JK unaipeleka wapi Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK unaipeleka wapi Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Jan 9, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Oktoba 31 2010 ulichaguliwa kuwa rais wa Tanzania. Tunajua uliupata kwa njia ya uchakachuaji. Hata hivyo tumekubali yaishe kwa sababu katiba yetu ndiyo iliyokubeba. Tumeamua tukuache uendelee na urais wakati sisi tunahangaika na katiba yetu.

  Ulipogundua kuwa Watanzania tumegundua mbaya wetu kuwa ni katiba na tumeamua tufanye mabadiliko yake. Umetushangaza tuliposikia kuwa unataka kuunda tume ya kurekebisha/kuratibu mabadiliko ya katiba. Tafadhali katika hilo utuache, tuhajua tunalofanya na wala usituingilie.

  Umechaguliwa kwa uchakachuaji. Leo hii dhambi ya uchakachuaji imeshindwa kuondoka tangu uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 2010 uishe. Tunaona yanayotokea katika chaguzi za mameya na wenyeviti wa Halmashauri za wilaya na miji. Kwanini unaingilia hadi huku? Ulizochakachua hazikutoshi? au unataka kusema kuwa huhusiki? kama huhusiki hao wanaochakachua siyo wateule wako?kazi wanayofanya wanafanya kwa ridhaa ya nani?bila shaka umo katika hilo.

  Sasa hivi bei ya bidhaa inapanda kila kukicha. unataka kutuambia nini? umeme unapanda bei. hata kama ukijitetea kuwa haupandi kwa sababu ya malipo ya Dowans nani atakuamini? umeshindwa kutuambia mmiliki wake na tukisema ni wewe mwenyewe Salva Rweyemamu anakutetea. Umeshindwa kujitetea mwenyewe? sisi wananchi tunafahamu wewe ndiye rais wetu kwa mujibu wa katiba yetu hata kama si kwa mujibu wa mioyo yetu na kura zetu. unafanya nini hapo Ikulu kama humjui mmiliki wa Dowans?

  Tukiandamana kueleza hisia zetu unawatuma Askari wako kutuua. Una maana gani Jk. unacheka wakati Watanzania wanakufa bila hatia. Unasema yaliyotokea Arusha tarehe 05/01/2011 ni kwa bahati mbaya? hakuna bahati mbaya katika maagizo uliyowapa watendaji wako bali umeamua kutuvunjia heshima. Watendaji wako wanadai Chadema wamefanya mkusanyiko haramu. umeshindwa kujua kuwa vyama vya siasa vina uhuru wa kufanya mkutano na wanachotakiwa kufanya ni kutoa tu taarifa polisi? kwa bahati waliomba ruhusa na wakapewa. kwanini uwaue? Watanzania wenzetu wameuawa kwa madai ya kuandamana na kushiriki mkutano uliokuwa haramu eti kwa madai kuwa ni Wanachadema, je huyo Mkenya alikuwa mwanachama wa Chama gani? Hakika nchi imekushinda.

  Tunakusihi JK unakoelekea siyo kwenyewe.JK nchi hii hutaiweza. Katiba imekubeba hubebeki. Umeng'ang'ania tu Ikulu lakini tunaoishi Tanzania hatukutambui kama kiongozi wetu.
   
 2. K

  Kiwete JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Bonge la ujumbe kwa JK.Nashauri ipelekwe kwenye tovuti husika wapambe wamwonyeshe.
   
 3. M

  Mundu JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mtu akishashikwa na mafisadi hata umwandikie nini hawezi kusikia. Mengi ya haya yameshaandikwa,na mengine yamejibiwa na makuwadi wake akina Salva. He is just not himself. Ni Lowassa na Rostam ndio wanampa directives.
   
Loading...