JK: Sina mpango kuvunja Baraza

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
JK: Sina mpango kuvunja Baraza

*Asema hizo ni fikra za watu binafsi
*Awambia waandishi ikibidi atarekebisha
*Aomba subira kwa TRL, ATC na TANESCO
*Aahidi mahujaji hawatahangaika tena

Na John Mapinduzi

RAIS Jakaya Kikwete amesema hana mpango wa kuvunja wala kubadili Baraza lake la mawaziri katika siku za karibuni.

Aliyasema hayo juzi Ikulu, Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari, kutathmini miaka miwili tangu Serikali yake ilipoingia madarakani, Desemba mwaka juzi.

Akijibu swali kuhusu tetesi za kufanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri karibuni, Rais Kikwete alisema taarifa hizo hazina ukweli na huenda zinatokana na mawazo ya watu binafsi wanaotaka kufanyika kwa jambo hilo.

"Ni uvumi kama tutakuwa na haja tutabadili au ni matakwa ya watu," alisema.

Akizungumzia ukubwa wa Baraza hilo ambalo baadhi ya wananchi wanadai linafanya kazi chini ya matarajio ya wengi, Rais Kikwete, alisema liliundwa kutokana na mahitaji na kama ni kufanyiwa marekebisho, suala hilo ni la baadaye na si sasa. "Tuliliunda kulingana na mahitaji, tutaona mbeleni tufanye marekebisho," alisema.

Ripoti ya REDET

Aliisifu ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) ambayo iliainisha masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Nne na kubainisha kulegalega kwa utendaji wa Baraza la Mawaziri, huku likimwachia mzigo yeye.

Alisema ripoti hiyo ni nzuri, kwani imekusanya maoni ya wananchi mbalimbali na Serikali inayatumia kama kioo kujitazama na kuona wapi penye kasoro ili kufanya marekebisho.

"Ripoti ya REDET ni nzuri, imekusanya mawazo ya wananchi mbalimbali, watu walitoa mawazo yao barabarani, sokoni, n.k., sisi kama Serikali tunatumia kama kioo kujitazama kuona wapi kuna kasoro na kujirekebisha," alisema

Rushwa kubwa

Akijibu swali kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kupambana na rushwa kubwa, Rais Kikwete alisema Serikali imepania kutokomeza tatizo hilo, lakini inakwamishwa na mikanganyiko iliyopo kwenye suala lenyewe.

Alisema mapambano dhidi ya rushwa kubwa yanahitaji mtandao mkubwa na pesa za kutosha kufuatilia na kubaini ukweli wa matatizo hayo, vinginevyo mambo hayo yataishia kuwashuku watuhumiwa bila kuwa na ukweli.

Kuhusu kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada, alisema uchunguzi wake unahitaji muda wa kutosha na jambo hilo linaendelea kushughulikiwa.

Ahadi ya maisha bora

Rais Kikwete alisema tofauti na mawazo ya baadhi ya watu kuwa ahadi hiyo imeshindwa kutekelezeka katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake, kilichofanyika ni kuweka misingi imara kwenye maeneo muhimu na kitakachofuata ni utekelezaji kuelekea mwaka 2010.

"Ahadi ni za miaka mitano, tumeweka misingi, sasa tunapoelekea mwaka 2010 tunaweka matofali. Kuna maeneo mengi yamefanyiwa kazi, huduma za afya, barabara, maji.

"Tutawaonesha Watanzania wapi tutafikia. Tunatayarisha Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi, kuanzisha zahanati zaidi na kuhakikisha huduma hiyo inapatikana chini ya umbali wa kilometa tano kwa wananchi na kuimarisha barabara za mikoa na wilaya kwa kiwango cha lami," alisema.

Serikali kuhamia Dodoma

Akijibu swali lililohoji kasi ya Serikali yake kuhamia Dodoma katika kipindi cha miaka miwili, Rais Kikwete alisema jambo hilo lipo na ni sera inayoendelea kutekelezwa.

Kuhusu kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuanzisha miji mipya mbali na wa sasa, Rais Kikwete alisema Serikali yake imeona umuhimu wa jambo hilo na imechukua hatua mbalimbali ukiwamo mradi wa upimaji viwanja kwenye maeneo mbalimbali.

Hata hivyo, alisema pamoja na jitihada zilizofanywa na Serikali mkoani Dar es Salaam na miji mingine kugawa maeneo ya makazi katika maeneo mbalimbali, ilisahau kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda yanayoweza kusaidia 'kusambaza miji'.

