JK sio dhaifu kivile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK sio dhaifu kivile

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kavulata, Aug 5, 2012.

 1. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 2,515
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Kuna watu walidhani kuwa Rais Kikwete ni dhaifu, hii ilikuwa wrong interpretation, mambo aliyoyafanya JK ni makubwa matupu na ya hatari kwa Rais yeyote kuyafanya. Kuyataja machache ni pamoja na kukubali katiba ya nchi ifanyiwe mabadiliko, utekelezaji wa zoezi la vitambulisho vya taifa, kuimarika kwa demokrasia nchini, kujenga barabara nchi nzima, kufukua mikataba ya madini, kubadilisha baraza la mawaziri na viongozi wengine mara kadhaa, ujenzi wa UDOM, n.k. mambo yote haya yalimshinda Nyerere, Mwinyi na Mkapa enzi zao, kilimo kwanza. Kigoma enzi hizo ulidhani haiko Tanzania.

  Ila watu wanasema ni dhaifu kwa sababu wananchi wanapenda kwa sasa kiongozi mwenye sifa ya udikteta kidogo ili kunyoosha makosa yaliyofanywa na marais na viongozi wetu waliotangulia. Ndio maana watu wanampenda Dk. Magufuli na bomoabomoa yake ya waliojenga pasipo, Prof. Tibaijuka, Mh. Lyatonga Mrema (enzi zake), Mh. Sokoine (enzi zake), Mh. Amina Chifupa (enzi zake)

  Mwaka 2005, JK alipata kura nyingi sana kutoka kwa wananchi wote bila kujali itikadi zao na kupata urais. Sababu kuu ya kupata kura nyingi wakati ule zilikuwa zilezile za wananchi kupenda kiongozi ambaye ni dikiteta atakayeweza kusawazisha maovu ya viongozi waliopita. JK alipata kura nyingi kwakua alikuwa anaonekana ni kijana, ni mwanajeshi, na ambaye alikuwa anachukia kuuzwa na kubinafsishwa kwa mashirika ya umma na nyumba za serikali. Ukweli huu ulichagizwa na kaulimbiu yake ya Ari Mpya, Nguvu mpya na Kazi Mpya aliyokuja nayo. Hivyo, wananchi walidhani Kikwete kwakutumia sifa hizo akipata urais angefanya kamatakamata ya mafisadi wote (wanafahamika), angerudisha mashirika na nyumba zilizouzwa na Mkapa, angerudisha open spaces zote nchini, angeimarisha michezo nchini kwakuwa ni kijana na mpenda michezo, na hata wanajeshi wenzake wangenufaika zaidi na ujio wake. Kilichotokea, baada ya JK kupata urais ile kamatakamata iliyotarajiwa na waliomchagua haikuonekana kabisa, utadhani hajawahi kuwa mwanajeshi wala mgambo hata siku moja. Na alikuwa anawakataza hata akina Magufuli na Makamba (mkuu wa mkoa) wasiwe madikteta kwa watu waliojenga kinyume na taratibu. Alitumia pesa za wananchi kwa kuwalipa watu wachache waliopatwa na mafuriko kwa kujenga sehemu za mabondeni(zisizoruhusiwa) na kugharamia wamachinga waliokimbia makusudi kutoka wilayani kuja mijini badala ya kutumia pesa hizi katika maendeleo ya ujumla ya wananchi kama kuongeza mishahara ya watumishi, madawati, vitanda hospitalini n.k. Wananchi walikufa moyo zaidi na JK na CCM yake hadi leo hii. Hali hii ya kukata tamaa ilionekana kwenye uchaguzi wa 2010 wakati kura zake ziliposhuka kwa kiwango cha kutisha.

  Lakini wananchi wanataka kiongozi dikteta wakati katiba, kanuni na sheria zetu hazimruhusu Rais kuwa dikteta, rais bora ni yule anayetekeleza matakwa ya sheria hata kama sheria hiyo ni mbaya. Ndiyo maana JK ameridhia katiba iandikwe upya ili wananchi tuamue tunataka rais wa namna gani pia.


  Nchi hii ni kubwa sana kuliko za wenzetu, ina hitaji wanajeshi wengi, walimu wengi, barabara ndefu na nyingi, nguzo nyingi, nyaya nyingi, transfoma nyingi za umeme, vituo vingi vya polisi, shule nyingi, zahanati na hospitali nyingi na watumishi wengi, n.k. Haya yote yanahitaji pesa nyingi za kugharamia huduma mbalimbali.

