Jk-tulipuuza uamuzi wa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk-tulipuuza uamuzi wa watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mvaa Tai, Sep 30, 2010.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nimesikitiswa sana na matamshi aliyoyatoa JK pale bukombe kuhusiana na vyama vingi nchini Tanzania.

  Ninavyfahamu mimi Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992.

  JK anasema Watanzania hawahitaji mfumo wa vyama vingi na ndiyo maana katika kura za maoni zaidi ya 80% waliukataa mfumo huu. Lakini kutokana na hekima na Busara za CCM walilazimisha kuwepo na huu mfumo bila kuzingatia kura za maoni zinataka nini, anaendelea kusema waliamua hivyo kwasababu waliona ni vizuri kuwe na hii 20% ya wanaopinga chama kimoja kwasababu wanaweza kuleta chachu kidogo kuiwezesha CCM kutawala vizuri, anaongeza kujigamba kwamba hata ushindi wa CCM uliopita wa zaidi ya 80% unatokana na sababu hii. Anawaambia wananchi wasibabaishwe na vyama vya upinzani maana ni vya kupita tuu.

  Kwa uwezo wangu huu mdogo wa darasa la tano nimefikiria yafuatayo:-


  1. JK- Anakiri hadharani kwamba CCM ina dharau maoni ya Watanzania, kwasababu watanzania hawakutaka vyama vingi wao kama chama na Serikali walilazimisha nini kifanyike. Hivyo tuchunge sana uchaguzi huu yaweza kujitokeza haya.
  2. JK- Anakiri hadharani kwamba Serikali iliyopo madarakani ilianza siku nyingi sana kutumia vibaya rasirimali za walipa kodi, kwa mfano;- kutumia mamilioni ya pesa za wananchi kuendesha shughuli za kura za maoni ilihali wanafahamu maoni yatakayopatikana hayatafanyiwa kazi.
  3. JK-Anaonyesha hadharani uwezo wake wa kufanya scientifical analysis, anadai ushindi wake wa zaidi ya 80% katika uchaguzi uliopita unauhusiano na zile kula za maoni zilizoukataa uwepo wa vyama vingi kwa 80%, najaribu kujiuliza ule ushindi wa Mkapa ambao ulikuwa wa chini ya 80% ulimaanisha nini? Kama siyo kumtusi mtangulizi wake ni nini?
  4. JK- anaonyesha hadharani kwamba haamini katika mabadiriko, kwani anaamini ule uhusiano wa 80% na 20% wa waliokataa vyama vingi na waliokubali(respectively) ndiyo uliopo leo hii. Bila kujua kwamba watu wanabadirika hawezi akafikiria miaka 20% iliyopita nchi ilikuwa na wasomi wangapi na watu wenye ufahamu wa dhati kuhusiana na vyama vingi walikuwa wangapi?
  5. JK- Anajaribu kudhurumu haki yetu ya msingi ya kusikiliza utekelezaji wa ahadi zake za uchaguzi uliopita na ahadi zake mpya, kwa kutuwekea mazingira ya kusiliza historia ya vyama vingi na kebehi dhidi ya vyama vya upinzani.

  JK- Anazidi kunifanya nizidi kuheshimu maamuzi niliyoyachukua dhidi yake hiyo october 31
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  "Siku zote huwa kuna asilimia 15 ya watu ambao watakupinga, asilimia 15 ambao watakuunga mkono na asilimia 70 ambao wanafuata upepo" J. K.
   
Loading...