Reli ya Kati

Akizungumzia huduma duni kwa usafiri wa reli ya kati baada ya lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kukodishwa, Rais Kikwete aliwatetea wawekezaji hao na kusema kuwa ni mapema mno kufanyika marekebisho makubwa ndani ya shirika hilo, kwani ni kipindi kifupi tangu ukodishaji huo ufanyike.

"Tusiwasukumie lawama, hawawezi kufanya miujiza, tuwape muda ndio kwanza wameanza kwa mazingira ya sasa. Tunafuatilia kwa karibu utekelezaji chini ya programu ya menejimenti mpya.

Shirika la Ndege Tanzania

Akijibu swali kuhusu huduma duni zinazotolewa na Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ambazo katika siku za karibuni, zilisababisha usumbufu mkubwa kwa mahujaji waliokuwa wakienda kuhudhuria Ibada ya Hija, Rais Kikwete alilitetea na kubainisha kwamba kwa sasa lina ndege moja tu, kilichotokea, lilikubali kuchukua dhamana ya kuwatafuatia usafiri mahujaji hao.

"Tunachofanya ni kuhakikisha tatizo walilopata wakati wa kwenda halitokei wakati wa kurudi. Awali tulianza na ndege tisa, tukabaki na ndege mbili. Sasa ndio tumeanza programu ya umiliki, tumeanza na mwanzo mzuri," alisema.

Uuzaji nyumba, Mgogoro Z'bar

Akijibu swali lililotaka kujua hatua iliyofikiwa na Serikali katika kurudisha baadhi ya nyumba zilizouzwa kwa watumishi wake, Rais Kikwete alisema shughuli hiyo inakwenda vizuri na Serikali inaendelea kuainisha nyumba hizo.

Kuhusu hatua iliyofikiwa katika suala la muafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, alisema suala hilo linaendelea vizuri na anaamini litamalizika salama.

Utendaji TANESCO

Akijibu swali kuhusu kusuasua kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na hoja ya kutaka libinafsishwe na kuruhusiwa wawekezaji wengine kwenye sekta hiyo, Rais Kikwete alisema:

"Fikra zetu zipo kwenye majibu mawili, kuwa na kampuni tatu tofauti, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Ililetwa Net Group ili irekebishe mambo pale TANESCO. Kazi iliyopo ni kulijenga Shirika lenyewe... TANESCO ndiyo yenye 'monopoly' wazalishe."

Mikataba ya madini

Kuhusu madini, alipoulizwa kwamba Serikali inaonekana kupuuza kauli na mwito wa wananchi kusitisha mikataba ya madini, Rais Kikwete, alisema baadhi ya watu wanaongea na kuonesha kana kwamba Serikali haijali maslahi ya nchi.

Alisema alipokuwa Afrika Kusini Machi mwaka huu, aliongelea suala la mikataba ya madini na lilizua maneno mengi.

" Huku nchini tayari nilikuwa nimeunda tume ya kupitia mikataba ili tuone jinsi gani inaweza kutunufaisha. Sisi hatuna mitaji, teknologia na rasilimali watu lakini tuna maliasili. Kama tunataka kufaidika na madini yetu ni lazima tuangalie namna ya kuyachimba tena kwa manufaa,"alisema.

Rais aliendelea kusema kwamba kwa hali iliyopo sasa, mikataba inamlinda zaidi mwekezaji. Hata hivyo alisisitiza kwamba si kosa la wawekezaji bali ni tatizo la mikataba yetu.

Alipotakiwa kueleza hatua ya wachimbaji wadogo wadogo kunyang'anywa ardhi na kupewa kampuni kubwa, Rais alisema kwamba shughuli ya uchimbaji madini inatawaliwa na sheria na si kama kilimo.
Alisisitiza kuwa mchimbaji anayesema eneo fulani ni lake athibitishe kisheria na asidhulumiwe.

"Pale tunapowakaribisha wawekezaji basi tuwe tayari kuwapa na ardhi ya kufanyia shughuli zao. Hatuwezi kumruhusu mwekezaji aje na tusimpe ardhi ya kufanyia kazi. Sasa atakapokuja tunategemea nini kama hatujampa ardhi?" alihoji.

