JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by taffu69, Oct 6, 2011.

 1. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Venance George, Kidatu
  RAIS Jakaya Kikwete ametaka marekebisho yanayofanywa katika Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma, yatumike pia kuwabana matajiri wasio watumishi wa umma ili kujua kama mali walizo nazo wamezipata kihalali au la.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya upelelezi na uchunguzi kwa maofisa 50 wa sekretarieti hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Maofisa wa Polisi Kidatu, Morogoro jana alisema hatua hiyo itawezesha watu binafsi kuchunguzwa.

  Aliitaka Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuingiza kipengele kitakachoipa nguvu kuchunguza mali za watu binafsi wakiwamo wafanyabiashara katika sheria inayofanyiwa mapitio.

  Alisema sheria ya sasa inawabana watendaji wa umma pekee, huku watu binafsi waliojilimbikizia mali wakibaki huru.

  “Wako watu binafsi waliojilimbikizia mali pengine wamezipata kwa kuuza dawa za kulevya au njia nyingine zisizo halali, watu hawa pia wafikie mahali pa kuchunguzwa ili waeleze walikozipata mali hizo,” alisema Kikwete.

  Alisema wakati wa uhuru kipindi cha utawala wa chama kimoja cha siasa, maadili yaliwakataza watumishi wa umma kumiliki mali, kutumia madaraka vibaya, kujipatia mali na kupata mali kwa njia ya rushwa, lakini akasema kubadilika kwa mfumo wa siasa kutoka katika Azimio la Arusha na sasa mfumo wa soko huru kumetoa ruhusa kwa watu kumiliki mali.

  “Hivyo kupitia mfumo huo, watu wote wakiwamo watumishi wa umma wameweza kumiliki mali, lakini tunachosema si kumiliki mali, hoja ni umezipataje mali hizo?”

  Rais Kikwete alisema kazi ya Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma ni kuwachunguza watumishi wote wa umma kwa kuwataka kujaza fomu za kutaja mali zao na jinsi walivyozipata na kusisitiza kuwa sekretarieti hiyo imeamuriwa kuanza kufuatilia ukweli wa kilichojazwa katika fomu hizo.

  Rais alisema bado kuna watumishi wadanganyifu ambao hawatoi taarifa sahihi hivyo ni lazima kufuatiliwa.

  Alisema japokuwa urejeshaji wa fomu za matamko ya watumishi wa umma umeonyesha kuongezeka kutoka watumishi 6,007 sawa na asilimia 76.8 hadi kufikia watumishi 8,465 sawa na asilimia 94 lakini kiwango hicho hakitoshi inapaswa kufikia asilimia 100.

  Ili kufikia lengo hilo, Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma imetakiwa kuwashirikisha wananchi katika kutambua mali za viongozi na jinsi walivyozipata.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti Baraza la Maadili ya Umma, Jaji mstaafu Damian Lubuva alimwomba Rais Kikwete kuwa mkali na kuwachukulia hatua watumishi wa umma wanaobainika kuvunja maadili ili kujenga imani na baraza hilo kwa wananchi.

  Mwaka jana, Baraza hilo lilipokea malalamiko 41 na kati ya hayo, 24 yalibainika kuwa ya ukweli na wahusika walichukuliwa hatua za kinidhamu.
  **********************************************************

  Napata taabu sana kuelewa JK anamaanisha kwani sidhani kama Sekretariati yenyewe imeweza kutekeleza majukumu ya msingi iliyotakiwa kufanya. Mpaka sasa tumeona viongozi wa juu Serikalini wakishindwa ama kukataa kutaja japo mali wanazomiliki lkn hawachukuliwi hatua yoyote!!

  Chanzo cha habari: JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280

  Hao wakubwa walioundiwa chombo hawajawahi kuchunguzwa na kama walichunguzwa ni fake uchunguzi sasa mnaingiza wadogo ili muwaonee. Shame!!!!!!!!
   
 3. SoNotorious

  SoNotorious JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 2,426
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  huwa nahisi jk hana ubongo.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  anouther corruption avenue... paved and street lights in place!!! hao wachunguzaji ndio wanaotutesa huku mitaani
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na ww nahisi ni mchicha mwiba !
   
