JK: Watanzania nunueni Matrekta badala ya anasa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Watanzania nunueni Matrekta badala ya anasa!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Akili Unazo!, Aug 4, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,818
  Likes Received: 2,530
  Trophy Points: 280
  Wakuu ebu angalieni hii kauli iliyotolewa na kiongozi wetu mwenye dhamana ya hali ya juu.

  JK ametaja anasa za watanzania kuwa m,oja ya mambo yanafanya sekta ya kilimo kushindwa kufika malengo ya kuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania.
  Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya nanenane katika viwanja vya Nzuguni njee kidogo ya mji wa Dodoma jana,JK alisema baadhi ya watanzania wanapenda kunua magari ya kifahari badala ya matrekta kwa ajili ya kilimo!!

  Kwa kifupi ni hayo.lakini jambo la kujiuliza hivo ni kwa nini anweza kuongea hivyo wakati hata kwenye bajeti kilimoa imepewa kiasi kido kuliko wizara nyingine?
  Kama hilo analijua kwa nini asifanye kama mwenzake kibaki alichofanya kurudisha magari yote ya kifahari ya serikali ili kuinua kilimo nchini?

  Katika kiongozi ambaye amewahi kuongoza hii nchi yeye anaongoza kwa matmizi mabaya ya mapato yapatikayo kwa kuwa na ziara sizizokuwa na msingi hivi anashindwa kuelewa kuwa kilimo kiimerudi nyuma kwa sababu ya viongozi wabovu aliowateua na kuwapa madaraka ya kuongoza wakati hawezi?

  KWELI HII KAULI ILITAKIWA KUTOLEWA NA YEYE AU AMETOMBOKA?
   
 2. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chaku!

  Achana na huyo Mkwere msanii tupu. Alitakiwa kwanza auze ile fleet ya magari yasiyopungua 1000 yaliyoko ofisi ya Rais ili akanunue matrekta na pia kupunguzo utegemezi wa mafuta ya diseli/petroli kama kianzio kikuu cha mapato ya serikali yake ya kifahari ili aiunue kilimo.

  Kama wakulima wadogo hawaruhusiwi kuuza chakula nje ya nchi huku wakulima wa maharagwe na maua wakiruhusiwa kuuza nje hicho kilimo kitakuwa kwa changamoto zipi?

  Pale nanenae aliwenda kwa ajili ya show biz tu na hayuko serious hata kidogo.

  Aache kuendekeza safari za kila siku za kwenda kutembea na pesa atayookoa azitumbukize kwenye kilimo!!

  This is just the same old song!!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani kati ya 'watanzania' na serikali yao ni nani anaongoza kwa anasa?
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani nimesikia hasira ghafla basi tu!
  Eti waache magari ya kifahari? hivi kwanini watu hupenda kusema yale ambayo hawawezi kuyatenda wao? Mbona asianze yeye kuachia hayo magari aliyo jirundikia magogoni anayabadilisha utadhani pea za kanga? Wakati mwingine ni afadhali kunyamaza kuliko kusema kile ambacho unataka wakifanye wenzio wakati kwako ni chukizo!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ama kwa hakika prezidaa tunaye..lol
   
 6. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapana Chaku hapa hujaweka sawa sio anasa msipindishe maneno. Alichoongea mm nilikuwepo Dodoma kasema "watanzania tununue Matrekta badala ya magari ya anasa maana utakuwa mtu ana magari kama 5 yote ya kifahari........"

  Please tuweke maneno ya ukweli na sio tupindishe pindishe hii sio asili ya JF.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Serikali inaongoza kwa anasa piga hesabu wa yale mashangingi,VX n.k alafu wananchi wanakumbukwa kwa Ambulance 50 tu nchi nzima.
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,818
  Likes Received: 2,530
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu naomba soma gazeti la mwananchi ukurasa wa tatu halafu sema huo ulinganifu.Kama aliyekusea ni huyu/hawa ( Hebel Chidawali,Patricia Kimelemeta na Hussein Kauli) waandishi mimi nawapigia simu waniagizie video ya maneno ya huyu JK.Kweli hawa wote watatu wamekosea kunukuu kauli za huyu ndugu?