Kwa wawekezaji wanaojenga mahoteli sehemu za ufukweni, Rais Kikwete, alisema kisheria hakuna mtu anayemilikishwa fukwe badala yake anapewa kiwanja kilicho karibu na fukwe.

"Hakuna ramani inayochorwa kufikia ufukweni kabisa, fukwe si mali ya mtu," alisisitiza.

Source: Majira
 
Hapa wananchi tumepigwa bao la kisigino, hakuna mabadiliko wala marekebisho, labda baadae ikikaribia mwaka 2010.
Kama wananchi hawatabadilika na kuamka na kuitetea/kuilinda nchi, maendeleo ya kweli TANZANIA itabakia kuwa hadithi za alfu ulela zitaendelea hadi ardhi yote itakaponyakuliwa na hao wawekezaji uchwara.
Nahisi ninaweza kuungana na 'kigoma' kujitenga.
 
Ukisoma maswali ya waandishi wa habari na majibu ya Mheshimiwa utagundua kitu kimoja kwamba alipewa maswali marahisi na majibu yaliandaliwa. Sina hakika kama waandishi makini wanaweza kumwacha atoe majibu marahisi kiasi hicho na wakaridhika bila ya kumbana na maswali ya nyongeza ili atoe majibu ya kueleweka. May be ndiyo maana kuna tetesi kwamba wahandisi wa habari walioitwa Ikulu walichaguliwa kutoka baadhi ya vyombo vya habari na mwaliko haukuwahusu wahariri wa nyumba zote za habari.

Kitendo cha kutumia wingi kwenye kubadilidilisha baraza la mawaziri kinatia shaka kwamba na kuonyesha wazi kwamba lilipoundwa alishirikiana na EL na mabadiliko yoyote lazima EL ahusike na hivyo uwezekano wa kumtema EL ni mdogo sana!
 
Hapo muungwana kaamua "kukata ngebe"! Na waandishi wamezidi woga, ni wepesi mno kuridhika na majibu rahisi.
 
...hakuna kitu hapo ni usanii kwa kwenda mbele,i have this funny funny idea ya JK doesnt care wala hatishiki na hana wasiwasi kwa sababu he knows anakubalika kwa wakubwa zake Marekani na Uingereza,yupo pale kumaliza miaka yake 10 na kuangalia maslahi ya watu wake sio kina duka la kaya na huyu JK anaonekana not very smart na hana idea nini maana ya kuwa President zaidi ya kukaa ikulu tuu,ndio maana ukimwangalia sasa hivi kanenepa sana
 
Keil,
Hii ya maswali kuandaliwa mapema ni hulka ya Mwungana. Hawezi kufanya mazungumzo/mahojiano na waandishi wa habari bila kupewa maswali in advance.
 
Hapa wananchi tumepigwa bao la kisigino, hakuna mabadiliko wala marekebisho, labda baadae ikikaribia mwaka 2010.
Kama wananchi hawatabadilika na kuamka na kuitetea/kuilinda nchi, maendeleo ya kweli TANZANIA itabakia kuwa hadithi za alfu ulela zitaendelea hadi ardhi yote itakaponyakuliwa na hao wawekezaji uchwara.
Nahisi ninaweza kuungana na 'kigoma' kujitenga.

Mimi bado naamini mabadiliko ya Baraza yanafanyiwa kazi na yatatangazwa. Nadhani JK hakutaka kuwapa "wasiwasi" mawaziri wake - idea ni kuwafanya wasi-lose concentration katika wajibu wao wa kila siku.
 
Rais J. M. K. I. Kwete ni mbabaishaji kabisa. Haya ndiyo malipo tunayopata Watanzania kwa kutofanya tathmini ya kutosha kuwajua watu wanaoutuomba kura zetu.
 
Ningetamani jamaa akutane na waandishi wa habari kama Stephen Sackur wa BBC hardtal na yule dada Zadawi wambane kwa maswali ya hapo kwa papo
 
JK: Sina mpango kuvunja Baraza

*Asema hizo ni fikra za watu binafsi
*Awambia waandishi ikibidi atarekebisha
*Aomba subira kwa TRL, ATC na TANESCO
*Aahidi mahujaji hawatahangaika tena

Na John Mapinduzi

RAIS Jakaya Kikwete amesema hana mpango wa kuvunja wala kubadili Baraza lake la mawaziri katika siku za karibuni.

Aliyasema hayo juzi Ikulu, Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari, kutathmini miaka miwili tangu Serikali yake ilipoingia madarakani, Desemba mwaka juzi.

Akijibu swali kuhusu tetesi za kufanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri karibuni, Rais Kikwete alisema taarifa hizo hazina ukweli na huenda zinatokana na mawazo ya watu binafsi wanaotaka kufanyika kwa jambo hilo.

"Ni uvumi kama tutakuwa na haja tutabadili au ni matakwa ya watu," alisema.

Akizungumzia ukubwa wa Baraza hilo ambalo baadhi ya wananchi wanadai linafanya kazi chini ya matarajio ya wengi, Rais Kikwete, alisema liliundwa kutokana na mahitaji na kama ni kufanyiwa marekebisho, suala hilo ni la baadaye na si sasa. "Tuliliunda kulingana na mahitaji, tutaona mbeleni tufanye marekebisho," alisema.

Ripoti ya REDET

Aliisifu ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) ambayo iliainisha masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Nne na kubainisha kulegalega kwa utendaji wa Baraza la Mawaziri, huku likimwachia mzigo yeye.

Alisema ripoti hiyo ni nzuri, kwani imekusanya maoni ya wananchi mbalimbali na Serikali inayatumia kama kioo kujitazama na kuona wapi penye kasoro ili kufanya marekebisho.

"Ripoti ya REDET ni nzuri, imekusanya mawazo ya wananchi mbalimbali, watu walitoa mawazo yao barabarani, sokoni, n.k., sisi kama Serikali tunatumia kama kioo kujitazama kuona wapi kuna kasoro na kujirekebisha," alisema

Rushwa kubwa

Akijibu swali kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kupambana na rushwa kubwa, Rais Kikwete alisema Serikali imepania kutokomeza tatizo hilo, lakini inakwamishwa na mikanganyiko iliyopo kwenye suala lenyewe.

Alisema mapambano dhidi ya rushwa kubwa yanahitaji mtandao mkubwa na pesa za kutosha kufuatilia na kubaini ukweli wa matatizo hayo, vinginevyo mambo hayo yataishia kuwashuku watuhumiwa bila kuwa na ukweli.

Kuhusu kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada, alisema uchunguzi wake unahitaji muda wa kutosha na jambo hilo linaendelea kushughulikiwa.

Ahadi ya maisha bora

Rais Kikwete alisema tofauti na mawazo ya baadhi ya watu kuwa ahadi hiyo imeshindwa kutekelezeka katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake, kilichofanyika ni kuweka misingi imara kwenye maeneo muhimu na kitakachofuata ni utekelezaji kuelekea mwaka 2010.

"Ahadi ni za miaka mitano, tumeweka misingi, sasa tunapoelekea mwaka 2010 tunaweka matofali. Kuna maeneo mengi yamefanyiwa kazi, huduma za afya, barabara, maji.

"Tutawaonesha Watanzania wapi tutafikia. Tunatayarisha Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi, kuanzisha zahanati zaidi na kuhakikisha huduma hiyo inapatikana chini ya umbali wa kilometa tano kwa wananchi na kuimarisha barabara za mikoa na wilaya kwa kiwango cha lami," alisema.

Serikali kuhamia Dodoma

Akijibu swali lililohoji kasi ya Serikali yake kuhamia Dodoma katika kipindi cha miaka miwili, Rais Kikwete alisema jambo hilo lipo na ni sera inayoendelea kutekelezwa.

Kuhusu kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuanzisha miji mipya mbali na wa sasa, Rais Kikwete alisema Serikali yake imeona umuhimu wa jambo hilo na imechukua hatua mbalimbali ukiwamo mradi wa upimaji viwanja kwenye maeneo mbalimbali.

Hata hivyo, alisema pamoja na jitihada zilizofanywa na Serikali mkoani Dar es Salaam na miji mingine kugawa maeneo ya makazi katika maeneo mbalimbali, ilisahau kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda yanayoweza kusaidia 'kusambaza miji'.

Reli ya Kati

Akizungumzia huduma duni kwa usafiri wa reli ya kati baada ya lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kukodishwa, Rais Kikwete aliwatetea wawekezaji hao na kusema kuwa ni mapema mno kufanyika marekebisho makubwa ndani ya shirika hilo, kwani ni kipindi kifupi tangu ukodishaji huo ufanyike.

"Tusiwasukumie lawama, hawawezi kufanya miujiza, tuwape muda ndio kwanza wameanza kwa mazingira ya sasa. Tunafuatilia kwa karibu utekelezaji chini ya programu ya menejimenti mpya.

Shirika la Ndege Tanzania

Akijibu swali kuhusu huduma duni zinazotolewa na Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ambazo katika siku za karibuni, zilisababisha usumbufu mkubwa kwa mahujaji waliokuwa wakienda kuhudhuria Ibada ya Hija, Rais Kikwete alilitetea na kubainisha kwamba kwa sasa lina ndege moja tu, kilichotokea, lilikubali kuchukua dhamana ya kuwatafuatia usafiri mahujaji hao.

"Tunachofanya ni kuhakikisha tatizo walilopata wakati wa kwenda halitokei wakati wa kurudi. Awali tulianza na ndege tisa, tukabaki na ndege mbili. Sasa ndio tumeanza programu ya umiliki, tumeanza na mwanzo mzuri," alisema.

Uuzaji nyumba, Mgogoro Z'bar

Akijibu swali lililotaka kujua hatua iliyofikiwa na Serikali katika kurudisha baadhi ya nyumba zilizouzwa kwa watumishi wake, Rais Kikwete alisema shughuli hiyo inakwenda vizuri na Serikali inaendelea kuainisha nyumba hizo.

Kuhusu hatua iliyofikiwa katika suala la muafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, alisema suala hilo linaendelea vizuri na anaamini litamalizika salama.

Utendaji TANESCO

Akijibu swali kuhusu kusuasua kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na hoja ya kutaka libinafsishwe na kuruhusiwa wawekezaji wengine kwenye sekta hiyo, Rais Kikwete alisema:

"Fikra zetu zipo kwenye majibu mawili, kuwa na kampuni tatu tofauti, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Ililetwa Net Group ili irekebishe mambo pale TANESCO. Kazi iliyopo ni kulijenga Shirika lenyewe... TANESCO ndiyo yenye 'monopoly' wazalishe."

Mikataba ya madini

Kuhusu madini, alipoulizwa kwamba Serikali inaonekana kupuuza kauli na mwito wa wananchi kusitisha mikataba ya madini, Rais Kikwete, alisema baadhi ya watu wanaongea na kuonesha kana kwamba Serikali haijali maslahi ya nchi.

Alisema alipokuwa Afrika Kusini Machi mwaka huu, aliongelea suala la mikataba ya madini na lilizua maneno mengi.

“ Huku nchini tayari nilikuwa nimeunda tume ya kupitia mikataba ili tuone jinsi gani inaweza kutunufaisha. Sisi hatuna mitaji, teknologia na rasilimali watu lakini tuna maliasili. Kama tunataka kufaidika na madini yetu ni lazima tuangalie namna ya kuyachimba tena kwa manufaa,”alisema.

Rais aliendelea kusema kwamba kwa hali iliyopo sasa, mikataba inamlinda zaidi mwekezaji. Hata hivyo alisisitiza kwamba si kosa la wawekezaji bali ni tatizo la mikataba yetu.

Alipotakiwa kueleza hatua ya wachimbaji wadogo wadogo kunyang'anywa ardhi na kupewa kampuni kubwa, Rais alisema kwamba shughuli ya uchimbaji madini inatawaliwa na sheria na si kama kilimo.
Alisisitiza kuwa mchimbaji anayesema eneo fulani ni lake athibitishe kisheria na asidhulumiwe.

"Pale tunapowakaribisha wawekezaji basi tuwe tayari kuwapa na ardhi ya kufanyia shughuli zao. Hatuwezi kumruhusu mwekezaji aje na tusimpe ardhi ya kufanyia kazi. Sasa atakapokuja tunategemea nini kama hatujampa ardhi?" alihoji.

Kwa wawekezaji wanaojenga mahoteli sehemu za ufukweni, Rais Kikwete, alisema kisheria hakuna mtu anayemilikishwa fukwe badala yake anapewa kiwanja kilicho karibu na fukwe.

"Hakuna ramani inayochorwa kufikia ufukweni kabisa, fukwe si mali ya mtu,” alisisitiza.

Source: Majira

Nimesoma maneno ya Rais Kikwete, maoni yangu ya haraka kwake…..

Sijafurahishwa na maneno ya ijumaa ya leo katika siku ya kutimiza miaka miwili ya utawala wako, nilidhani ungetangaza hatua thabiti za kurejesha matumaini ya wananchi na serikali yako katika mstari kwenye ministerial issues- lakini major national questions are yet to be answered! Nadhani washauri wako wanakushauri vibaya; kama matokeo ya REDET ni sahihi kabisa kwamba umaarufu wako ni mara mbili ya Baraza lako basi hatua zozote za kujaribu kulisaficha baraza hilo kwa PR Gimmicks zitakushushia umaarufu zaidi na wewe mwenyewe. Mr President, you can’t swim with them, you will stink and sink with them.

Naona washauri wako wamekushauri ufanya smooth operation! Someni vizuri public opionion na alama za nyakati, hicho sicho umma unatarajia. Sababu za umma kutoridhishwa na Kikwete- Mosi, Ahadi ya Maisha Bora kutotimia(naoana washauri wako wamekushauri ianze PR Gimmick ya kwamba ni mapema sana, na kwamba Maisha Bora hayaji kama Manna toka Mbinguni). Pili; kutotimiza ahadi(naona washauri wako wamekushauri kwamba ifanyike PR Gimmick kwamba wewe ni Muungwana Mtu wa Vitendo hivyo utatekeleza ahadi zako zote); Sababu ya Tatu ni Kuchagua Viongozi dhaifu/wabovu( hapa ndipo mzizi wa mambo ulipo!). Suluhisho lake si hii njia unayopitia hivi sasa; toka Julai kulikuwa na muda wa kutosha sana wa kuwafanyia tathmini, sasa ilikuwa ni wakati wa hatua, kadiri unavyochelewa kuchukua hatua Matumaini ya wananchi yanazidi kupungua na Imani inaanza kujengeka kwamba wewe u mmoja wao).

Opinion polls zinaonyesha kwamba Matumaini ya wananchi juu yako yako inverse proportional na elimu ya wananchi; wale waliofika chuo kikuu ndio hawana imani zaidi na wewe kuliko wale ambao hawakwenda shule kabisa(ambao ndio walio wengi). Hii ina maana kwamba watu wengi wa kawaida wahajui uhusiano wako wewe na Baraza lako la Mawaziri pamoja na kuwekwa kwenye list of shame. Wanapeleka kila lawama kwa viongozi wengine na kukupa benefit of doubt. Sasa kadiri unavyochelewa, utaendelea kuwaamsha walio lala…

Sasa ingia ndani zaidi kwa nini wananchi hawana imani na serikali yako? Sababu ni tofauti kidogo na kwa nini hawana imani na wewe- serikali yako inaonyesha kushindwa kufuatilia utekelezaji, serikali yako inalaumiwa kwa kuwa na ufisadi na kushindwa kutumia vizuri rasilimali za nchi; serikali yako inalaumiwa kwa kushindwa kutoa huduma bora za msingi za kijamii.

Haya ni mambo ambayo yote yanahitaji vitendo na si defense through PR Gimmicks. Uamuzi wa kuunda Kamati ya Madini, Uamuzi wa Kuunda Kamati ya Richmond; Uchunguzi wa BOT; Uamuzi wa kupeleka Kesi ya Rada Mahakamani; Uamuzi wa kumtoa Severe na Wenzake; Uamuzi wa Balali Kujiuzulu; yote haya- yamepunguza mjadala mkali wa umma lakini hayajabadili public opinion- in fact yanatengeneza sustained opinion kwamba serikali inalindana na wewe Mheshimiwa Rais unashindwa kuchukua hatua! Maoni haya yakigeuka kuwa msimamo wa umma mtizamo hautabadilika hata siku utakapoamua kuchukua hatua! It will be too late. The only way is to break this spiral of effect!

Anzia na Baraza la Mawaziri- ukianza kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya hapo Taasisi nyingine za umma zitafuata maana kila moja ina ‘ka-skeleton kake kwenye kabati’. PCCB imeathiriwa na ile ripoti kanyaboya ya Richmond-wananchi wamepunguza imani nao; mahakama imeathiriwa na mchakato Kesi ya Ditopile wananchi wakaanza kuihoji; Bunge limeathiriwa na kupitisha bajeti iliyongeza gharama za maisha na kumfukuza Zitto Kabwe-wananchi wamepoteza imani na uwingi wa wabunge wa CCM; orodha ya Taasisi inaendelea. Na katika kipindi cha miaka miwili ilijitokeza pia mijadala mingine ambayo pamoja na kuizima kinamna bado inafukuta: Mpasukuko wa kisiasa Zanzibar, Suala la Mahakama ya Kadhi, Suala la Katiba Mpya- orodha ni ndefu kwa kweli. Lakini ni jinsi gani kila mmoja atajirekebisha inatemea ni jinsi gani wewe utarekebebisha mhimili wa serikali(hususani baraza lako la mawaziri).

Tendo la kuunda Kamati ya Madini ama ya Richmond pekee hayajaweza kuwasafisha wakina Lowasa na Karamagi! Huu ni wakati wako wa kuchukua hatua kama Amiri Jeshi Mkuu- ni wakati wa kumwondoa Lowassa na Kuvunja Baraza la Mawaziri. The Karamagi’s are too many and they are tainted beyond painting. The more you be with them the more people confirm that you deserve to be in the “list of shame”; the more you will take a spade for a spade not a big spoon; the more people will take you in the “list of fame”! Nchi inahitaji dira na vitendo.
 
JJ
 
Sijafurahishwa na maneno ya ijumaa ya leo katika siku ya kutimiza miaka miwili ya utawala wako, nilidhani ungetangaza hatua thabiti za kurejesha matumaini ya wananchi na serikali yako katika mstari kwenye ministerial issues- lakini major national questions are yet to be answered!

JJ

Kuna maneno nimeruka kidogo hapo-nilitaka kumaanisha interview ya Rais imejikita katika kufanya PR Gimmick on ministerial issues instead of responding to lingering national questions! Nadhani ya wizara angeziachia wizara. Angejikita katika masuala machache yenye kutoa Dira na Uongozi wa Vitendo kuelekea Tanzania tunayoitaka katika miaka michache ya utawala wake iliyobaki na pengine kujenga misingi ya miaka mingi ya baadaye ya Taifa letu hata kama yeye hatakuwa Rais tena wakati huo

JJ
 
JK:
Utendaji TANESCO

Akijibu swali kuhusu kusuasua kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na hoja ya kutaka libinafsishwe na kuruhusiwa wawekezaji wengine kwenye sekta hiyo, Rais Kikwete alisema:

"Fikra zetu zipo kwenye majibu mawili, kuwa na kampuni tatu tofauti, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Ililetwa Net Group ili irekebishe mambo pale TANESCO. Kazi iliyopo ni kulijenga Shirika lenyewe... TANESCO ndiyo yenye 'monopoly' wazalishe."

Source: Majira

...tatizo kubwa kama la umeme ambalo linaathiri maendeleo ya nchi hili ndio jibu lake,inakatisha tamaa sana jinsi muungwana anavyofanya kazi na sijui kama tatizo la umeme litaisha kwa majibu kama haya
 
Nilisema kuwa hatuvunji isipokuwa tunapangua na kupanga safu mpya ,hii ndio CCM kama mko na tamaa za kuvunja natumai itakuwa sasa hazipo,Muungwana amesema tunarekebisha tena kama makelele yakizidi ndio tunapangua.CCM Oyee !!!
 
Hao mawaziri wanaovurunda wana mkataba na JK kukaa hapo hadi 2010, ili waweze kurudisha walichokitoa mtandao na wapate 1000% faida.
Sisi tulie tu!
 
Nilisema kuwa hatuvunji isipokuwa tunapangua na kupanga safu mpya ,hii ndio CCM kama mko na tamaa za kuvunja natumai itakuwa sasa hazipo,Muungwana amesema tunarekebisha tena kama makelele yakizidi ndio tunapangua.CCM Oyee !!!

...mwenyewe unajiona insider kumbe mpiga ngoma tuu,they dont even know you
 
Mh! Majibu ya muungwana yanashangaza sana. Masuala nyeti kama TANESCO na ATCL anatoa majibu marahisi sana! Sijaona jibu la kiutendaji kuhususuluhisho la huu umeme wetu wa kuazima.
Nini kinamfanya awe mzito kuibadili baraza la mawaziri? Ama walichangia pakubwa sana katika kampeni za mwaka 2005, ndio sababu anakuwa mgumu kuwamwaga?
Inashangaza sana.
 
...LOL I guarantee he says the Economy is doing great and mgawo is no more. You can't believe anything this dope says.
 
I guess the guy is even weaker than Mzee Ruksa. The bad news are: We are still to leave with these for another 8 years. Watanzania inabidi kujadili jinsi ya kumuondoa 2010 na sio yeye kurekebisha kitu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom