JK vs CDM ni sawa na disco la urafiki wa mashaka, swara anacheza na chui, simba anacheza na mbuzi wa

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417

Mazungumzo ya mahasimu wawili kisiasa nchi, jana yalisitishwa ili JK na wapambe wake wakayatafakari mapendekezo ya CDM kabla ya kuyatolea maamuzi.
Naona kama marafiki hawa wanacheka pamoja machoni lakini mioyoni mwao kila mmoja anadukukudu.
Hata vicheko na tabasamu zao zilionyesha kuwa kama watu ambao kila mmoja alikuwa akijaribu kuwa makini na kujenga hofu na mashaka kwa mwenzake.
Ilikuwa ni sawa na urafiki wa mashaka wa swala kucheza disco na chui huku simba akiselebuka na mbuzi wakati fisi akiendelea kuchoma mishikaki jikoni. Acha tusubiri tuone mwisho wako
 
Back
Top Bottom