  Kikubwa hapa tuangalie tuache kuanza kukosoa ila tuseme ukweli nani anatakiwa kukipa kipaumbele kilimo?Selikari au mwananchi?angalia msistizo mzima hata kwenye bajeti iliyopita umepelekwa wapi?si kwenye kilimo lakini ni moja ya sekta ambayo i na kiasi kidogo cha bajeti kuliko hata secta zingine.

  pale ikulu kuna magari mangapi ya kifahari?
  Anatumia kiasi gani cha fedha ambacho kama angekiweka kwenye kilimo tungekuwa nyuma kiasi hicho?
  Angalia maonyesho yote ya nanenane yanayoendelea nchi nzima kuna show to za promotion za soda na pepsi njoo morogoro ambako ndo moja ya mikoa iliyotengwa kuwa ghala ya kilimo ujionee yanayopewa hamasa.

  Nenda arusha kumeja wamachinga wa kihindi na maua yao?
   
 9. S

  Sendeu Member

  #9
  Aug 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli nchi imeshauzwa wadau yaani RAIS anasema mambo haya aibu tupu huku SPIKA wa bunge akiishi kwenye nyumba ya USD 8000 kwa mwezi,huku mafisadi wanachota pesa za kutosha kwenye tenda mbalimbali za serikali jamani muandalieni Rais hotuba nzuri kwa watz kwani wengi wamechoka na blahblah ipo siku nchi itaingia kwenye vurugu ndugu zanguni!!!!!!!!...............
   
 10. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #10
  Aug 4, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  RAIS tumeshamzoea huyu..anachemka kila siku..im not surprised..endeleeni kumuombea ndugu wana maombi.pepo wa rushwa na uzinzi na uasherati na ufisadi ndiyo umewagubika viongozi wengi wa ccm..hawawezi kutuhurumia sie wananchi kwa sasa..mpaka pepo watolewe..endeleeni kuomba.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hili waswahili wanaliweka katika lile kundi linaloitwa "Nyani haoni kundule"
   
 12. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lawama zote nazipeleka kwa sisi wananchi na sio serikali ukitaka kujua sababu zipo nyingi.
   
 13. m

  muhanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  wakati mwingine mtu ninaedhani ameenda shule akiongea/ akifikiri pumba za ajabu ajabu huwa ananichanganya sana, huyu JK ana wazimu haswaa! nafananisha kauli yake na ile ambapo mtu anaona kuliko anunue kilo ya nyama bora anunue mchicha mafungu 100! lakini ukweli utabaki pale pale kuwa atakuwa kanunua mchicha na si nyama aliyodhamiria. kumshawishi mfanyakazi kwa mfano wa benki eti aache kununua ka-spacio kake akanunue trekta!!! wajati yeye anahitaji zaidi usafiri wa kumpeleka ofisini na hana hata shamba la nusu eka wewe umshauri eti anunue trekta halafu akalime kwenye lami?????? serikali iwasaidie wale watumiaji wa tractors (wakulima) kuinua kipato chao, kwa mkulima akipata pesa ya kutosha lazima atafikiria kuboresha kazi yake kwa kujipatia tractor ambayo itamsaidia kilimo, na si kumbadili mawazo mfanyakabiashara wa nguo kariakoo akaache kununua range rover eti anunue trekta!!! atalipitisha wapi mjini???? hayo ni mawazo ya mwenda wazimu tu siasa na uhalisia wa mambo havitangamani abadan
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nimeshangaa sana. Mkulima gani anaweza kuwa na gari (hata kama ni Starlet) achana na hayo yao ya anasa. Kwa kweli hayo ni matusi na dhahaka kwa ndugu zetu wanaotaabika kurushana na jembe la mkono. Halafu sijawahi kuona rais weak kama JK. Badala ya kutoa amri kuwa kuanzia leo ni mwisho wa mashangingi anaishia kucheka cheka na kukera watu! Kama kuna mtu anafuja pesa za nchi hii ni viogozi wa serikali yake ya kishikaji wakianzia na yeye mwenyewe! Labda huko Bagamoyo wakulima wanatesa na Benz, VX, BMW n.k.
   
 15. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Pia waswahili huwa wanasema, "Huyo ni Domo Kaya tu"
   
 16. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mimi nilitegemea mheshimiwa angesema kwa kuanza kampeni hii ya "Kilimo Kwanza" hela yote iliyotengwa kwa "Chai na Vitafunwa, Tshs19 billion" itanunua matrekta mwaka huu na viongozi wote katika wizara na idara za serikali "Wajinunulie Chai na Vitafunwa" kutoka mifukoni mwao.

  What a waste!
   
Loading...