JK: Wafanyabiashara chanzo cha ufisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Tumechoka na hotuba za ufisadi, sasa ni wakati wa kuwashughulikia mafisadi wa EPA, Richmond, Kiwira n.k. Pia kwa taarifa yako wanasiasa ndiyo chanzo cha ufisadi. Porojo sasa basi!!!!

Date::7/14/2008
JK: Wafanyabiashara chanzo cha ufisadi
Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, amepasua ukweli mbele ya wenye viwanda, akisema kuwa, rushwa kubwa nchini zina mkono wa baadhi ya wafanyabiashara.

Kutokana na hali hiyo, Rais alilitaka Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), kushirikiana na serikali kupambana na rushwa nchini.

Akizungumza juzi usiku wakati wa utoaji wa Tuzo bora ya Rais kwa Wazalishaji Bora, Rais Kikwete alisema, hakuna biashara inayoweza kudumu katika mazingira ya rushwa na ukiukaji wa sheria.

Rais Kikwete ambaye alizungumza mbele ya wenye viwanda akiwemo Mwenyekiti wa CTI, Reginald Mengi, alisema, wakati mwingine katika kutafuta upendeleo wa ushindani ni wafanyabiashara ndio wanaochochea rushwa.

Alisema, kama wafanyabiashara wataamua kuacha kupenda upendeleo na upindishaji sheria, basi rushwa kubwa zitakoma.

"Lakini, pia na wenyewe mjitazame katika shughuli zenu. Na nyie mnalalamikiwa kwa rushwa katika ajira na kupata shughuli ya kufanya kama vile kupata uwakala, wahusika kuomba na kupokea rushwa," alisema Rais Kikwete.

Rais alisema: "Kama mwombaji ni msichana, basi huombwa penzi ndipo apate kazi au shughuli."

Alisema, imezoeleka kusemwa kwamba, rushwa ni adui wa haki; na akasisitiza kuwa sheria za nchi ziheshimiwe katika mienendo ya biashara na wafanyabiashara.

Alisema kuwa, serikali inatambua na kuridhishwa na mchango mkubwa wa sekta binafsi na umuhimu wa sekta ya viwanda katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa.

Alisema, serikali inajivunia uamuzi wake wa kuifanya sekta binafsi kuwa injini ya ukuaji uchumi, kwani imeonyesha mafanikio ambayo ni kufanya ukuaji wa haraka wa Pato la Taifa kwa wastani wa asilimia sita kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Rais aliongeza kuwa, mchango wa sekta ya viwanda katika pato hilo umeongezeka kutoka asilimia 17.2 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 18.4 mwaka 2007, lakini akasema bado haridhishwi na mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

"Vile vile, pamoja na kwamba mchango wa Pato la Taifa umeongezeka katika mauzo ya nje kutoka asilimia 5.3 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 8.3 mwaka 2007, mchango huo ni mdogo mno ukilinganisha na uwezo wa sekta hii," alisema Rais Kikwete.

Rais alisema kuwa ni vema pia watu wakachangamkia soko katika Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuongeza: "Leo mkulima wa machungwa kule Muheza, anaweza kupakia machungwa yake katika Fuso na kupeleka Mombasa tu, tofauti na kwamba apeleke Marekani itakuwa ni matatizo, mambo ya kupakia. Sisi tumefungua mipaka, fanyeni biashara."

Rais alikabidhi tuzo mbalimbali kwa viwanda katika sekta tofauti huku Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiibuka mshindi wa jumla.
 
Huyu Rais kweli HAMNAZO!
Si niliwaambia jana kwa hata kuhamishiwa madeni kwa DOWANS NA RICHOMD ALIKOFANYA ROSTAM AZIZ NA KUYAHAMISHIA KWA MANJI..Ni plan ambayo JK amepewa na ROSTAMA ya kuanza kudai kuwa UFISADI NI VITA DHIDI YA WAFANYA BIASHARA?
Naona kageuza hii hotuba kidogo labda alikuwa hapa jf akona mjadala kuwa tuko one step ahead na sasa kageuza na kudai eti hata uko viwandani watu wanadaiwa rushwa ya mapenzi!
Unajuwa mi naona kuwa kuna uwezekano mkubwa wa machafuko.
Sasa nimeamini!
Halafu Rais mzima anaona mali zetu zimeuzwa na yeye anjizungusha na kuwambia watu wapakie FUSO LA MACHUNGWA WAPELEKE MOMBASA...MOMBASA KUNA NINI?
AMA NI DOGO DOGO?
Mi nakwambia Rais hatuna na pale ni kanyaboya tu!
Rais MKAPA NA MAKAMU NI ROSTAM...Mwanansheria mkuu bado ni CHENGE NA SPIKA HAKOHOI!
Mi nakwambi watu watalimana risasi!
Sidhani kama ni kila mtu atakubali huu UPUUZI uliovuka mipaka!
 
I am too ashamed to have him as the President of the country I call Mother-Country coz he is an embarrasment.
 
yaani tatizo la rushwa ni kwa sababu wafanyabiashara wanapenda rushwa?

...anachosema JK kina ukweli ila sio kweli wanapenda rushwa ila system inawafanya hivyo,lakini sio excuse hiyo maana mtoa rushwa na mpokea wote sawa,waache kutoa tuu itaisha/itapungua.
 
JK, everyone knows U r MSANII SR. Fanya kazi acha hadithi. Unajua unaipeleka hii nchi pabaya kwa kuachia FISADIZ kufanya watakavyo. Sasa wanaanza kuchanganya wananchi na hata huko makanisani. Unajifanya una NTA masikioni lakini pale wananchi watapoamua kuchukuwa sheria mikononi mwao dhidi ya FISADIZ ndipo utang'amua kuwa wananchi wamechoshwa na style yako ya uongozi. Wee na SIRIKALI yako mtaanza kuadhibishwa si muda mrefu. Endelea kufumbia macho hayo huku ripoti zote ukiwa nazo. Uraisi si kusafirisafiri tu, shughulikia na matatizo ya nyumbani. Shughulikia FISADIZ.
 
Mhishimiwa,
Kama wala rushwa wakubwa hawashitakiwi unafikiri wataacha tu kwa mapenzi yao?

Ukitaka kupambana na rushwa anzia juu kwa viongozi na wanasiasa kwanza badala ya kuleta porojo za kila siku.
 
Back
Top Bottom