  Tupeane ushauri kama taifa kuhusu maswali yafuatayo: Hivi wabongo tulipane bei gani kama mishahara (elimu, uzoefu)? Vyanzo vyetu vya pesa viwe vipi? Nani alipe kodi na nani asamehewe? Tutampataje kiongozi safi? Tumfanye nini kiongozi anayeiba mali yetu kwa njia yoyote ile? Tutajuaje kama hela ya kulipana ipo hau haipo hazina? Anayekwepa kodi tumfanyeje? na mwishowe ni nini vipaumbele vyetu mwaka huu, ujao, n,k?

  Haya ndo maswali yatakayompa kiongozi yeyote ujasiri wa kutenda bila kulazimika kutumia utashi wake binafsi.
   
 2. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,929
  Likes Received: 2,994
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wako udhaifu uko pale pale!
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ngoja uje usikie vikaragosi watakavyo bisha, ngoja usikie
   
 4. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  umelipwa bei gani ujaze server hapa  [​IMG]
   
 5. m

  mharakati JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,276
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  udhaifu wa huyu bwana ni pale anaposhindwa kuwachukulia hatua wanaoharibu kazi ya serikali yake na chama chake....hata akivunja baraza la mawaziri mara 10 ndani ya mwaka kama mafisadi na ufisadi wao wana nguvu kwenye serikali yake na chama chake Jk bado ni dhaifu.
   
 6. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 921
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  DHAIFU ni yule aliyeshindwa upadir akaamua kuiba wake za watu.
   
 7. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  TRA wamevuka lengo la kukusanya kodi,lakini serikali haina pesa na deni la nchi linazidi kuongezeka.Huo nao ni udhaifu mwingine.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,913
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  ...na kila Mtanzania ana maisha bora.
   
 9. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwa maoni yangu ni yule aliekabidhiwa nchi na mamlaka akashindwa kuyatumia akabaki kulalamika kuwa wasaidizi wake wamemuangusha,Kama umefanya kila kitu katika uongozi wako na umeshindwa kwa nini usijiuzulu?
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,898
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  yote uliyoorodhesha hapo ndio udhaifu tunaousema.
  kudai nchi ni kubwa ni sawa na kushindwa kujinunulia shati kisa mwili ni mkubwa.
  kuvunja baraza la mawaziri ndio udhaifu mkubwa kabisa kwa sababu kama si udhaifu mwanzo lingekuwa baraza imara.
  ukidai aliacha kuwachukulia wale waliofanya makosa katika tawala zilizotangulia kwani waliotangulia walikuwa chama gani na mbona alilelewa ndani ya huo mfumo toka kijana mdogo.
  ukiongelea kujenga barabara hiyo ni sawa lakini kwa rasilimali tulizo nazo hatuhitajika kukopa ili tujenge barabara piga hesabu alipoingia deni la taifa ilikuwa sh ngapi linganisha na barabara alizojenga na deni la sasa ndipo ujue ni wa kusifiwa au kulaumiwa.

  bila kujibu hoja hizi yote uliyoorodhesha hapo ni madhaifu.
   
 11. peri

  peri JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kama alivyo mwanasiasa/mwanadam mwingine yeyote, jk anamadhaifu yake na mazui yake. Huo ndo uhalisia.
  Hajatokea kiongozi hata m1 duniani wala hatotokea asiyekuwa na madhaifu.

  Nb: udhaifu mwingine wa jk ni kushindwa kuimarisha sekta ya viwanda, tuna import vitu vingi ambavyo tungeweza kuzalisha.

  Ktk mazuri yake ni kuimarisha sekta ya afya na elimu nchini. Ktk kipindi chake tuna wasomi wengi kuliko hapo awali.
   
 12. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,190
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Once DHAIFU, always DHAIFU.

  Kikwete ni dhaifu pale alipolekewa muswaada wa kukataza wafanyakazi wasichukue mafao yao hadi miaka 55 huku akijua life span ya mTZ ni miaka 35 now.

  Ni dhaifu pale anapoweka utaratibu wa kulihutubia taifa kila mwisho wa mwezi halafu 80% ya hotuba hizo ni kulalamika tu kwamba mimi siwezi, mnanionea na kuongea kama mwanamipasho vile eti "Mimi sielewi wanaosema hivi na hivi. sielewi serikali ifanyeje", badala ya kuongea mipango, mikakati, mafanikio (kama yapo), changamoto, what nect, etc.

  Once DHAIFU, always DHAIFU.
   
 13. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,906
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ni kazi sana kumtetea mtu dhaifu
   
 14. h

  hacena JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haki ya Mungu hauko makini wewe ni dhaifu, Kikwete alipogombea urais 2005 hakuwa kijana, alishakuwa mzee,
   
 15. b

  bdo JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,676
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  aaak Kavulata, hivi kweli wewe upo hai? mwaka 2005 aliiba kura na 2010 mianya ya wizi ilionwa kwa macho mangavu ila 2015 utaona maajabu
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 25,252
  Likes Received: 7,073
  Trophy Points: 280
  kwani wakati anaomba urais hakujua ukub wa wa Tanzania? tuache kutetea ujinga
   
 17. h

  hoyce JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,113
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huu ndio udhaifu wa kushindwa kujenga hoja ya mezani, ukakimbilia vioja
   
 18. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 897
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mh Raisi Kikwete hatutakaa tumsahau, thread hii nitaitafuta tena baada ya 2015 maana naamini maneno yangu ni ya uhakika na kweli. Kama hutumii ushabiki kupitia magazeti na siasa za msimu, na una uwezo wa kutafakari kwa undani, pamoja na mapungufu ambayo katika Afrika nchi zote zina changamoto, Raisi kuna mambo ambayo hakuna mwingine ameweza kuyafanya. Uhuru wa maoni na mawazo tulio nao, itatuchukua muda, kwakuwa viongozi wengi si wavumilivu. Angekuwa Mzee Ben, hata jamii Forums isinge-survive I doubt, Mfano mmojawapo tu ni leo hii si wanasiasa wa CCM au wa Upinzani wana nafasi kubwa ya kujadili wanayoyataka. Maswala mengine ya kiuchumi n.k ni menig nadhani hayatoshi hapa kuyasema. Na naomba nikosoe jambo moja, mambo haya hajafanya Kikwete, ila ameyasimamia yafanyike, kusema Kikwete amefanya nini ni upotoshaji na unatumika sana kwumanipulate watu wasiotumia muda wao kutafakari.

  Nasikitishwa na baadhi majibu yaliyopo humu, hasa yale yasiojadili hoja, natumaini hawa sio wanachama wa chama chochote cha siasa, maana wanaonyesha wanakerwa, ila usipo sema hoja yako huna tofauti na wale ambao hatutaki kabisa kuwapa dhamana ya kuongoza, kwakuwa hatuwezi kungozwa na watu wanaotumia ushabiki watatupeleka pabaya. Ila mungu atuweke hai, kama chama kingine kitachukua serikali 2015 badala ya CCM, hawa washabiki wote wa chama hiki ninawapa mwaka mmoja, hutaamini watakachosema kuhusu serikali itakayokuwa madarakani. Ninaona wanaofikiri kwa kutumia hisia sio halisia wala hawana muda wa kutafakari. Ninawasoma humu wanaofanya ushabiki, na hata hawajui yaliyomo kwenye vyama hivi. Mfano political idiology ya CCM ni "Ujamaa na Kujitegemea"??, Sera ya CHADEMA ni??? UDP?? TLP?? CUF?? na vingine... kuzitekeleza ni juu ya wanachama kusimamia Chama na kuhakiksiha kinaowapa dhamana wanasimamia waliokusudia. "People's Power (naamini hii ni sera ya msimu ya kisiasa kwa ajili ya kampeni kama ilivyo ya CCM ya "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania")"??? Political idiologies huwa zinakuwa base ya economy na hivyo basi jamii imara. Wakati mwingine vyama huongezea issue juu ya idiology mfano kuhamasisha na kusimamia mabadiliko ya sera ya ardhi (imilikiwe na uma au watu binafsi) au haki za kundi fulani la watu muhimu mfano uhuru wafugaji kulinda mila zao na desturi kwa ajili ya hiostoria na kuwapa nafasi ya kumiliki maeneo yao ya malisho kimila bila kuingiliwa na mtu yeyote, au elimu na afya jinsi itakavyosimamiwa. Lakini cha msingi kabisa ni idiology inayoguide hizo issue nyingine.

  Tufike mahali tuone kabisa unaamua kuwa mwanachama wa chama hiki kwakuwa unaamini idiologies zake za ki-siasa Mfano za Ujamaa, Kibepari, au ki-komunisti. Na Kampeni za kuongoza nchi zinajikita kwenye mfumo na kuwahamasisha watu kwa kutumia idiologies zao.
   
Loading...