JK tulia kidogo nchini: Meli inapigwa mawimbi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK tulia kidogo nchini: Meli inapigwa mawimbi!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Jul 23, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu wangu JK, Meli yako inayoitwa Tanzania inaelekea iko kwenye mawimbi ya kati hadi mazito kidogo.
  Kwa sisiwadau wako tunaona ni kwa sababu nahodha uliyemuachia usukani ukiwa katika ziara zako nyingi nje ya nchi naye anayumba na Meli hiyo.
  Yanayoniskitisha zaidi ni Serikali kukosa muelekeo hasa wakati huu wa Bunge.
  Rushwa ya David Jairo imetushitua sana na imebidi ikusubiri kimaamuzi.

  Kushitakiwa Chenge imekuwa wimbo wa itakuwa au haitakuwa, Serikali haina maamuzi ya kujionyesha iko safi.
  Kwenye chama nako mambo si shwari, Sitta na Guninita wanaparurana hadharani.

  Mzee mzima Rostama kaachia ngazi, hakuna wa kucomment rasmi juu ya kuvua gamba

  Sie tuna uhakika Meli haizami, lakini dhoruba wananchi wanayoipata inawatia wasiwasi juu ya umahiri wa Nahodha.
  Naomba tulia kidogo nchini mawimbi yaweze kutulizwa Mkuu wangu
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda , kuelewa hayo uliyoainisha inataka Hikma, kitu ambacho kwa huyo ****** 'Meti-Onyo', yaani hamna kitu!
  Anaongea BBC kuwa shida ya umeme Tz inaletwa na ukame, wakati anajua wazi watu wanahongana billions ili kuliua Taifa kupitia bajeti ya Wizara ya Nishati!
  Anachekelea hata hayo, anashindwa kuamua, wakati anayo full-support ya Bunge lote na Wananchi wote!
  My Hairs!
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hata akikaa nchini hana jipya. Akae huko huko ili tuparuane vizuri. Kama ni mtu wa maamuzi angeshamtimua Jairo kabla ya giza kuzama siku ile na hayo aliyoyaamua ndio angeamua hata akiwa hapa! Natamani yamkute huko wala asirudi tena!
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Nchi haina utamaduni wa maamuzi magumu, hata Lowassa alisema
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  anawashwa yule miguuni soon utasikia hayupo
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hili la kuhonga wabunge wanaotuwakilisha ni fedhea kubwa sana.
  Unanyamazisha wananchi kwa kuwapa sukari inayoozesha meno yao!
   
 7. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wale jamaa zangu wa magwanda kuandamana sijui wako wapi?
  Au nao wameshanojeshwa lawalawa!
  Sisi hapa miguu inawasha , hatujatembea siku nyingi.
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kuto tulia kwake nchini kuna nipa shaka kubwa kuwa anatafuta nchi ya kukimbilia maana mwenzaka Mutharika yameisha mkuta na sasa zamu yake. Cameron alirudi England after Phone Hacking ziara zote akatupa kapuni yeye kasikia wabunge wa chama chake walikuwa wanatakiwa kuhongwa alot of Millions naye wala hata kushtuka kuwa ana scandal la umeme na watu wanajifanyia watakavyo yeye kabaki S.Africa huyo ndio leo mi nijivunie ndie Rais wa BongoLand over my Dead Body heshima ya yeye kuwa Rais ina shuka every day kukicha sielewi washauri wake ni akina nani.

  My Take : Mr.President doesnt give a damn at all about this TZ ameisha ichoka kabisa anajilazimisha kututalawa na sio kutuongoza na ile kasumba ya kufuata Utawala wa Sheria na Haki huku wakiipindisha sheria kwa manufaa ya wao kubaki hapo madarakani
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli mkuu hili la David Jairo na rushwa kwa wabunge ni scandal of un-imaginable proportions.
  Serikali, mhimili mmoja wa dola, inapowahonga watunga sheria -wabunge, mhimili mwingine wa dola , hapo tuna kuwa na a constututional crisis.
  Nafikiri wengi hawalioni hili.
  Je serikali hiyo hiyo ikiingia na kuhonga mhimili mwingine, mahakama , sijui nchi itaelekea wapi?
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280

  Hiyo unayoongelea sio meli ya Tanzania hiyo ni CCM na unaweza kwenda kupanda meli ingine kama hiyo unaiona haikufai.

  Meli ya Tanzania ni shwari na inahimili mawimbi na dhoruba wala si kama vijahazi.
   
 11. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako bibie weye ni kiruka na njia katika kufikiri.
  Elewa kinchoongelewa kabla ya kuposti na tahadhari yakhe hapa si mchambawima.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Yatakushinda, Soma vizuri weeewe! Rostam serikali inamuhusu nini?
   
 13. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yakheeee!!!
  Yamemshinda JK itakuwa miye?
  Weye Rostam unamsikia tu au una mfahamu?
  King maker huyo!
  Yeye yamemshinda kabwaga manyanga.
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Chama tawala kinaunda serikali na kinaongoza nchi.Si lazima uchangie kama huna la kuchangia,unajaza post zisizo na hoja na unasababisha urefu wa thread na wengine wanaweza kukata tamaa kusoma hata kama thread ina make sense.Tulia unawashwa mno.Aagh.
   
 15. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  jairo alikuwa anafanya kazi za CCM au kazi za serikali . Mwenzae PM wa UK issue ya gazeti imefanaya tu akatishe safari. Yeye issue ya katibu mkuu wake kutoa rushwa tena kwa wabunge anaona powaaa tu.

  Siku moja moja kuwa sensible
   
 16. nzumbe

  nzumbe Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wizara nzima iwajibikeee!!...
   
 17. nzumbe

  nzumbe Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kule South Africa anawataka wawekezaji waje kuwekeza wakati nchi yake ipo gizani!!.. Hai-sense hata kidogo, mwenzake David Cameron alikatiza ziara akarudi nyumbani kushughulikia matatizo ya nchi yake......
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Vita ya MAGAMBA Vs MAGAMBA. Hapa patamu sasa maana Lole kashatangaza kabisa kuwa yeye ni MAGAMBA.

  Ila naona hii inaenda ndani sana na kuwa MAGAMBA vs Muungwana team.
   
 19. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ''eti miye nikae nyumbani, mle mawe! Natafuta chakula na wingu kubwa nikaweke kwenye mabwawa yote yanayozalisha umeme. Tehe! Tehe! Tehe! Tehe!''
   
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Du, mie magamba damu damu.
  Na je FF katumwa?
  Na inasaidia nini kama boti la magamba na serikali yake vinapigwa mawimbi na mtu anachekelea na kudai kuwa unaweza panda meli nyingine kama unaona haikufai?
  Mtu unakutakia mema kweli chama chako?
   
Loading...