JK: Takrima NGUMU kuikwepa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Takrima NGUMU kuikwepa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijafulia, May 15, 2010.

 1. s

  sijafulia Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete amesema utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi hasa katika kipengele kinachokataza takrima, ni mgumu.
  Rais Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika katika Hoteli ya WhiteSands jijini Dar s Salaam.

  “Tumeendelea kuboresha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, lakini, lile la takrima ni gumu. Mfano katika mkoa wa Kilimanjaro huwezi kuwaita wazee ukazungumza nao bila kitochi,” alisema Kikwete.

  Kitochi ni kipimo cha lita moja ya pombe ya kienyeji aina ya mbege inayotengenezwa mkoani Kilimanjaro.

  Rais aliendelea kusema “Wakati wa kampeni mwaka 2005 nilifika mahali wakawa wananiambia, mzee hili ni jambo la kawaida hata Chadema, CUF wakija wanafanya hivi, hiyo ni sehemu muhimu kwao, huwezi kuwaita wazee bila mbege.”

  Katika kuthibitisha kauli yake hiyo Rais Kikwete alimtaka mmoja wa maaskofu wanaotoka Kanda ya Kaskazini kueleza endapo inawezakana kuwaita wazee wa mkoa huo bila kitochi.

  Askofu huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alimjibu Kikwete "Kwa kweli hili haliwezekani. Hiyo ni sehemu ya maisha ya watu wa Kilimanjaro."

  Baada ya jibu hilo la askofu, ukumbi mzima akiwa Rais Kikwete mwenyewe ulilipuka kwa kicheko na baadaye rais aliendelea kuzungumza na viongozi hao bila kusema nini kifanyanyike ili sheria hiyo iweze kutekelezeka maeneo kama hayo.
  Kwa mujibu wa Rais Kikwete kabla ya kutungwa kwa Sheria hii mpya ya Gharama za Uchaguzi, hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kabla ya mtu kufikiria kugombea, alianza kufikiri kwanza jinsi ya kupata fedha za kununua watu ili wampitishe kwenye kura za maoni.

  “Mwende mkawahubirie watu kuwa wawachague watu wenye nia njema, watakaoweza kuliendeleza taifa, msiengemee chama chochote na pia tuendelee kukumbushana kuyakubali matokeo,” aliagiza Rais Kikwete.
  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete pia alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi hao juu ya tabia inayoanza kujitokeza ya dini moja kuikejeli dini nyingine.

  Alisema ingawa Tanzania ina uhuru wa kuabudi, pale dini yoyote itakapofanya kitendo hicho hadharani, serikali itaingilia kati.

  “Wengine wanasema kuwa tunaingilia uhuru wa kuabudu, lakini siyo kweli, sisi sheria zetu zinasema usikejeli dini ya mwenzako, ukifanya hivyo sisi tunaingilia kati,” alisema Kikwete.

  Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kushirikiana kati ya viongozi wa dini na serikali akieleza kuwa pande hizo zote zina lengo moja la kutaka upendo na maendeleo kwa jamii.
  Alisema wakati mwingine serikali inaweza kufanya jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linaweza kuwakera viongozi hao wa dini na kuwa hali hiyo itakapotokea, viongozi hao wasisite kuwasiliana naye moja kwa moja au kupitia mawaziri.

  “Sisi wote ni binadamu kwa hiyo tutaweza kukosea lakini, nyie mna watu, unaweza kumwambia waziri au mtu mwingine amwambie waziri mkuu kuwa mnataka kuonana naye au aniambie mimi.Pia mnaweza kutumia simu yangu iko wazi muda wote unaweza kunipigia uniambie moja kwa moja,” alisisitiza Kikwete.

  Awali Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Iringa Dk Owdemburg Mdegella alisema kikao hicho kimepitisha maazimio saba ambayo pande zote mbili; serikali na viongozi wa dini wamekubali kuyatekeleza.

  “Kwa kuwa Serikali imeona umuhimu wa kutayarisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kuwashirikisha viongozi wa dini ili kuielewa, kuijadili na kuifikisha kwa waumini; viongozi wa dini tunapongeza na kuhimiza serikali kuwa waaminifu katika kuitekeleza,” alisema Askofu Dk Mdegella.

