JK touts religion on peace

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
JK touts religion on peace
MKUMBWA ALLY in Rome
Daily News; Monday,October 22, 2007 @00:03

PRESIDENT Jakaya Kikwete said yesterday that social disparities at national and international levels were largely responsible for conflicts spread throughout the world and called for action to redress the situation.

He told an international Inter-religious Congress for Peace in Naples, South Italy, attended by Pope Benedict XVI, that there would be no sustainable global peace before the elimination of violence at national level and among
nations.

"It is unacceptable that with all the wealth available in the world, some people continue to live in abject poverty while others are basking in embarrassingly extravagant luxury," he said.

Disparities among nations were the cause of poverty in the developing world, which was a serious threat to world peace, he added.

"It is obvious that those who are poor and in dire need will continue to struggle for justice and a fairer share of the world's wealth," he explained.

The president told the congress organised by the Community of Saint'Egidio, that religion had the moral authority to prevent and resolve conflicts.

"Religion can be the voice of reason to help nations and people solve their differences peacefully," he said.

Mr Kikwete cited the role of the Community of Saint 'Egidio in peace negotiations in Mozambique and Burundi. However, intervention by religious leaders must be impartial to be effective. "They must be objective even where their followers are party to the conflict," he said.

He stressed that religion, which has massive following, cannot afford to watch as conflicts ravage the world. "It is the duty of every one of us to eliminate violence and ensure that peace, security and stability reign in the world for our common good," he told the congress.

He praised religious leaders in Tanzania for preserving the inter-faith harmony founded by the Father of the Nation, Mwalimu Julius Nyerere, which he said was hinged on the principle of a secular state and freedom of worship.

Mr Kikwete arrived in Paris, France last evening and is today scheduled to address the General Conference of the UN Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO).
 
Posted Date::10/22/2007
Wahadzabe walia njaa, wamkumbuka Nyerere
Na Mussa Juma, Mbulu
Mwananchi

WAHADZABE wanaoishi katika Bonde la Yaeda chini, wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara wanakabiliwa na njaa hivyo maisha yao kuwa hatarini.

Wakizungumza na waandishi wa habari na ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) juzi katika Kijiji cha Sanora, wilayani hapa, Wahazdabe hao walisema kutokana na njaa kali na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, watoto wao wamekumbwa na magonjwa ya kuharisha na kutapika.

Wakizungumza kwa shida huku baadhi yao wananchi hao walimkumbuka hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye walisema alikuwa akiwapatia chakula na kwamba aliwahi kuwatembelea.

Walisema wanaamini kama Nyerere angekuwa hai wasingekuwa kwenye taabu ambayo wanaipata kwa sasa.

Mmoja wa wananchi hao, Tale Mudenda, alisema hivi sasa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika jamii hiyo baada ya kupungua kwa wanyama kutokana na eneo lao kuvamiwa na wafugaji na kusitishwa kwa huduma za kitalii katika bonde hilo.

Alidai kuwa kutokana na upungufu huo wa chakula wazee wawili wamefariki dunia katika kijiji hicho.

�Tunaomba serikali kama kweli ndiyo ya yule Nyerere aliyewahi kuja huku na kutujengea nyumba itukumbuke..,� alisema Mudenda.

Mkazi mwingine, Mandenge Tonga alisema hivi sasa katika eneo hilo hawana huduma zozote muhimu, kama vile huduma za afya, maji na chakula na wanahisi kutelekezwa.

Alisema jamii yao hivi sasa imepungua na kubaki watu 1,800 tu katika bonde hilo na kuonya kuwa kutokana na eneo lao kuendelea kuvamiwa na watu, hasa wafugaji wapo hatarini kupungua zaidi.

�Hatuna huduma za maji hivi sasa, wafugaji wametuvamia, wanafukuza wanyama na pia tunasikia kwamba kuna mwekezaji ameelekezwa kuja kuwekeza huku. Haya yote yanatuathiri na kusababisha tusipate chakula,� alisema Jonga.

Alisema hata mizizi aina ya 'ekwa' na 'mibuyu' ambayo wanaitumia kama chakula imepungua katika bonde hilo tofauti na miaka ya nyuma.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na CCT, Mchungaji John Magafu, alisema kanisa limesikitishwa na hali za wananchi hao.

Alisema anaamini jamii hiyo bila kuwezeshwa kuishi katika maisha bora ipo hatarini kutoweka.

�Leo tulikuja hapa kujionea hali yenu, hasa kutokana na taarifa tulizozipata kupitia kwenye vyombo vya habari, na mimi baada ya kujionea hali halisi nitapeleka taarifa kwa maaskofu na kanisa kwa ujumla ili lifikirie namna ya kuwasaidia,� alisema Mchungaji Magafu.

Hata hivyo, mchungaji huyo alitoa papo hapo msaada wa Sh 100,000 kusaidia jamii hiyo kununua chakula na kuwatibu watu wanne ambao hali zao zilikuwa mbaya kutokana na kukosa chakula.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Naijayaija Koira, alikataa kuzungumzia juu ya janga hilo la njaa katika jamii ya Wahadzabe kwa madai kuwa hakuwa na taarifa za ujio wa ugeni huo.

�Mimi siwezi kusema lolote, mlipaswa kabla ya kuja mnipe taarifa ili niwaandae wataalam wangu wa kila idara, lakini kwa sasa siwezikusema lolote na nina kazi za kiofisi,� alisema Koira.

Jumuiya ya Kikristo Tanzania kwa kushirikiana na dini nyingine wapo katika ziara za kutembelea maeneo yenye rasilimali na migogoro ya kijamii ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi yakiwemo maeneo ya madini, hifadhi na mengine ili kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko rasmi.
 
Kwi kwi kwi kwi!!!! Oh!!! DEAR DEAR ME!!!

Sijui watu wanatoa wapi hata nguvu ya kukaa hoteli za bei mbaya, kuvaa nguo za bei mbaya wakati kuna watanzania wenzao wanakosa
tu hata maji ya kunywa.
 
Nyani haoni Kundule-Sasa Nyani Yupi Hapa anazungumziwa? Tuwe wawazi jamani!!
 
Nyani haoni Kundule-Sasa Nyani Yupi Hapa anazungumziwa? Tuwe wawazi jamani!!


"It is unacceptable that with all the wealth available in the world, some people continue to live in abject poverty while others are basking in embarrassingly extravagant luxury"

Si JK aonyeshe kwa vitendo yeye kwanza? Ukiangalia pesa anazotumia kwenye mizunguko yake, suti anazonunua, wapambe anaozungukwa nao, hizo pesa zingeokoa hao ndugu zetu huko Mbulu wanaokufa njaa, japo kuwapatia maji ya kunywa tu.
 
Kwi kwi kwi kwi!!!! Oh!!! DEAR DEAR ME!!!

Sijui watu wanatoa wapi hata nguvu ya kukaa hoteli za bei mbaya, kuvaa nguo za bei mbaya wakati kuna watanzania wenzao wanakosa
tu hata maji ya kunywa.

Mtanzania, unless I am mistaken by your response, this seems to be in very terrible taste here; considering the plight of these compatriots.
 
"It is unacceptable that with all the wealth available in the world, some people continue to live in abject poverty while others are basking in embarrassingly extravagant luxury"

Si JK aonyeshe kwa vitendo yeye kwanza? Ukiangalia pesa anazotumia kwenye mizunguko yake, suti anazonunua, wapambe anaozungukwa nao, hizo pesa zingeokoa hao ndugu zetu huko Mbulu wanaokufa njaa, japo kuwapatia maji ya kunywa tu.

I take back my earlier comment.
 
Back
Top Bottom