 6. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ukituchokonoa tutakuchokoa
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wakishajulikana ni wezi nini kitafwata?????????kama sio upuuzi mwingine wa jk
   
 8. u

  utantambua JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa wachunguzwe kwa sheria ipi wakati sheria imeainisha ni watu wa kada flani (viongozi) tume iwachunguze. Jamani mimi nachoka kabisa
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well, aanze na ridhwani
   
 10. kanywaino

  kanywaino Senior Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hiyo tume yenyewe imeundwa na mafisadi asa kesi ya ngedere unampelekea nyani ha ha ha ha wangewka projector tukaona wanafanyiwa interview kama wenzetu juz..ili tujue uwezo wa watendaji wa tume ya maadili,isiwe tume ni ya kurutubisha wizi wa mali za umma
   
 11. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Jk ni mtu wa ajabu kweli, du! Hivi huyu jamaa hana washauri? Ina maana hiyo secretariate imefanya kazi nzur sana mpaka ionekane iongezewe tena majukumu mengine. Hii secretariate ni kati ya taasisi za serikali zinazolipwa hela za walipa kodi bure bila kuwepo kitu cha maana wanachokifanya. Hivi tutaacha lini huu ujinga wa kuwa utitiri wa regulatory authorities which are useless such this, PCCB, EWURA, SUMMATRA, TFDA, TBS, DPP, TISS etc. Naomba wale wanazi wa JK na CCM watuambie hiyo secretariate imefanya nini cha maana tangia iundwe, ni viongozi wangapi wamekamatwa wameikuka maadili na kufikishwa mahakamani? Kila siku tunaona jinsi maadili ya viongozi wetu yanavyoporomoka wakime marais Jk na mwanaye, Mkapa, mawaziri, katibu wakuu, wabunge, wakurugenzi nk, lakini hatujawahi kuambiwa wamekamatwa. Nimesikitishwa sana na hii hotuba ya jk. Bora angesema hii secretatriate naivunja na kuwaachisha kazi watendaji woote since they are not productive, and are eating taxpayers money innappropriately. I am tire of illusions!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  God bless this land
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  sioni jipya hapo......................sheria za ufisadi zipo wazi kabisa hazihitaji kuongezewa nakshi..........................mtoa na mpokea rushwa njia yao huwa moya.............................wote ni watuhumiwa wa uhalifu........................awe serikalini au nje ya serikali anapaswa kuchunguzwa............sidhani kurekebisha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inahitaji marekebisho yoyote ya kuwajumusiha watu wasio ndani ya ajira serikalini.................hizo ni kazi zina taasisi zake yaani Takukuru....................But I have always find JK's lack of brain power truly astonishing.........................
   
 13. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Utakataje matawi ya mti bila kuukata mzizi Kama nia ya kweli ni kuuteketeza!!?.Hawa viongozi walipo Serikali ni wangapi wameshashughulikiwa!?Adhabu zenyewe jela miaka2 wakati mtu kaiba mabilioni ya walipakodi!!huu ni unafiki wa waziwazi anaouonyesha raisi Jakaya kikwete dhidi ya raia wake na hapa nikisema JK anajuana na hao wezi(wahujumu uchumi)nntakuwa nnakosea!???
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  JK huwa hafikirii nini cha kuongea anapokuwa kwenye hadhira! Chochote kinachomjia kichwani huwa anakiongea bila kufanya tathmini ya faida ama madhara ya anachoongea. Nakumbuka issue ya Maaskofu na biashara ya madawa ya kulevya ilivyomletea tafrani mpaka Ikulu ikawa inatoa maelezo yasiyo na kichwa wala miguu.

  Kama ni washauri wake wanaomshauri hivyo ni bora awatimue wote abaki na waliomsaidia kupiga kampeni mwaka 2010.
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  TAKUKURU, DPP, TISS, na POLISI wana kazi gani mpaka kuwaongezea majukumu hiyo tume ambayo haijaweza kuchukulia kiongozi yoyote (tangu kuundwa kwake) hatua juu ya wizi au viongozi wetu wote ni safi? Ataleta mgongano wa kiutendaji tu kuna idara ambazo zinawajibika kufanya hayo ila hazifanyi suala ni kufukuza wote wanaopaswa kufanya hayo na hawafanyi
   
 16. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Aanze yeye kwanza kutoa uthibitisho wa nyumba ya Ursino Estate aliijenga kwa hela za namna gani halafu mengineyo yafuate halafu aseme mtumishi wa umma anayesomesha watoto Kamuzu Academy, Malawi anapata wapi hela hizo badala ya kuwasomesha shule za kata.
   
 17. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimecheka mpaka bac!
  Ina mana baba alipokuwa anatangaza hakujua mwanaye anaweza kuwemo?
   
 18. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hvi VIJISENTI aliishia wapi vile?
   
 19. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,803
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Grand corruption and big bussiness more often than not are two sides of same coin ,Bussiness becomes a conduit to luander the spoils of high corruption. The question is do we have institutional capacity and will to fight corruption ? Answer is definate NO.
   
 20. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  yeye anachunguzwa na nani?.....na suti zake za dubai
   
Loading...