  Alisoma maazimio hayo kuwa ni serikali kuweka utaratibu maalum wa kukutana na viongozi wa dini mara mbili kwa mwaka na Serikali kudumishe utaratibu wa kutumia mtandao wa viongozi wa dini kwa kupanua wigo wa ushiriki ili kufikisha taarifa sahihi kwa jamii yote.

  Maazimio mengine ni viongozi wa dini washirikishwe mapema katika hatua za awali wakati wa kushughulikia masuala mbalimbali muhimu ya kitafa na viongozi wa dini wasishabikie siasa katika nyumba za ibada.

  Kwa mujibu wa Askofu Mdegella maazimio mengine ni ilani za vyama vya siasa zitayarishwe kwa namna ambayo hazitawagawa Watanzania kwa misingi ya dini, kabila, rangi, jinsi ama eneo analotoka na Serikali na taasisi za dini na zile za kijamii zishirikiane kuandaa mikakati endelevu ya maadili ya kitaifa

  Rais Kikwete alikubali hoja zote zilizofikiwa katika mkutano huo akipendekeza kuwa katika suala la kukutana mara mbili kwa mwaka na viongozi hao, ligawanywe katika mafungu mawili.

  Alisema fungu la kwanza liwe lile la kukutana na viongozi kutoka katika madhehebu na jumuiya mbalimbali kwa nyakati tofauti na lile la pili viongozi wote wa dini na serikali wakutane kwa wakati mmoja.

  Hata hivyo, kama ilivyokuwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo, wahandishi wa habari jana pia hawakuruhusiwa kuingia katika mkutano huo wakati majadiliano hayo yanaendelea.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Mkutano huo, Philip Marmo alikijiuta katika wakati mgumu jana asubuhi baada ya waandishi wa habari kumbana awape maelezo endapo hawatakiwi kwenye mkutano huo.

  Waandishi hao walitaka Marmo aeleze kwanini amekiuka ahadi aliyoitoa mwanzoni kuwa waandishi wa habari wangeruhusiwa kuingia katika mkutano huo na kwanini vyombo vingine viliruhusiwa na vingine kukataliwa. Chombo kilichoruhusiwa katika mkutano huo ni TBC1 pekee.

  Hata hivyo, Waziri Marmo hakutaka kujibu swali hilo akieleza kuwa ana haraka, kitendo ambacho kiliwafanya waandishi wa habari wamzuie kwa nguvu na kuendelea kumhoji.

  Baadaye Marmo aliwaomba waandishi hao kutulia akiwaahidi kwamba wataingia katika majadiliano, lakini pia hakutekeleza ahadi yake hiyo.

  “Jana niliona hali inataka kuchafuka ndiyo sababu nikiwa kama mwenyekiti nikachukua hatua ile ya kuwafukuza. naomba mnisamehe na hao TBC1 walirusha zile habari kimakosa walitakiwa wachukue picha kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi tu,”.
   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  *ASEMA K’LIMANJARO HUWEZI KUWAITA WAZEE BILA KITOCHI CHA MBEGE

  Imeandikwa na Fredy Azzah
  14 May 2010

  [​IMG]

  Rais Kikwete

  RAIS Jakaya Kikwete amesema utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi hasa katika kipengele kinachokataza takrima, ni mgumu. Rais Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika katika Hoteli ya WhiteSands jijini Dar s Salaam.

  “Tumeendelea kuboresha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, lakini, lile la takrima ni gumu. Mfano katika mkoa wa Kilimanjaro huwezi kuwaita wazee ukazungumza nao bila kitochi,” alisema Kikwete.


  Kitochi ni kipimo cha lita moja ya pombe ya kienyeji aina ya mbege inayotengenezwa mkoani Kilimanjaro.


  Rais aliendelea kusema “Wakati wa kampeni mwaka 2005 nilifika mahali wakawa wananiambia, mzee hili ni jambo la kawaida hata Chadema, CUF wakija wanafanya hivi, hiyo ni sehemu muhimu kwao, huwezi kuwaita wazee bila mbege.”


  SOURCE:
  Mwananchi
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  There hev goes again the con artist!!!!!
   
 4. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu Muungwana haishi kustaajabisha ..yaani utie saini sheria kwa mbwembwe kuonyesha ulivyo serious baada ya siku kadhaa unadai sheria hiyohiyo haitekelezeki...! damn
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  hahahahaa
  jk jk jk jk jk jk jk jk jk kikwete

  huwa ananifurahisha sana
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wizi wa urubuni watu ataufanya-atatokaje; lazima atoe kauli- ndio tanzania yetu; ni kama tumelogwa wote na aliyetuloga kafa
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  that was a pr stint, kuwafurahisha wafadhili kuwa tunapambana na rushwa vilivyo
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kweli nilipomsikia jamaa anazungumza na viongozi wa dini jambo hili sikumuelewa hasa akili yake ikoje. Nadhani anao ule ugonjwa wa kusahau sijui wanauita vipi? maana aliye na ugonjwa huu akienda kwa daktari akapewa dawa uisahau pale pale kwa daktari. Bwahahahahahahahaha.

  Na hapa watetezi wa JK mtakuja na lipi tena wandugu. Maana mla Rushwa ameshindwa kuacha kisa ni vigumu kutokula rushwa. Ndio sababu watetezi wa rushwa utawasikia wakidai kuwa hata aingie nani ikulu lazima ale rushwa iliyobatizwa jina zuri la takrima.
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani sijui lini maigizo yataisha tanzania yani kusaini sheria kwa mbwembwe yote maigizo unawaita maaskofu unwawaambia rushwa aiwezikuisha ss kwanini usema utawashugulikia wala rushwa wakati mwenyewe unaibariki.
  kama uliweza kusema utaki kura za wafanyakazi kwa kudai haki zao unashindwa nini kuwaambia hao wazee kuwa uwapi kitochi kama awataki wakunyime kura? ulishindwa nn?
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Serial artful dodger! That's what he is!!!!!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  May 15, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa kweli amenishangaza sana. Kama Rais anakiri haya, sasa sijui sheria yake aliyoisaini kwa mbwembwe itfanikiwa katika utekelezaji wake?
   
 12. M

  Moitalel Member

  #12
  May 15, 2010
  Joined: May 8, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani tufike mahala sasa tuseme basi!!! Tuchague watu wenye uwezo wa kupambanua na kusimamia yale wanayo amini. Soft people, play boys na waswahili will never take as anywhere. Ila wana faida kwa mafisadi kwani hupata nafasi ya kufanya upupu wao. Mafisadi hawa wameonekana kututeka na kutufanya tuamini na kufanya mambo kwa matakwa yao.

  Ni lazima tubadilike na kufanya maamuzi bila ushawishi wa waru katika kufanya maamuzi. Hapo ndipo tutaondokana na watu kama akina jk. Ambao kamwe hawatatuongoza kuelekea maendeleo ya kweli. Watu ambao hawajui dhamana ya nafasi walio nayo katika jamii wanayoingoza
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bwana wanajf huyu ndo alivyo mwacheni alivyo
   
 14. m

  miss annie Member

  #14
  May 15, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi kila siku ninavyosema tupindue serikali/CCM huwa sieleweki...,tumechoka kufanywa wakimbizi ndani ya nchi yetu na wachache wasio na akili.Tanzania bila vita haitawezekana,we have to get rid of ccm no matter what it costs...:angry:
   
 15. m

  mtemi Member

  #15
  May 15, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu mtu anashangaza sana,anaprove kuwa analinda mafisadi
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  What?!!!!! Apete tena?
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mkuu sasa tumfanyeju labda kwangu mimi October namtupilia mbali mana amezidi kwa upuuuuzi huyu :flypig::flypig::flypig:
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha!Funi but there's a point....Unajua watanzania tumezoea kuongozwa kwa maneno,ambayo mara nyingi yamekuwa ni "matupu" Shangazwa kiongozi ikifika wakati wa uchaguzi wanakuwa si "mafala" tena...Ni wasanii at their best! wamefanya na kuongea mambo ya ajabu wakati wa uongozi lakini sasa wakati wa kura hawa tena,wanagonga pale kwenye udhaifu wa watanzania...Sasa kama wana jf wengi tunakubali kuwa ni usanii,na kwamba maybe tumefanyiwa usanii na bado tunaendelea kufanyiwa hivyo,sasa sijui wananchi wa kawaida huko mitaani,nadhani wataona kuwa ni excellent point.

  Mimi naona wale wenye uwezo wa kuchanganua mambo,walitizame hili...Kwenye semina hiyo,wageni waalikwa walikuwa ni viongozi wa dini,kama nilivyosema hapa wiki iliyopita kuwa udini unaweza kuchangia maamuzi ya wananchi wengi uchaguzi ujao,tunaweza kuona kuwa Pinda is not dumb.

  However i have a chalenge,hatujaweza kupata yote yaliyoongelewa kwenye semina,isipokuwa bado ninachallenge hoja ya mh rais kuwa takrima ni ngumu,na akatolea mfano wa wazee wa Kilimanajaro na kitochi,nilipoisoma hiyo heading nikadhani kuwa hana haja ya kuongea na wazee wa Kilimanjaro kama alivyoongea na wale wa Dar kwa sababu ya kitochi,lakini niliposoma nikaona kwamba anafananisha kitochi na rushwa AKA takrima....Nani kamwambia kwenda Kilimanjaro kuongea na wazee plus kitochi ni rushwa? Ama anamaanisha nini?

  Hakuna kabila linalokuabaliana na rushwa,kila kabila ama watu wa maeneo flani wana tamaduni zao amabazo tunaweza kuziangalia kama zina amount to rushwa,na kama thats the case then tunaziweka kwenye kundi la rushwa.....Na kwa taarifa yako mh rais,kama waswahili wananunuliwa kwa pilau,khanga,ndala, AKA malapa,ghahawa or whatever,wachagga kamwe hawanunuliwi kwa kitochi,huo ni utamaduni tu,cha muhimu ni hayo maongezi na wazee hao,wazee wa Kilimanjaro si wajinga,wanatambua usanii,na kama wazee hao watakubaliana na points za yule ambaye hakuwapa kitochi,then usije kudhani kwamba watamchagua mwenye kuwapa kitochi kama watagundua usanii,hamjajiuliza kuhusu perfomance yenu nyie ccm hapo Kilimanajaro licha ya kukiri kuwapa kitochi wazee hao?

  Wakae chini watu wenyekuthink deep,ambao tunao Tanzania,rushwa itenganishwe na tamaduni za wananchi,rushwa is bad period,na rushwa ni rushwa tu,sasa mzee Mkapa nadhani ndo alikuja na hili la takrima,mimi nadhani tusiite takrima,tuite "The culture clause" ambayo itatofautisha kipi ni rushwa na kipi ni utamaduni usio amount to rushwa.Na kama waswahili wataendelea kununuliwa na culture yao ya pilao na khanga,basi hiyo ni juu yao,however ninaamini wanaweza kuelemishwa kuwa wasichague kwa madhumuni hayo.
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata kama ailikuwa akitania, suala hili la takrimna si la utani kabisa! A lot of effort, time and resources were used to make that law so as to deal away with corruption, the malady that can consign the country into a civil war. I am surprised that he cannot see be yond his nose, just like the lot in CCM that he's supposed to be leading!

  Anaonekana anataka kusema kwamba pamoja na sheria hii ya campaign fundsing, takrima inaweza ikatumika!!!!! Hawa CCM ukiwaruhusu hivyo, basi, believe me, this second trime siyo kama wataghushi nyaraka na kuiba mabilioni kutoka a BoT, bali watabreak in in broad daylight!!! Wanahitaji kasababu kadogo tu ka kuwapiku wapinzani wao kwa njia za haramu!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hapo utakuta alipata 'standing ovation' kutoka kwa audience (wtz wenzetu). No challenge!
   
Loading...