JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,011
6,261
Wednesday, 05 October 2011 19:52
Venance George, Kidatu
RAIS Jakaya Kikwete ametaka marekebisho yanayofanywa katika Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma, yatumike pia kuwabana matajiri wasio watumishi wa umma ili kujua kama mali walizo nazo wamezipata kihalali au la.
Akizungumza katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya upelelezi na uchunguzi kwa maofisa 50 wa sekretarieti hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Maofisa wa Polisi Kidatu, Morogoro jana alisema hatua hiyo itawezesha watu binafsi kuchunguzwa.
Aliitaka Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuingiza kipengele kitakachoipa nguvu kuchunguza mali za watu binafsi wakiwamo wafanyabiashara katika sheria inayofanyiwa mapitio.
Alisema sheria ya sasa inawabana watendaji wa umma pekee, huku watu binafsi waliojilimbikizia mali wakibaki huru.
"Wako watu binafsi waliojilimbikizia mali pengine wamezipata kwa kuuza dawa za kulevya au njia nyingine zisizo halali, watu hawa pia wafikie mahali pa kuchunguzwa ili waeleze walikozipata mali hizo," alisema Kikwete.
Alisema wakati wa uhuru kipindi cha utawala wa chama kimoja cha siasa, maadili yaliwakataza watumishi wa umma kumiliki mali, kutumia madaraka vibaya, kujipatia mali na kupata mali kwa njia ya rushwa, lakini akasema kubadilika kwa mfumo wa siasa kutoka katika Azimio la Arusha na sasa mfumo wa soko huru kumetoa ruhusa kwa watu kumiliki mali.
"Hivyo kupitia mfumo huo, watu wote wakiwamo watumishi wa umma wameweza kumiliki mali, lakini tunachosema si kumiliki mali, hoja ni umezipataje mali hizo?"
Rais Kikwete alisema kazi ya Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma ni kuwachunguza watumishi wote wa umma kwa kuwataka kujaza fomu za kutaja mali zao na jinsi walivyozipata na kusisitiza kuwa sekretarieti hiyo imeamuriwa kuanza kufuatilia ukweli wa kilichojazwa katika fomu hizo.
Rais alisema bado kuna watumishi wadanganyifu ambao hawatoi taarifa sahihi hivyo ni lazima kufuatiliwa.
Alisema japokuwa urejeshaji wa fomu za matamko ya watumishi wa umma umeonyesha kuongezeka kutoka watumishi 6,007 sawa na asilimia 76.8 hadi kufikia watumishi 8,465 sawa na asilimia 94 lakini kiwango hicho hakitoshi inapaswa kufikia asilimia 100.
Ili kufikia lengo hilo, Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma imetakiwa kuwashirikisha wananchi katika kutambua mali za viongozi na jinsi walivyozipata.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Baraza la Maadili ya Umma, Jaji mstaafu Damian Lubuva alimwomba Rais Kikwete kuwa mkali na kuwachukulia hatua watumishi wa umma wanaobainika kuvunja maadili ili kujenga imani na baraza hilo kwa wananchi.
Mwaka jana, Baraza hilo lilipokea malalamiko 41 na kati ya hayo, 24 yalibainika kuwa ya ukweli na wahusika walichukuliwa hatua za kinidhamu.

Source : JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma

Tumeshuhudia wafanyakazi wa sehemu nyeti nchini, BOT, TRA, THA, TPDC, PPF, WIZARANI hasa za fedha, maliasili, n.k. Hata mamisheni town, kama wakina papa msofe n.k.
Wakijenga majumba ya kutisha na kuendesha magari ya kifahari, wakati mishahara yao au biashara zao ni ndogo. Utajiri wa hawa wafanyakazi na wafanyabiashara haulingani na vipato vyao.

