kbs si ya wakristo....wao wanajisahau safu nzima uongozi mkuu ni waislamu. waache kupotosha wananchi
 
CCM ni CHAMA CHA WAISLAMU

Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),

1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye
serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu

Hizi siku hizi sio 'Nyadhifa Muhimu' ndio maana JK kawateua Wakristo.
1.Uwaziri Mkuu.
2.Uwaziri wa Fedha.
3.Uwaziri wa Mambo ya Ndani.
4.Uwaziri wa Mambo ya Sheria
6. Uwaziri wa Mambo ya Nje.
7.U katibu Mkuu Kiongozi Ikulu.
8.U Anasheria Mkuu.
9. UKUU WA MAJESHI
10. UNADHIMU MKUU WA MAJESHI
11.UWAZIRI WA UTUMISHI WA UMMA.
12.UKUU WA SECREATRIET YA AJIRA
13.UKUU WA TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA.
14. Ukurugenzi Mkuu PPF,LAPF,PSPF
15.U Governor Bank kuu.
Tumeshawazoea Mkiona Umaarufu unashuka kwa Kasi hilo ndo Pori lenu la kusafishia Nyota ya kurejesha Umaarufu.

Mnachokozaga hoja msizoweza kujibu mpaka mnalazimisha Mods kufuta Comments na Ushahidi Mchungu.( Rejea Thread ya Dkt Dau kUPATA ujumbe wa Association ya Pension Funds)
 
Jamaa naona alihajipangia kila mwezi lazima asafiri nje,na hakuna rais duniani ambaye nmeona amesafiri km huyuukizingatia na ni yetu ilivyo masikini,njiuliza sijui wanatumia pesa ngapi iyo entourage yake per trip walipa kodi?
Hivi ule utabiri wa TB Joshua uliishia wapi??
 
CCM ni CHAMA CHA WAISLAMU

Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),

1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu
Tunakoelekea ni kubaya sana kama tukiendekeza mambo haya ya udini.
 
mambo ya CDM yamretufanya tusijadili masuala ya msingi ya Taifa.

soma hapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wiki hii atahudhuria mikutano miwili mikubwa ya kimataifa ukiwamo wa kujadili amani na usalama Barani Afrika kwa mwaliko wa Rais Francois Hollande wa Ufaransa.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumatano, Desemba 4, 2013, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika ambao watahudhuria Mkutano Kati ya Marais wa Afrika na Ufaransa, ambao utafanyika kwa siku mbili katika Kasri ya Elysee mjini Paris kuanzia keshokutwa Ijumaa, Desemba 6, 2013.

Mkutano huo uliopewa jina la Elysee Summit utakuwa ni mkutano wa 26 wa Mikutano ya Wakuu wa Nchi za Afrika na Ufaransa ambao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1973 kwa madhumuni ya kuzikutanisha Ufaransa na makoloni yake ya zamani katika Afrika.

Kwa mikutano miwili ya kwanza, washiriki walikuwa ni marais wa nchi za Afrika zilizokuwa makoloni ya Ufaransa lakini mwaka 1976 zilialikwa nchi zinazozungumza lugha ya Kireno katika Afrika kama watazamaji tu.

Mwaka 1981 jina na madhumuni ya mkutano huo yalibadilika na ukaanza kuitwa The Conference of Heads of States and Government of Africa and France na mwaka 1996 mkutano huo ulifunguliwa kwa nchi zote za Afrika bila kujali zinazungumza lugha gani. Awali mkutano huo ulikuwa unafanyika kila baada ya miaka miwili, sasa ni kila baada ya miaka mitatu.

Kama ilivyokuwa mkutano uliopita uliofanyika mwaka 2010 mjini Nice, Ufaransa, mada kuu ya Mkutano huo ni kujadili amani na usalama katika Bara la Afrika vikiwemo vita ndani ya nchi mbalimbali, uharamia kwenye bahari, biashara ya dawa za kulevya, ugaidi na ujambazi wa vikundi na jinsi mambo hayo yanavyoathiri Afrika na Ufaransa.

Aidha, Mkutano huo utajadili mada nyingine mbili ambazo ni Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Rais Kikwete na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Hollande watakuwa Wenyeviti-Wenza wa kikao kitakachojadili madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi. Rais Kikwete atakuwa Mwenyekiti-Mwenza wa kikao hicho katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU)Juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).

Back
Top Bottom