JK: Waliofaulu na kutokwenda sekondari wote wasakwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Waliofaulu na kutokwenda sekondari wote wasakwe

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, May 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Pia aagiza wazazi wao wanaowazuia wahojiwe
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete  Rais Jakaya Kikwete, amewaagiza wakuu wa wilaya zote nchini kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini watoto waliofaulu kuingia sekondari mwaka huu lakini wameshindwa kuanza masomo mpaka sasa.
  Aidha, ameagiza kuwa katika zoezi hilo, wazazi wote ambao wanawazuia watoto wao kuanza masomo ya sekondari kwa sababu yoyote ile, wahojiwe kwa nia ya kuhakikisha kwamba wanawapeleka watoto wao haraka.
  Rais Kikwete alitoa maagizo hayo juzi mjini Masasi wakati akipatiwa maelezo ya maendeleo ya Mkoa wa Mtwara baada ya kuelezwa kuwa asilimia 35.6 ya watoto wote 12,843 waliochaguliwa kuingia sekondari mkoani humo, hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
  Rais aliambiwa kuwa ni asilimia 64 tu sawa na watoto 8,278, ndiyo walioripoti na kuanza masomo ya sekondari wakati watoto 4,565 hawajaripoti shuleni na hawajulikani waliko.
  Katika idadi hiyo, Wilaya ya Mtwara ndiyo inayoongoza kwa asilimia 54, ikifuatiwa na Nanyumbu asilimia 48, Masasi asilimia 35, Tandahimba asilimia 32, Mikindani asilimia 22 na Newala asilimia 21.
  Rais Kikwete aliambiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali (mstaafu) Anatory Tarimo, kuwa baadhi ya sababu zilizowazuia watoto hao kuripoti shuleni ni pamoja na baadhi yao kupata mimba, kuozwa ama kuzuiwa na wazazi wao kwenda shule.
  Baada ya kupewa takwimu hizo, Rais Kikwete aliagiza: “Hizi takwimu ni za juu sana. Haiwezekani tukaendelea kuwadhulumu watoto wetu maisha bora kwa kuwazuia kwenda shule wakati shule zipo, nafasi zipo na kila kitu kipo.”
  Aliongeza: “Tafuteni majina ya watoto hawa wote, wazazi wao waitwe, wajieleze na kama hawana majibu, wawajibishwe. Afuatwe mtoto mmoja baada ya mwingine bila kumwacha yeyote. Na njia rahisi ufanywe msako wa nyumba kwa nyumba, kama ilivyokuwa zamani wakati wa kukusanya kodi.
  Alisema wazazi wa watoto hao wahojiwe siyo kwa nia ya kutaka kujua sababu gani zinazuia kuwapeleka watoto shule, bali kwa nia ya kuhakikisha kuwa watoto wanapelekwa shuleni mara moja na kwamba kazi hiyo ifanyike katika kila wilaya nchini na isimamiwe na mkuu wa wilaya katika kila wilaya ambako yapo matatizo ya namna hiyo.
  Rais Kikwete alipewa ripoti hiyo ya maendeleo ya Mkoa wa Mtwara, ikiwa sehemu ya shughuli zake wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo ambako miongoni mwa mambo mengine, juzi alishirikiana na Rais wa Msumbiji, Emilio Armando Guebuza, kufungua rasmi daraja jipya linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwenye Mto Ruvuma.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...