Je JK yuko sawa hawa watu wachunguzwe, ikiwezekana wafilisiwe na kusekwa jela?
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,011
6,261
Sio hao tu, pia kuna wengine humu humu JF ambao wanapenda kuponda watu wanaotaka ushauri wa kuanzisha biashara, hasa kama ni milioni moja, mbili au tau, eti kwa kusema kwa majigambo, hio hela ni ya kunywea bia tu!
Lazima ujiulize kama wanaponda hivi, basi lazima kuna ufisadi wanaoufanya maofisini ya kuwapa kejeli ya namna hio!
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Wameshindwa kuwabana watumishi wa serikali wataweza kwa watu binafsi!!
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Sio hao tu, pia kuna wengine humu humu JF ambao wanapenda kuponda watu wanaotaka ushauri wa kuanzisha biashara, hasa kama ni milioni moja, mbili au tau, eti kwa kusema kwa majigambo, hio hela ni ya kunywea bia tu!
Lazima ujiulize kama wanaponda hivi, basi lazima kuna ufisadi wanaoufanya maofisini ya kuwapa kejeli ya namna hio!

hao wasikuumize kichwa, wengine hawana hata hiyo laki 5 cash, ila wanaponda.
Sio wote wanaoponda wana uwezo kifedha.
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,011
6,261
Haijali watumishi wa serikali wala watu binafsi, wote wale kibano tu!
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,835
25,559
Watumishi wa serikali ambao JK alizikataa kura zao mwaka jana walikisiwa kuwa laki 3 au 4 tu wamewatoa jasho, na mpaka leo wanapeta tu.
Vipi kuhusu sisi wa binafsi na mitaani ambao ki-idadi ni wengi kuliko hao waliowashindwa?
Labda alikua anafurahisha kijiwe tu kwa stori za hapa na pale!!
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,011
6,261
Inawezekana kabisa "Shark", JK alikua anafurahisha kijiwe, ila ni ukweli usiokatalika kuwa wizi na ufisadi umekithiri, watu wanaajiriwa sio zaidi ya miaka mitanoi na kuweza kujenga mijengo ya nguvu zaidi ya 2, na kuendesha magari ya kifahari.
Sasa sie wabongo katika kuwajibika tunasemaje?
Lazima wahusika waulizwe.
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,011
6,261
Nashangaa watu wameitupa hii post, wakati ndio trend iliopo kwa sasa, watu kuwajibika, kuacha rushwa, ufisadi, kuipenda nchi yao, na kusema umaskini basi, hasa unaosababishwa na wizi, ufisadi na kutokuwajibika!
 

kichomi

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
508
54
Jk bana ana bwebwe sana na yeye inabidi abanwe ataje mshahara wake,na kodi anayolipa pamoja na bajeti za safari zake,hapo tutaenda sawa.
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Nashangaa watu wameitupa hii post, wakati ndio trend iliopo kwa sasa, watu kuwajibika, kuacha rushwa, ufisadi, kuipenda nchi yao, na kusema umaskini basi, hasa unaosababishwa na wizi, ufisadi na kutokuwajibika!

hakuna la kujadili.
 

macinkus

JF-Expert Member
Sep 15, 2007
260
19
wameshindwa kuwabana watumishi wa serikali wataweza kwa watu binafsi!!

nadhani rais alikuwa anafurahisha wasikilizaji wake tu. Tangu hiyo tume ipewa madaraka ya kuwashughulikia watumishi wa umma, ni wa ngapi imewatia hatiani mpaka waanze kupanua mabawa yao kushughulikia wananchi wa kawaida?

Macinkus
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,764
4,181
Aanzie ikulu na ajianze yeye mwenyewe, kisha first lady kisha wasaidizi wake: tazama January amekaa miaka 4 tu ikulu na kuendesha X5 hiyo pesa amepata wapi? Au ikulu ni WTC?.
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,611
7,782
Wamekuwa na ufanisi kiasi gani katika hilo jukumu la kuchunguza watumishi wa umma? Kabla ya kuwaongezea majukumu ingekuwa vema kuangalia mafanikio waliyoyapata so far.......maana ufisadi katika sekta za umma bado upo na ni kama vile unaongezeka! Wasiwasi wangu ni kuwa wanatafuta mteremko/au kukwepa jukumu lao la msingi kwa sababu wanahisi pengine ni rahisi zaidi 'kuwashughulikia' watu binafsi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom