JK tukithibisha hili, utakuwa umevunja katiba

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,347
6,471
JK kuzuia/ kuchelewesha huduma kwenye majimbo ya upinzani

Kama JK alivyowaambiwa wabunge wa Chadema wakati akizindua Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano kuwa ndiye Rais na watatoka, watarudi kwake yaani serikalini kutaka msaada.

Katiba inasema:

Ibara ya 13
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi


(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina Fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno “kubagua” halifafanuliwa kwa namna ambayo itazuia serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahususi katika jamii

[Maswali ya Msingi: Hivi JK atakapotoa maagizo kwa viongozi wa maeneo ambayo wananchi wamewachagua wabunge wa Chadema ambao walitoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati JK akihutubia, sio wote akiwemo JK watakuwa wamevunja katiba? Kuwanyima wananchi huduma au maendeleo kwa sababu ya kuwa na maoni tofauti ya kisiasa, sio kuminya demokrasia huko? Hili likitokea na kuthibitishwa basi, JK apitishiwe azimio la kuondolea madarakani ndani ya Bunge]
 
JK hasomi katiba bali hata hilo neno alilisema kwa kukurupuka. Inawezekana hicho kipengere hajakisoma! madamu kimewekwa hapa, basi atafuatilia na kurekebisha. Lakini tunamtaka anapotaka kutoa ufafanuzi wake juu ya uropokaji bila kufuata sheria, aseme hadharani kuwa "nilikosea hapa". Utakuwa ni mfani mzuri. Maana hata nyerere katika speech zake alisema ... Tumefanya makosa, tusifanye makosa sisi ni malaika?...
 
Maswali ya Msingi: Hivi JK atakapotoa maagizo kwa viongozi wa maeneo ambayo wananchi wamewachagua wabunge wa Chadema ambao walitoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati JK akihutubia, sio wote akiwemo JK watakuwa wamevunja katiba? Kuwanyima wananchi huduma au maendeleo kwa sababu ya kuwa na maoni tofauti ya kisiasa, sio kuminya demokrasia huko? Hili likitokea na kuthibitishwa basi, JK apitishiwe azimio la kuondolea madarakani ndani ya Bunge>>>>Mimi nilivyoelewa pale ilikuwa nikupeleka ujumbe kwenye umma kwamba hawakubaliani na yeye kuwa Rais wa JMT kwakuwa zilikiukwa taratibu!Kwa maana hiyo Chadema hawakutaka kuburuzwa na kwakuwa katiba imezuia kuchunguza rais kapatikanaje akisha tangazwa na tume basi hivyo wataendelea kumtambua kama rais aliyeingia madaraka kwa hila na kukiukwa taratibu!
 
Nimeipenda hii, asante sana. Kwani wanachama wa Chadema hawalipi kodi? Pesa za kutoa huduma za serikali zinatokana na ada za wanachama wa ccm? Wananchi wanajua mapato na matumizi ya serikali? Wabunge na madiwani wanajua na wana mamlaka ya kuamua mapato na matumizi ya serkali kuu na wilaya?

Awamu ya kwanza JK alikuwa anaropoka mipasho kwa waliodai haki zao. Alionesha asivyojua sheria hata alizosaini mwenywe. Alionesha alivyokuwa na washauri mbumbumbu. Yeye na watendaji wake ngazi zote wakionesha kutosikiliza vilio vya wananchi.

Unadhani JK wa awamu ya pili ni tofauti na Yule wa awamu ya kwanza? Je tumejiandaaje kumdhibiti yeye na watendaji wake? Unadhani wananchi wanajua haki zao na kwamba wako tayari kuzitetea?
 
Back
Top Bottom